Scorpion anayetoboa watu Macho Buguruni, akamatwa

Scorpio Me

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2016
Posts
6,119
Reaction score
7,952
Kuhusiana na tukio la Hekaheka ya jana kuhusu Mwanaume mmoja mkazi wa Ubungo Makuburi Saidi almaarufu baba D kujeruhiwa vibaya na kutolewa macho na Mbabe mmoja wa Buguruni anayejiita Scorpion tena mbele za watu na hakuna hata mmoja aliyejitokeza kumsaidia kwa madai ya kamba huyo Scorpion anaogopeka na watu wote maeneo hayo ya buguruni.

Idara ya Hekaheka ikishirikiana na website yako pendwa geahhabibu.co.tz imefika eneo la Buguruni kwa mnyamani ambapo ndipo tukio hilo lilifanyika nakuweza kuongea na baadhi ya wananchi wa waeneo hilo kutaka kujua zaidi kuhusiana na huyo jamaa anayejiita scorpion imekuaje mpaka mtu anapigwa hadi kutolewa macho mbele yao bila wao kutetea chochote.

Wengi wao hawakuwa tayari kumuongelea kutokana na hofu waliokuwa nayo juu ya mtu huyo na hata hao waliokubali walijikuta wakielezea kwa kujificha bila kutaka kujulikana.

Wakazi hao wa Buguruni walidai kuwa jamaa ni mtaalamu wa mambo ya ngumi na huwa haogopi mtu yoyote hata mkienda wengi yeye ndio anafurahi.Vilevile walieleza kuwa hilo ni tukio lake la tatu la kumjeruhi mtu na kumtoa macho alishawahi kumvunja kiuno na mkono mwanamke mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Salum Hamdani amethibitisha kukamatwa kwa jamaa huyo ambapo anasema kwa sasa yupo ndani Magereza na kesi yake itasomwa tena tarehe 5 mwezi wa 10 2016.

Ni kweli hilo tukio limetokea na polisi tayari walishachukua hatua kwa maana ya huyo mtuhumiwa Scorpion jina lake halisi anaitwa Salum Mpepe alikamatwa siku ya tarehe 12 mwezi wa 9 akawa pale kituo cha polisi Buguruni wakati upelelezi ukiendelea tarehe 23 mwezi wa 9 alifikishwa mahakami na kusomewa jinai namba 276 unyanganyi kwa kutumia silaha, yupo magereza kesi yake itatajwa tena tarehe 5 mwezi wa 10 2016.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda zimemfika taarifa hizi ambapo yeye pamoja na Idara ya Hekaheka kupitia Leoetena ya Cloudsfm tutaungana kwa pamoja siku ya jumapili saa tisa jioni kwenda kuongea na wakazi wa Buguruni ili kuweka sawa mambo haya ya uhalifu yanayoendelea mtaani


Habari zaidi soma=> Mahakama ya Ilala imemhukumu Salum Njwete 'Scorpion' Kifungo cha miaka saba na faini ya sh milioni 30
 
 
Nikajua feedback kuwa jamaa ni marehemu kumbe bado mzima.
Mimi binafsi nilitegemea hivi mkuu. Ana bahati sana huyo nyang'au. Maana kikosi kazi kilikuwa kazini. Eti mtaalamu wa ngumi anapendelea watu wakija wengi!!!! WTF!!??
Haina haja ya kupoteza hela ya walipa kodi....huyu jamaa ilibidi atumbukizwe kwenye cyanide kule mgodini.

Hapo bugurini inatakiwa pasafishwe. Maana inaonekana bado kuna hao wapolimpo wenzake.
 
Hapa ndipo napokosa imani na viongozi wangu mtu kama huyu unampeleka jela akafanye nini? Huyu ni wakumalizana nae kimyakimya na akibahatika kwenda huko jela anaenda akiwa hana mikono au macho.
Huu sio mda wa kuendekeza ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…