mtafuta-maisha
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 1,982
- 2,934
Hii story inaanzia hapa Wakala wa kifo alivyowatesa polisi katika kesi ya aina yake
Tarehe 27, mwezi 8 mwaka 2003.
Ilikuwa ni muda wa mapumziko kwa ajili ya chakula katika kituo kidogo cha polisi cha Melbourne, kachero wa kitengo cha kupeleleza mauaji Bwana Johnny Lawson akiwa na mwenzake, inapigwa simu ya dharura ikimtaka afike kwenye Hoteli ijulikanayo kama Trimland iliyoko katikati ya mji wa Melbourne na mpigaji alikuwa akihitaji uwepo wa polisi kwenye hiyo hoteli akidai kuna tukio la mauaji limetokea hotelini hapo. Hoteli ya Trimland iko Maili zipatazo 14 kutoka Brevard ambapo siku mbili zilizopita Kachero Carlos alikumbana na tukio la kumkamata kijana aliyekuwa akiendesha gari hovyo hovyo.
Kachero Lawson anamwambia kachero mwenzake mwamama Borne Renk waelekee kwenye eneo la tukio bila kufahamu wanaenda kukutana na tukio moja la mauaji mabaya ambayo hawakuwahi kushuhudia na kukaa kwenye vichwa vyao kwa kipindi kirefu sana. Walipofika kwenye eneo la hoteli hiyo walikuta askari waliotangulia kufika wamekwisha zungusha utepe wa njano kuashiria kuwa eneo lile haruhusiwi mtu asiyehusika kukatisha kuna shuguli za kipolisi zinaendelea.
Mtu wa kwanza kukutana naye alikuwa mlinzi wa hoteli hiyo ambaye Lawson alimuuliza ni nini kimetokea, naye alimjibu kwamba mfanyakazi anayehusika na usafi alienda kusafisha chumba alipofungua mlango aliona damu sakafuni akatoka amekimbia na kumjulisha mlinzi ambaye aliamua kuwapigia simu polisi.
Pia pale kulikuwa na kachero mzoefu wa Melbourne ajulikanaye kwa jina la Scott Dwyer ambaye alikuwa ametangulia kufika kabla ya akina Lawson. Kwa pamoja wote watatu wanakubariana waanze kufanya uchunguzi kuanzia nje ya chumba wakikusanya chochote muhimu na kutazama mazingira kwa uangalifu huku wakielekea ndani. Hivyo upelelezi uanze nje kuelekea ndani na walianza mara moja kabla hata ya kuingia ndani ya chumba hicho.
Walipoingia ndani baada ya kumaliza uchunguzi wao nje, walistaajabu kuona chumba kikiwa katika hali ambayo hawakutegemea. Kwanza hakukuwa na sanduku au begi lolote maana walitegema huenda waliokuwemo walikuwa wasafiri au wageni hvyo walikuwa na mabegi lakini hakukuwa na begi lolote, pia hakukuwepo nguo mahali popote kwenye chumba kile, pia taulo na matambara mengine yatumikayo bafuni hayakuwepo.
Kufikia hapo hawakuwa wameona hata uwepo wa mwili wala mtu yoyotye chumbani mle mpaka Scott alipogeuka na kutazama kitandani ndipo aliona doa kubwa la damu, huku kukiwa na mashuka na blanketi kubwa kitandani. Scott aliondoa Blanketi, na chini yake kulikuwa na shuka limelowa damu alipoliondoa ndipo walipigwa butwaa. Alikuwa umelazwa mwili wa kijana mdogo wa Kihispania ambaye alionekana akiwa kwenye umri wa miaka 20, mwili haukuwa na nguo hata moja. Moja kwa moja wakampigia daktari wa polisi aje kuutazama mwili huo kabla haujaondolewa hapo kitandani.
Kwao haikuwa habari ngeni mwili kukutwa hotelini lakini mara nyingi uwa mtu anakuwa kafariki kwa matatizo ya kiafya au kujiua mwenyewe lakini kwa hali iliyvyoonekana ilionekana wazi kuwa marehemu kauawa tena kifo cha kinyama na ilichukua muda mrefu kutoa uhai wake. Baada ya kumgeuza waliweza kuona kuwa alikuwa kaumizwa shingoni, na kwenye mikono na miguu kulikuwa na alama ya kuonyesha kuwa alikuwa kafungwa kwa kamba mikononi na miguuni maana alikuwa kachubuka na mwekundu maeneo hayo. Na daktari alipomkagua macho yake aligundua kwamba mishipa ya damu machoni mwake ilikuwa imepasuka jambo lililoashiria kuwa alikabwa pia.
