Scientific fact na knowledge Thread

Hahahaaa impossible but possible kama universe ukiiterm kinamna hiyo
 
Siku za zamani zilikuwa fupi kuliko za leo.

Mabilioni ya miaka iliyopita, Dunia ilikuwa inazunguka kwa kasi zaidi.

Mwezi unapovuta bahari kupitia tides, polepole unachukua rotational energy ya Dunia.

hivyo siku inaongezeka kwa kiasi kidogo sana kadiri muda unavyopita.

Kwahiyo miaka 10 ya saizi ni miaka 25 ya zamani.
 
Kwahiyo unataka kusema kijana wa miaka kumi sasa hivi ni sawa na yule wa miaka 25 wa zamani?... Na hiyo zamani unayoizungumzia ni kuanzia wapi hadi wapi? Coz tupo mwaka wa 2026 so probably hiyo miaka billion itakua mabadiliko mengi sana yametokea and data hizi zilikusanywa kwa njia gani hasa?

Then elezea kidogo hiyo mechanism inavyotokea na mabadiliko yake yamesababishwa na nini
 
Mwezi → tides → tidal friction → Dunia inapoteza rotational energy → rotation inapungua → siku inakuwa ndefu.


Dunia ya zamani ilikuwa ikizunguka kwa kasi kiasi kwamba siku zake zilikuwa fupi sana kuliko za leo.

Mwezi umekuwa kama brake ya gravitational kwa mabilioni ya miaka.

elewa kwamba tides zinachukua sehemu ndogo sana ya rotational energy ya Dunia kwahiyo ina slow down mzunguko time after time.

hivyo kila baada ya muda mrefu sana siku huongezeka urefu kwasababu rotational speed inapungua.

Ndiyo maana ukilinganisha muda uleule, Dunia ya zamani ingeweza kuwa imefanya mizunguko mingi zaidi.

kwa mfano wa kufikirika, muda ambao leo tunauhesabu kama siku 10 ungeweza kuwa sawa na siku 25 za Dunia ya zamani.

Kwahiyo siku za zamani zilikuwa ni 40% ya siku za leo.

NB: ni takribani billions of years ago.

Thecoder hapa ntakuwa nimeeleweka vizuri ? 😊😊
 
Bahari ya Pacific ilipata jina hilo mwaka 1520 kutoka kwa mwanamaji wa ureno Ferdinand Magellan, ambaye baada ya kukumbana na dhoruba kali alipofika kwenye bahari hii alikutana na utulivu akaamua kuiita mar Pacifico, kabla ya hapo Bahari hii kubwa kuliko zote ilikuwa ikiitwa the great southern ocean.
 
Yeah hapa nimekuelewa vizuri mkuu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…