Secret admirer; hii ipo jamani?

Nadhani FL, hupaswi tu kumshangaa. Hebu tueleze baadaye wewe ulimsaidiaje? au utamsaidiaje au ndo unaendelea kumshangaaa!!

Kweli mie sijamsaidia lolote mpaka sasa ndo naona huu ushauri wa wadau najaribu kufikiria cha kufanya :A S 39:
 
huyo ni mental case aisee, ni obsessive disorder

duh

...hahaha,...halafu kaka mbona hukumsaidia mawazo Boss hapa https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/65771-hivi-hii-ni-normal-au-nina-tatizo.html

...Hapana bana, siyo mental disorder. Sijui asili ya huyo dada lakini inaelekea anauasili wa kibantu. Ili kudumisha mila, desturi na tamaduni haikubaliki binti kumtongoza mwanaume.
Sasa nyie mlitegemea angefanya nini zaidi ya hapo, maana kama kujipitisha keshajipitisha kuliko Fire engine na ving'ora vyake, huenda hata kimavazi alishavunja sana makabati.
Huyo kaka lazima alijifanya mpofu, either kwakuwa hana kabisa hisia nae au alikuwa anapata mixed messages.
 
FL Am standing to be corrected, kama ni secret admirer ina maana huyu kaka hajui kama huyo binti kampenda so anafanya mambo yake vile anavyofikiri kuwa ni sawa, kama kweli huyo dada yuko penzini kiasi hicho si asonge tu front akamueleze huyo secret admirer wake kuwa amevumilia ameshindwa so anatangaza nia!
 
Mpendwa katika bwana itabidi unipe mbinu mbadala hivi akikataliwa si ndo atakufa huyu dada ..mapenzi gani haya ya kuuguzana .??
Itamsaidia sana tu.Atafanikiwa kumtoa moyoni mwake hata kama kwa maumivu ili apishe nafasi kwa mwingine atakaempenda.Hata hivyo itabidi umkanseli kwanza kuwa kukataliwa sio mwisho wa maisha na kwamba Mungu ana Mpango maalumu kwa ajili ya maisha yake ikiwa ni pamoja na kumpa mwezi sahihi atakaempenda bila masharti.
 
Kweli mie sijamsaidia lolote mpaka sasa ndo naona huu ushauri wa wadau najaribu kufikiria cha kufanya :A S 39:

...mwambie haikuwa rizki yake ndio maana akayaona hayo. Kilichomliza siku hiyo ingekuwa kilio chake cha kila siku. Akiacha alinacha zake, atawaona 'secret admirers' wanaotamani yeye awe la'aziz wao vile vile.
 
FL Am standing to be corrected, kama ni secret admirer ina maana huyu kaka hajui kama huyo binti kampenda so anafanya mambo yake vile anavyofikiri kuwa ni sawa, kama kweli huyo dada yuko penzini kiasi hicho si asonge tu front akamueleze huyo secret admirer wake kuwa amevumilia ameshindwa so anatangaza nia!

Duuh nadhani hofu yake kubwa ni zile aibu za kike za kuanza ,na tatizo linakuja akianza akakataliwa si ndo atakuwa anaona aibu hata kupita mbele ya huyo broda
 
...mwambie haikuwa rizki yake ndio maana akayaona hayo. Kilichomliza siku hiyo ingekuwa kilio chake cha kila siku. Akiacha alinacha zake, atawaona 'secret admirers' wanaotamani yeye awe la'aziz wao vile vile.