Mwili wa marehemu ulikuwa una majeraha ya kukatwa katwa kwa kisu chenye ncha kai, jumla ya majeraha ya kukatwa yalikuwa nane na hii ilionyesha kuwa muaji alikuwa akimtesa kabla ya kumuua. Pia ilionekana kwamba marehemu kabla ya kuawa alilawitiwa, japo muaji hakuacha ushahidi wakumkamata ila waliweza kupata baadhi ya nywele za sehemu za siri za huyo aliyemuingilia kinyume na maumbile zikiwa zimebaki kwenye sehemu ya nyuma ya mwili wa marehemu.
Kwa jinsi marehemu alivyouawa, polisi hawakuwa na shaka kwamba muaji alikuwa na hasira na marehemu na walihisi uenda walifahamiana na ka kumtesa vile marehemu kulikuwa na ugomvi na kisasi baina yao hivyo muaji alikuwa na hasira sana juu ya marehemu. Ila jambo moja ambalo polisi liliwastaajabsha ni kwamba kila kitu mle ndani kilikuwa kimepangusa kuanzia kuta za chumba, viti, meza kabati chooni na kila kitu kilikuwa kimepanguswa hivyo hawakufanikiwa kupata alama za vidole wala kitu chochote ambacho kingeweza kuwasaidia kupata DNA ya mhusika isipokwua zile nywele za sehemu za siri ambazo walikuwa wanaomba Mungu ziweze kufaa kwa ajili ya kuchakata DNA.
Jambo lililowashutua polisi ni kwamba, waligundua muuaji alikuwa ni mtaalamu wa kile anachofanya ndiyo maana hakuacha ushahidi na walihisi huenda siyo mara yake ya kwanza kuua na haitokuwa mara yake ya mwisho kuua, ataua tena.
Japokuwa muaji alijitahidi kusafisha eneo lote, ila kitengo cha CSI waliweza kupata alama ya sole ya kiatu cha mguu wa kushoto bafuni, ambapo walifanya utaratibu wa kuchukua alama hiyo na kuifadhi kama ushahidi katika upelelezi wa mauaji hayo.
Wakati makachero wakiendelea na upelelezi wao mara Borne analeta taarifa inayowapa mwanga kidogo wapi waanzie. Taarifa hiyo inasema kwamba kuna kachero mwenzao ameombwa kufanya upelelezi juu ya kadi ya benki iliyoibwa kutoka Tennessee na imegundulika ilitumiwa maeneo ya Melbourne siku ya Jumapili karibu na mauaji yalipotokea. Na zaidi ni kwamba aliyeiba kadi hiyo aliacha ameua watu wawili ambao walikuwa wanandoa. Mauaji hayo yallikuwa yametokea umbali wa maili 800 Kaskazini mwa Melbourne katika mji wa Bartlett huko Tennessee, siku tano zilizopita yani tarehe 22, mwezi wa 8 mwaka 2003.
Moja kwa moja jioni ya siku hiyo Kachero Lawson aliamua kuwasiliana na kituo cha polisi cha Tennessee, na kuwataarifu kuwa anapeleleza kisa cha mauji ya kijana mmoja ambacho nahisi kinahusiana na kisa kingine cha mauji kilichotokea huko Tennessee. Lawson alimueleza kachero aliyeongea naye kwenye simu kuwa ameelezwa kuwa kadi ya benki ya wahanga hao imetumika kwenye eneo karibu na hoteli walipokuta maiti ya kijana huyo.
Kachero huyo alimtaarifu Lawson kuwa wahanga wa mauaji hayo walikuwa wanandoa ambao umri wao ulikuwa umewatupa mkono na walikuwa wanajulikana kama Bwana Clerence James aliyekuwa na umri wa miaka 82, na mkewe Bi Lilian aliyekuwa na umri wa miaka 64. James na mkewe walikuwa wanajishughulisha na shughuli ya kurekebisha samani za watu kwenye eneo la Bartlett Tennessee. James na mkewe walikuwa wanafahamika kwa watu wote wa Barlett na James alikwua mtu wa watu alikuwa akipendwa sana na watu wa eneo hilo. Kila Jumapili yeye na mkewe walikuwa lazima wahudhurie ibada na katika siku ambazo hawakuwa na kazi walipenda kujumuika na familia yao hasa wajukuu na watoto wao.
