Scholarships kwa wawanawake tu

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,568
2,911
Hi kama una binti au mama at least kidato cha nne basi mwambie achangamkie hapo!! aweza kubahatika na maisha yakabadilika. ndo maana ya mtandao hii kupeana taarifa kama hizi.

FUNGUA ATTACHAMENTS 2 KWA MAELEZO ZAIDI



TANGAZO LA KOZI NA UDHAMINI
Nafasi Opportunity Society (NOS) ni taasisi iliyoko
nchini Canada inayosaidia wasichana wa Kitanzania
kwa kuwapatia ujuzi ili kujikomboa na umasikini.
Katika mwaka wa 2014 NOS itatoa udhamini kwa wasichana
25 kwa kuwalipia ada na fedha ya kujikimu ili kupata
mafunzo ya “Hairstyling and Business Skills”
Mafunzo yatatolewa kuanzia Novemba 2014 mpaka Mei
2015 jijini Dar es Salaam kwa ushirikiano na Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania. Kozi itahusisha nadharia na vitendo
katika Shule ya Urembo.
Sifa za Mwombaji:
• Awe msichana wa Kitanzania wa umri wa kati ya
miaka 18 – 28.
• Awe amehitimu elimu ya Kidato cha Nne au Zaidi.
• Awe na ufahamu wa awali wa Lugha ya Kiingereza.
• Awe na shauku/ari ya kujifunza mambo ya urembo.
• Awe ametoka katika familia isiyo na uwezo
kiuchumi.
Jinsi ya Kutuma Maombi:
Fomu za maombi zinapatikana katika ofisi za Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania zilizoko;
1. Kinondoni Makao Makuu (Block C, Ground Floor
ICE office, ulizia Mr Muda)
2. Kinondoni Regional Centre (karibu na Kiwanja cha
Biafra, ulizia Mr. Adrian)
3. Temeke Regional Centre (ndani ya viwanja vya
Sabasaba, ulizia Mr. Ben Mwinuka)
4. Ilala Regional Centre (Jengo la Taasisi ya Elimu ya
Watu Wazima, ulizia Ms Martha Kabate)
Fomu zilizojazwa ziambatanishwe na
• Vyeti vya elimu ya Sekondari
• Nakala (photocopy) ya kitambulisho chochote
kinachokubaliwa na Serikali kama vile,
Kitambulisho cha Mpiga Kura, Kitambulisho cha
Taifa, cheti cha kuzaliwa n.k.
• Picha ndogo ya rangi (passport size)
Zitumwe Kwa:
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Nafasi Opportunity Scholarship Committee,
Kawawa Road, Kinondoni Municipality,
P. O. Box 23409,
Dar es Salaam
Au zirudishwe moja kwa moja kwenye moja ya Ofisi za
Chuo zilizotajwa hapo juu
NB: Maombi yatumwe kabla ya Oktoba 27, 2014
Waombaji watakaoorodheshwa wataitwa kwa
usaili
Kwa Maelezo Zaidi Wasiliana Na:
Program Coordinator:
Simu: 0767-971015
Baruapepe: krwegasira@gmail.com.
HAIRSTYLING CERTIFICATION
 

Attachments

  • MCHONGO KW WASICHANA TU!!!!!!!.pdf
    439 KB · Views: 164
  • Scholarship Application KWA WASICHANA TU.pdf
    532.2 KB · Views: 277
Bonge la opportunity kwa dada zetu, ila ningependa kozi kama hizi zingefundishwa kwa Kiswahili maana uelewa wa kiingereza wa form four ni wa kuunga na gundi,tena shule zetu hizi za kata ni majanga. Anyway dada zetu changamkieni deal hilo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom