Kweli kabisa mimi ilishanitokea mtu ananipigia simu anasema anataka kuongea na mimi ana kitu cha kuniambia, anauliza kama nina muda, nikamwambia mimi nipo busy aongee mwisho wa siku eti ameniona siku nyingi sana ananipenda ila anaogopa kuniambia eti nikipata muda nichagua sehemu tukutane.., alafu mwisho akajichanganya akasahau eti kwani unafanya kazi wapi / unafanya nini ?, (sasa mtu ananifahamu na kunipenda na ameniona siku nyingi alafu hajui nafanya nini ?), mwisho wa siku nikagundua kwamba hawa watakuwa wale wale wanatafuta namba za watu na wanaomba mkutane sehemu ili waweze kukuvamia na kukuibia (ukizingatia sio vigumu kupata simu ya mtu). Au hata ukikutana nae kesho yake mtu akija na kusema yule ni mke wangu ?
Nadhani hii njia ni hatari sana na ni kujitafutia matatizo ya bure cha kufanya jamaa ni ku-block namba ya huyo so called binti atachoka mwisho wa siku atatafuta mwingine wa kumuibia