Tarehe 23 mwezi wa 8 mwaka 2003, mtoto wao wa kike ajulikanaye kama Magret Coleman anaamua kwenda kutazama kuna tatizo gani baada ya kuwa kila akimpigia simu mama yake inaita tu bila kupokelewa. Alipofika alikuta nyumba iko kimya na mlango wa mbele umeegeshwa tu haujabanwa kabisa hivyo aliingia ndani huku akiita jina la mama yake. Lakini ukimya uliokuwa mle ndani ulimtisha na aksikia sauti moyoni ikimsihi atoke nje apige simu polisi.
Kachero aitwaye Marsey ndiye anafika nyumbani kwa James na kuingia ndani kwa tahadhari kubwa huku nyuma akifuatiwa na kachero mwenzake, na ndipo wanapogundua tukio la mauaji ya kutisha mle ndani.
Trevoir ambaye alikuwa kachero mwenzake Marsey anaamua kuelekea chumbani wakati Marsey akielekea sebuleni, TYrevoir kuingia chumbani anakutana na mwiliwa Lilian ukiwa umelala chini kwenye dimbwi la damu na kichwa chake kikiwa kimekatwa imebaki kidogo tu kitenganishwe na kiwiliwili. Trevoir anatoka nje akiwa na Marsey na Lilian aliyekuwa anawasubiri nje anamuuliza kama wamempata mama yake, Trevoir anamjibu kuwa hawajaweza kumtambua ila kuna mwili wa mwanamke humo ndani. Lilian anaangua kilio na kuwauliza je baba yake wamemuona ndipo wanaamua kurudi ndani na mara hii wanaeleke kwenye sehemu iliyojengwa mahususi kwa ajili ya kuhifadhia gari na huko wanakuta mwili wa James na hapo ndipo wanagundua kufikia hapo wanachunguza kesi ya mauaji.
Muda huo wote kachero Lawson alikuwa akisikiliza maelezo ya kachero mwenzake aliyekuwa akizungumza naye kupitia simu na kuajribu kuyaringanisha na tukio la kesi aliyokuwa akiifanyia upelelezi. Kutokana na maelezo aliyopewa aliambiwa marehemu walikuwa wakatwa koromeo kwa kisu na kukatwa katwa kwenye miili yao. Pia aliambiwa kwamba walikuwa wamefungwa mikono na miguu kabla ya kuawa, pia aliambiwa kuwa sehemu kadhaa za nyumba mhusika alikuwa amezipangusa kiasi kwamba hakuacha alama za vidole wala DNA. Mambo haya yalikuwa yanashabihiana na jinsi yule kijana alivyouawa na Lawson alihisi moja kwa moja kwamba huenda mhusika ni yule yule.
Japo matukio yalioonekana kushabihiana lakini lengo la muaji katika matukio hayo mawili lilionekana kutofautiana. Tukio la Tennessee ilionekana mhusika alitenda mauaji hayo katika harakati za uporaji na ndiyo maana aliiba baadhi ya vitu vya thamani na kadi ya benki wakati tukio alilokuwa akipeleleza Lawson lilionyesha kuwa halikuhusiana na upioraji. Pia kachero aliyekuwa anazungumza naye alimwambia ana video kutoka kwenye kamera za usalama zilizo kwenye kituo kimoja cha kujaza mafuta ya gari ambapo mhusika alitumia kadi hiyo kujaza mafuta kwenye gari lake, hivyo kama nahitaji anaweza kumtumia hiyo video muda huo huo. Lawson aliomba atumiwe hiyo video mara moja na alitumiwa.
Baada ya kupokea video na kuifungua, kama zilivyo kamera nyingi za ulinzi za wakati huo hazikuwa zikirekodi matukio katika kiwango chenye ubora hivyo Lawson alifanikiwa kuona gari la huyo aliyetumia kadi kujaza mafuta lakini hata hivyo hakuweza kuona vitu muhimu kama namba ya gari kitu pekee alichoweza kung’amua ni kwamba ile gari ilikuwa ya muundo wa Ford wa miaka ya 90.
Bonyeza link hapo chini litatokea tangazo sekunde 5 kisha utaona next bonyeza next kuendelea sehemu ya tatu
Earn money on short links. Make short links and earn the biggest money - shorte.st