Science, Technology, and the Mind | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Science, Technology, and the Mind

Discussion in 'Great Thinkers' started by Raia Fulani, May 31, 2012.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Science is a systematic enterprise that builds and organizes knowledge in the form of testable explanations and predictions about the universe.

  Aristotle: Science refers to the body of reliable knowledge itself of the type that can be logically and rationally explained.

  Technology is the making, modification, usage, and knowledge of tools, machines, techniques, crafts, systems, methods of organization, in order to solve a problem, improve a preexisting solution to a problem, achieve a goal or perform a specific function.

  Mind is the faculty or complex of faculties that enables conscious thinking, reasoning, perception, and judgement.

  Nimeandika kwa lugha hiyo kutokana na ukweli kuwa maana ya maneno hayo yanapatikana kwa ufasaha kwenye hiyo lugha husika.

  Kwangu mimi, teknolojia ni sehemu ya sayansi. Sayansi ni ufumbuzi na uvumbuzi wakati teknolojia ni njia ya kufikia ufumbuzi/uvumbuzi.

  Sijui kwa ufasaha maana halisi ya neno 'mind' kwa kiswahili. Labda tuseme ni 'fikra'. Fikra ya mwanadamu inapokuwa na ujinga (ujinga si tusi bali ni hali ya kutojua kitu-ignorance), ni rahisi kushambuliwa na madhara mbalimbali ambayo yatayadhuru maisha yake kwa namna ambayo kwa asilimia kubwa ni hasi. Fikra sahihi hutoa uamuzi/hukumu sahihi. Hukumu sahihi huja kutokana na ushahidi uliothibitishwa kisayansi.

  Fikra na imani (belief) vinaendana. Fikra huitangulia imani. Fikra ikipotoka kwa kukosa uamuzi sahihi, huathiri maamuzi juu ya namna ya kuamini jambo fulani.

  Mfumo wa maisha katika jamii fulani huathiriwa na kiasi cha sayansi na teknolojia iliyopo. Jamii yenye uelewa wa kutosha juu ya mazingira waliyomo haina matatizo yaliyokosa angalau ufumbuzi kutokana na tatizo lililo mbele yao. Kuwa na sayansi na teknolojia pekee haitoshi. Ni kiasi gani jamii imeerevuka kutokana na hizo variable mbili?

  Mathalani ni kwa kiwango gani tunajua kuwa maji na chakula haviendani kwa wakati mmoja? Huo ni mfano mdogo sana. Tunawezaje kutumia sayansi na teknolojia kuwaelewesha jamii za wakeketaji kuwa wanachofanya si sahihi? Kuwaambia tu kuwa kitendo hicho ni kinyume na haki za binadamu, kiafya si nzuri, ni kosa la jinai inatosha? Ni kwa vipi utamweleza kisayansi kuwa kiafya si nzuri na akuelewe? Ni jambo ambalo limeshathiri 'Mind' yake. Kuwa mwanamke asiyekeketwa hawezi kuolewa. Kwamba mwanamke asiyekeketwa hana thamani wakati sio?

  Inatosha kumwambia mtu kuwa macho mekundu ni dalili ya kuathirika na moshi? Imefikaje hapo hadi kuamini kuwa ajuza mwenye macho mekundu ni mchawi? Utatumiaje sayansi na teknolijia kumwelewesha huyu mtu kuwa fikra zake si sahihi hivyo hukumu anayotoa si sahihi pia? Inakuwaje haya yanaendelea kutokea wakati nguvu ya dola inatumika na elimu inatolewa? Hiyo ni mifano michache sana!

  Hii ni dalili tosha kuwa jamii zetu hazijafikiwa vya kutosha na sayansi na teknolojia, hivyo fikra zetu zinatoa hukumu zisizo sahihi kwa mambo mengi sana ambayo tunakutana nayo katika maisha yetu ya kila siku. Nawasilisha.
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Naanza kuamini kuwa kuwa Great thinker ni lazima uwe na mawazo ya kisiasa zaidi? Tujaribu pia kuidadavua hii mada ili kuona mchango wa hizo variable tatu katika kumletea mtanzania maisha nafuu
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Dk Mafunda: Ugunduzi wa kisayansi utainua maendeleo ya jamii [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 26 June 2012 09:40 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Ibrahim Yamola
  UGUNDUZI wa kisayansi na kiteknolojia ni muhimu katika dunia ya sasa ambapo utandawazi unaelezwa kuchukua nafasi kubwa katika maendeleo ya nchi mbalimbali duniani.