Thanks Mbu kwa hiyo hapa binti inabidi ajaribu kuondoa hisia zake juu ya kaka huyo na kusonga mbele na maisha
nadhani hii itakuwa njema kwake ..nitaongea naye yote na pia baada ya muda nitamwambia pitie hapa Ndani
 
FL labda hii inaweza kumsaidia, nakumbuka wakati nasoma Pugu Boys ( si mnajua kule kuona flowers ni adimu sana) tulikuwa tunakuja tambaza kusoma tuition wakati wa likizo, sasa pale Tambaza kulikuwa na Flowers ( wadada) za kutosha tu, kwa hiyo sisi tukiwa darasani mabinti wakipita basi mimacho kodoooo! sasa tulikuwa na mwalimu mmoja anaitwa Mkandawile aliposhtukia issue akatupa mbinu mbadala ambayo ndio naipropose huyu binti aitumie kwani ilifakiwa kwa wengi wetu. Alituambia kwa kuwa possibility ya kuwapata wale mabinti ilikuwa ndogo na ili tusiumie tukiwakosa ni bora tu "kuwa resolve" maana yake ilikuwa ni bora uanze kutafuta kasoro kwa binti huyo ili utafute sababu ya kutomtamani tena! Kwa hivyo namimi namshauri huyu binti aanze kuangalia upande wa pili wa huyu jamaa,mfano anaweza anza kwa kusema " kwanza jamaa mwenyewe miguu mibovu, aaaa jamaa mwenyewe j hajui kuvaa, na sababu zingine. mwisho wa siku atamuona jamaa ana kasoro kibao so atampotezea kimtindo !
 
Thanks Mbu kwa hiyo hapa binti inabidi ajaribu kuondoa hisia zake juu ya kaka huyo na kusonga mbele na maisha
nadhani hii itakuwa njema kwake ..nitaongea naye yote na pia baada ya muda nitamwambia pitie hapa Ndani
Hapo kwenye RED hawezi kuondoa hisia bila kuujua ukweli.....maana nnawezekana mkaka wa watu wala hana hili wala lile....We mwambie bana "Avunje Ukimya".... kama "mbwai mbwai tu bana".....hakuna kitu kizuri cha kua na amani kama kuujua Ukweli ingawa sometimes unauma....
 
sidhani kama amevuka kikomo...hapo ndio hisia zake zilipofikia mwisho....japo hata mimi namlaumu muda wote huo miaka miwili mbona mingi sana, alitakiwa ndani ya miezi sita awe anammiliki mkaka

Huyo Dada ahitaji msaada wa kidakitari; kwani hata akim-miliki huyo kaka , ikitokea wamekosana dada huyo aweza fanya madhara. Hiyo ni kupenda overdrive!!!
 
Mi ninaye hapa naona tatizo ndo hilo hilo hebu nisaidieni wadau:A S confused:
 
Hapo kwenye RED hawezi kuondoa hisia bila kuujua ukweli.....maana nnawezekana mkaka wa watu wala hana hili wala lile....We mwambie bana "Avunje Ukimya".... kama "mbwai mbwai tu bana".....hakuna kitu kizuri cha kua na amani kama kuujua Ukweli ingawa sometimes unauma....

...hehe, keshamuona ana kiss na mwanamke mwingine...kiashiria kwamba huyo mwanaume yupo kwenye uhisiano tayari. Halafu binti wa watu 'ajivue' heshima yake kumtongoza bwana wa watu? hapana bana. Ilishasemwa "you are a genius mpaka utapofungua mdomo wako!",... Truth hurts bana, anaweza kuumizwa kuliko alivyoumizwa unless unataka dada wa watu aingie kwenye utatu 'usio mtakatifu.'
 
Mi ninaye hapa naona tatizo ndo hilo hilo hebu nisaidieni wadau:A S confused:

...LOL, kaka ndio kusema una Secret-Crush isiyosemeka kwa mrembo fulani hapo, au ni wewe unapewa Green-lights :humble: na ving'ora mfululizo na not-so-secret admirer?
 
