Scotland na maamuzi ya muungano

Scotland na maamuzi ya muungano

mzenjiboy

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Posts
907
Reaction score
387
Wananchi wa Scotland watakuwa na uchaguzi hapo tarehe 18/9/2014 wa kuamua kama ni kuendelea na muungano na England au kujitoa na kuwa nchi kamili. Kwa mujibu wa mahojiano na wananchi wa Scotland ni kwamba zaidi ya asilimia 60 wanataka kujitoa.

Muungano wao umedumu zaidi ya miaka 300.

Na huu muungano FAKE uliopo baina ya Zanzibar na Tanganyika nao unasubiri siku na wakati ili kila mmoja awe kivyake.
 
Sina tatizo na muungano kudumu au kuvunjika nina tatazi na kuiga kila kitu toka kwa wazungu, hata siku moja muungano wa scotland huwezi kuufananisha na wa kwetu kwa namna yeyote ile ni kosa kubwa
 
Wazanzibari wanapenda wenyewe kua nyumba ndogo utawafanyaje?acha watanganyika nasi tuweke historia kua nasi ni wakoloni,tunaitawala zanzibar.
 
Wazanzibari wanapenda wenyewe kua nyumba ndogo utawafanyaje?acha watanganyika nasi tuweke historia kua nasi ni wakoloni,tunaitawala zanzibar.

MOD, hivi huwezi kuweka kitufe cha " like" kwenye mobile version ya JF?
 
Sio kila kitu kuiga Ulaya,Wenzio wana Sheria ya Ushoga na kwao ni Halali.
Sasa wewe sijui ndio kinachokuvutia hicho?
 
Na haya ya Zanzibar yanatoka wapi wkt tayari ni nchi???????/
 
Hatuigi ila swala la kuungana nchi inafaa liwe la wananchi si la viongozi na vyama vya siasa kuamua.Wengine wanasema sera yetu ni serikali mbili,ujinga gani huo jamani?Waacheni watu waamue hatima yao.
 
Back
Top Bottom