  Kwa nchi kama Tanzania ambayo bado imo katika kundi la nchi zinazoitwa za dunia ya tatu, haina jinsi ya kuepuka kujihusisha zaidi na michakato ya ugunduzi wa kisayansi na hata matumizi yake kama inataka kupiga hatua zaidi kimaendeleo.
  Hata hivyo, inasikitisha kuona kuwa bado kumekuwapo na kasi ndogo ya Watanzania kujihusisha na masuala ya ugunduzi na ubunifu hasa katika nyanja za sayansi na teknolojia ambazo kwa sasa zimeshika kani duniani kote.
  Lakini hali hii haijawazuia wadau wa sayansi na teknolojia nchini, ikiwamo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kuendelea na mipango na mikakati ya kuimarisha maendeleo ya sayansi.
  Kwa mfano, Kaimu Mkurungezi wa Kituo cha Kuendeleza na Kuhawilisha Teknolojia (CDTT) katika tume hiyo, Dk Dugushilu Mafunda anasema kwa kutambua umuhimu wa teknolojia, tume imekuwa na utaratibu wa kuwatunuku wagunduzi katika kada mbalimbali za sayansi na teknolojia.
  Kwa mujibu wa Dk Mafunda, utaratibu huo ulioanza mwaka 1981ikiwa ni sehemu ya kuwatambua na kuwatunuku wagunduzi na wabunifu hasa wale wadogo, unalenga kutambua mchango wa wagunduzi hao katika jamii zao na Taifa kwa jumla.
  "Kufanya hivyo ilikuwa ni njia stahiki kwa wagunduzi kuamsha morali na watu wengi kujiingiza katika ugunduzi kwa manufaa ya jamii inayowazunguka" anasema na kuongeza:
  "Ni wajibu wetu kuhakikisha tunatambua mchango wa wananchi wanaogundua vitu mbalimbali, hususani vifaa vya kisayansi kwa kuwatunuku na kuwaendeleza kwa manufaa ya Taifa letu.''
  Anaeleza kuwa kwa sasa tume imekuwa ikitoa tuzo kadhaa ikiwamo Tuzo ya Sayansi Shuleni (SSA) inayolenga kujenga misingi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika ngazi ya shule za sekondari na vyuo.
  "Tuzo hii hutolewa kwa shule itakayokuwa imeonyesha juhudi katika matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu hasa katika kufundishia, kutengeneza zana za kufundishia au katika majaribio ya kisayansi,''anabainisha.
  Tuzo nyingine ni ile ya Utafiti wa Hifadhi na Uendelezaji wa Mazingira (NAEM) ambayo hutolewa kwa wanasayansi na wanateknolojia wanaotoa mchango katika kubuni teknolojia zinazopunguza uharibifu wa mazingira kama vile uchafuzi wa hewa, taka za sumu, uharibifu wa maliasili na wanyama pori.
  Nyingine ni tuzo ya Taifa ya Mafanikio katika Sayansi na Teknolojia (TASTA). Hii hutolewa kwa Watanzania waliofanya ugunduzi ambao unaweza kuleta manufaa katika kuboresha maisha na uchumi nchini au kuendeleza elimu na taaluma za fani mbalimbali za sayansi, teknolojia na ubunifu.
  Akieleza sifa ambazo mgunduzi hutakiwa kuwa nazo ili aweze kutunukiwa tuzo, Dk Mafunda anataja kuwa ni pamoja na mgunduzi kuonyesha uasili wa alichokigundua, kuwapo kwa tathimini ya kitaalamu, uwezo wa manufaa ya ubunifu wake kwa jamii na Taifa, upya wa ugunduzi wake, matumizi ya malighafi zinazopatikana nchini na uendelevu wa ugunduzi.
  "Mara baada ya mtu kufanya ugunduzi anatakiwa atume maombi kwetu, na sisi tutawashirikisha wataalamu wetu kuupitia ugunduzi huo na kuona kama kweli unakidhi haja na hatimaye tunaanza kumtambua," anaeleza.
  Anaongeza: "Baada ya kuona watu wengi wanagundua vitu mbalimbali bila ya kuviendeleza, COSTECH ilianza utaratibu wa kuwatunuku vifaa vinavyoendana na ugunduzi wao ili waweze kujiendeleza kwa manufaa ya jamii zao.''
  Akitoa mfano wa matatizo yaliyoko katika sekta ndogo ya nishati umeme, anasema wamekuwa wakipokea gunduzi za wananchi wanaozalisha umeme hasa katika maeneo ya vijjini ambayo hayafikiwi na umeme wa gridi ya Taifa.
  "Endapo tutawapa vitendea kazi hawa wagunduzi, nina uhakika watasaidia kuondokana na utegemezi wa umeme wa gridi ya Taifa kwa baadhi ya maeneo.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Najiuliza, tuzo tu zinahitajika? Ni vipi tunaweza kuitumia hii sayansi na teknolojia kutatua matatizo yanayotukabili? Naona hapo hamna popote yalipoorodheshwa mambo ambayo yanaweza kutatuliwa.
   
Loading...