Kuna Binti hapa kaniacha hoi mie labda na nyie atawashangaza
Huu ni mwaka wa pili sasa yuko kwenye hiyo secret admirer na kaka mmoja ,
Kila siku binti anategeshea amuone huyu kaka ndo apande gari aliyopo,Lunch time anategea mida ya huyo kaka kwenda lunch ndiona yeye anaenda amekuwa kama mtumwa wa penzi na kusema hawezi.
Cha kushangaza jana tumeenda kwenye Party moja,,,,Binti akiwa anaenda Toilet kamkuta huyo secret admirer wake amekumbatiana na mdada mmoja wa haja wanakiss
Kaja kuniaga huku anabubujikwa chozi eti anaenda home hawezi kuendelea na partyl,leo hajafika kazini namuuliza kulikoni kanipa mkasa kamili...
Kumwambia amesema hawezi tena sasa anauguza majeraha ya mapenzi
Hii imekaaje wadau?:A S 39::A S 39:

Masikini, dada wa watu, pole yake kuna rafiki yangu mmoja yeye alishawahi kunisimulia kuhusu secret admirer wake, huyo shoga yangu ana - supermarket jamaa alikuwa mteja wake, sasa eti akihisi harufu ya perfume ya huyo secret admirer wake yeye hooooooooooooooooooooooooi, lakini hamwambii, ila kusema ukweli tulivyopata fursa ya kumuona tukiwa pamoja dada alinionyesha huyo kaka kwa kweli alikuwa yuko good looking sana tu. Mbaya zaidi dada alifanya jitihada za kumwonyesha kaka lakini naona mwenzake hakuelewa kabisa. Sasa ikatokea kukawa na harusi ya mdogo wake na rafiki yangu, dada akampa kadi ya mwaliko, kweli kaka akahudhuria sherehe na mchuchu wake, looooh dada karibia arudi nyumbani maana alibadilika ghafla, akawa mwekundu, uchangamfu wote ukamwisha, aliugulia maumivu, akapoteza mwelekeo, jamaa naye hakuwa na hiana wakati wa kuondoka akajakumuaga na kumtambulisha. Ila story ya huyu shosti wangu mwishowe walikuja kupendana lakini pia hawakudumu. Kwa sababu kumbe jamaa alikuwa ana mke mwingine zaidi ya yule aliyemtambulisha shotsti wetu. Haya sasa ku-admire vitu vya wenye navyo.
 
Ndiyo matatizo ya ku-fall in love na mtu. Mahusiano hata yakifanikiwa kuanza huwa hayadumu kwa vile mtu anaye-fall in love hufikia kipindi cha kutoka kwenye hilo blanketi au - tuseme - ulevi na kuwa mwenyewe kabisa. Hapo ndipo yale "mapenzi" aliyoingia nayo hukuta hayapo tena. Na ndo unakuwaga mwisho wa uhusiano.

Mi nashauri huyo dada avumilie tu. Ni suala la muda - hicho ya kipindi cha kumpenda jamaa kupindukia kitapita tu. Tena atashangaa kitakapopita ataanza kujiuliza maswali mengi tu: "hivi kitu gani kilinifanya niwe kichaa kwa jamaa"!? Ataishia kucheka; na huko mbeleni atawasimulia marafiki na hata wajukuu zake hiyo experience. Naona atulie, ajikaze, asimwambie jamaa kwani jamaa ana mtu wake. Halafu mara nyingi mtu aki-fall in love kwa mtu yule aliyependwa huwa haitikii mwaliko wa kupendwa (naongea kwa uzoefu wangu). Huwa kunakuwa na kutofautiana sana kwa vitu mbalimbali kati ya wawili hao. Ni ajabu lakini ndivyo ilivyo. Utakuta jama hana mpango hata chembe!
 
Is she a virgin? Mbona anakuwa na aibu hivyo? Mwambie kuna njia za mwanamke kutupa ndoano. Wanaume sisi tunategeka kirahisi kwa kutazama tu ... kwa hiyo mwambie avae nguo za kimtego mtego halafu ajipitishe kwa huyo secret admirer. Au kama ni mtu wa maadili basi ajaribu njia ya maongezi ... kama vile kujifanya anaulizia kitu / jambo fulani la kizushi.

Huyo mwanamke mwingine aliyemkuta naye si tatizo, anaweza kumpindua kama kweli anamtaka.
 
Back
Top Bottom