Second round application

Second round application

thomas_360

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2015
Posts
1,458
Reaction score
1,436
Napenda kuchukua fursa hii kuweza kuchangia kile ambacho kinaweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine
Kwa wale ambao walikosa first round application napenda kuwapa pole na wasikate tamaa kwani bado wananafasi second round.
Changamoto ni nyingi hivyo basi waombaji nawaomba kabla haujafanya hiyo second round kwanza kuwa na plan x kama kile unachokitarajia hautakikuta, namaanisha uwe na kitu cha ziada kingine cha kusoma kama hicho unachohitaji itakuwa ngumu kukipata
Napenda kuwajulisha pia kuna degree progam za ualimu kama ya bachelor of science with education, ni nzuri kwani unaweza kufanya masters katika fani ambayo ulikuwa na interest nayo before so usidharau maana hii watu huwa wanaitumia kama daraja..
Lakini pia kuna degree program kama vile za bachelor of science in chemistry, biology, mathematics, statistics, and physics na zenyewe ni nzuri ingawa unakuwa unasoma genarally but huwezi kukosa kitu cha kufanya baada ya kuhitimu lakini pia tunaweza kusema ni daraja zuri la kupata ticket ya kusoma masters kwa kile kitu ambacho upo interested much..
Lakini pia kwa wale ambao mnajua hali yenu ya kifedha haipo vizuri usilazimishe kuchagua vyuo vya private vye gharama kubwa ukashindwa mwisho wa siku kulipia ada...
Lakini pia wakati mnasubiria hizo post pamoja na mkopo kutoka loans board mkae mkijua kuwa mkopo unaweza kusumbua watu wanaweza kupata asilimia chache so pia tujiandaye kuikabili hili maana unaweza usilipiwe ada ukapata tu pesa ya kujikimu au ukakosa kabisa hata kama ulikuwa na vigezo...
 
Pole kwa kukosa first round maana second round huwa inamajanga yake...
 
Unajua wakati mwingine huwa inatokea mtu kukosa first round sio kwa sababu ya competition ila tu ni mtu mwenyewe kutakuwa na plan zaid ya mbili kichwani mwake
 
Mwaka juzi wakati tunafanya application competition ilikuwa ni kubwa mno maana watu walifahulu sana na cutting point zilikuwa hadi za 2.5 kama sijakosea..so kwa wale ambao waliishia kujaza program zile zenye ushindani waliishia kukosa first round na hata second round ilivyokuja hakukuwa na program za afya wala za engeneering kwa asilimia kubwa so ilipelekea watu mpaka kuhahirisha mwaka.
 
Na kuna wengine walikuwa wanadharau baadhi ya vyuo na kuona sio bora but mm najua elimu popote tu ukiishi kwa kufuata ya watu utaishia kuambulia nothing...cha msingi ni kupiga kitabu na kuchomoka...
 
Back
Top Bottom