Secret admirer; hii ipo jamani?

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,374
Kuna Binti hapa kaniacha hoi mie labda na nyie atawashangaza .

Huu ni mwaka wa pili sasa yuko kwenye hiyo secret admirer na kaka mmoja.

Kila siku binti anategeshea amuone huyu kaka ndo apande gari aliyopo,Lunch time anategea mida ya huyo kaka kwenda lunch ndiona yeye anaenda amekuwa kama mtumwa wa penzi na kusema hawezi.

Cha kushangaza jana tumeenda kwenye Party moja,,,, Binti akiwa anaenda Toilet kamkuta huyo secret admirer wake amekumbatiana na mdada mmoja wa haja wanakiss

Kaja kuniaga huku anabubujikwa chozi eti anaenda home hawezi kuendelea na partyl,leo hajafika kazini namuuliza kulikoni kanipa mkasa kamili...

Kumwambia amesema hawezi tena sasa anauguza majeraha ya mapenzi

Hii imekaaje wadau?

:A S 39::A S 39:
 
Duuuu..........duniani kuna mambo kweli. Namuonea huruma sana huyo mdada. Mwambie tu kuwa it wasnt meant to be.
 
heheheh kanishangaza sana............maana nilijua wanaume ndio wenye mtindo wa hivi!

FL wewe hujawahi kupata kaji-stalker au ndio hiyo admirer kwani?

waweza kuona mwanzo mchezo lakini mwisho ukachukukia!

huyo bishosti mwambie amwambia jamaa ...........ama akataliwe ama akubaliwe sio kuishi katika fantasy kama hivyo
 
huyu dada kajitesa jamani, analia nini sasa?

alikosea sana bora angetafutaga njia ya kumwonesha jamaa kuwa anam-feel kabla ya haya, huwezi jua labda angem-win.

pengine hajachelewa basi amwambie huyo secret admirer wake ukweli......
 
ooh masikini...mimi hajanishangaza....nimejaribu kumuelewa.....hii huwa ipo sana
 
Hata wanaume wanayo sana hii ya secret admirer.

Kwa mfano wakati wa lunch time unaweza kwenda kula mahali ili umuone tu kimwana ambaye anakuvutia sana maana unajua anapenda kula mahali hapo baada ya kumuona mara mbili tatu (hata kama hupapendi sana mahali hapo) au kwa kufuatilia nyendo zake lakini baada ya muda inabidi uchangamke na kutupa ndoano yako, lakini kabla hujafanya hivyo ukigundua binti ana njemba basi reaction yako si ya kama ya huyo binti.

Ana matatizo fulani huyo katika kichwa chake. Mwambie hajachelewa lakini anaweza kabisa kumpindua huyo dada mwingine lol! na yeye awe mshika usukani.
 
hii kitu huwa ipo sana, tatizo ni kwamba kimaumbile binti huwa ni ngumu kuweza kujieleza kwa mwanaume vile anavyo umia juu ya kwamba amempenda, labda awe jasiri wa hali ya juu, lakini pia anaona hawezi kueleweka mbele ya huyo jamaa kwa kuhisi ataonekana malaya, lakini ni kitu cha kawaida kuwepo kwenye jamii, hata wanaume wapo wenye kuumia kimya kimya, hata kufikia kujenga wivu pale wanapowaona wale wanaumia juu yao wako na wenzi wao.

Hapo maadamu kaona kwa macho yake juu ya hilo, nadhani hapaswi kujiumiza ama kumwambia huyo jamaa juu ya hali yake kwake maana ataonekana anamharibia yule binti alomkuta naye, kwa sababu kuna mijanaume mingine huwa haikatai bwana atawakusanya wote na kuwapangia zamu tu.

Dunia yenyewe iko wapi ya kuzungukiana?
 
This is pathological na inabidi huyo dada atafute msaada fast. Tabia kama hizo zinaweza kukupelekea kuwa stalker au hata serial killer.... This is quite disturbing.
 
kweli haya mambo yapo sana tu!tatizo linakuja pale utakapoamua kumtolea uvivu huyo secret admirer atakuchukuliaje?kwa huyo dada itabid ajitahid kumfuta akilini huyo secret admirer wake coz kashashuhudia ana m2!!!!!la sivyo akubali kuzungukiwa...........
 
FirstLady1 unaweza kumsaidia mwenzako kwa kufikisha ujumbe kwa huyo bwana anayekuwa admired.

By chance unaweza kukuta wote wawili ni secret admirers wa each other na wanaogopana tu, ukitekenya tu mambo msweno.
 
This is pathological na inabidi huyo dada atafute msaada fast. Tabia kama hizo zinaweza kukupelekea kuwa stalker au hata serial killer.... This is quite disturbing.
senki very much theodora... historia ya serial killers wengi ni obsessive compulsive disorders!!! secret admiration ina kikomo na huyu dada amevuka hicho kikomo

DN
 
senki very much theodora... historia ya serial killers wengi ni obsessive compulsive disorders!!! secret admiration ina kikomo na huyu dada amevuka hicho kikomo

DN

sidhani kama amevuka kikomo...hapo ndio hisia zake zilipofikia mwisho....japo hata mimi namlaumu muda wote huo miaka miwili mbona mingi sana, alitakiwa ndani ya miezi sita awe anammiliki mkaka
 
Ndiyo ndiyo Preta, bhaelezee in wat tym? So u mean ungekuwa ww ndani ya miez 6 ushaweka chombo kwny milki yako, huh!!
 
sidhani kama amevuka kikomo...hapo ndio hisia zake zilipofikia mwisho....japo hata mimi namlaumu muda wote huo miaka miwili mbona mingi sana, alitakiwa ndani ya miezi sita awe anammiliki mkaka
you are pretta adamant when it comes to these things aren't you??! kinda sweet and scary altogether though!! lol
 
Wengine tuna uso za chuma...kumilikiwa inataka muda ati sio hiyo miezi sita ya kukadiria
 
NAANZA KUONA OPPERTUNITIES ZA KIJASIRIAMALI HAPA KWENYE JUKWAA LA MAPENZI..FL- mwambie huyo binti asipate taaabu..mie najitolea kum-imbishia mpaka mshkaji aingie laini..sema issue ni pale mshkaji atapo hit n run...naona huyo rafikiyo ATAJIUA MAANA ATAKUWA AMEMWAGWA na mnavyojua kulia eti mmechezewa basi ni balaa tupu...mwambie anipatie particularz za muhusika nianze kumlia mingo za kufa mtu...ndani ya 2weeks lazma wapate dinner pamoja... ila atalipia gharama zangu za hiyo consultancy nitayomfanyia.
 
Back
Top Bottom