Scholarships for Masters Degree for Women in Australia

Scholarships for Masters Degree for Women in Australia

Joined
Sep 10, 2016
Posts
63
Reaction score
170
Scholarship za Australia Zipo, where are the Young Women and Others in Tanzania?
Nilialikwa kwenye Mkutano wa Alumni wa Australian Gov. Scholarships ambapo Balozi mdogo wa Australia alizungumzia jinsi watanzania tulivyo na muitikio mdogo wa fursa hizi za wanawake. Kwa mwaka huu alisema ni watanzania 8 tu mpaka tarehe hiyo (6 octoba, 2016) waliokua wamewasilisha maombi, ambayo deadline ni Dec 15, 2016.

Waombaji Hakuna
Tulipouliza kwa nini maafisa wa fursa hiyo wenye makao yao makuu kenya walitujibu, (1) kuna waombaji wachache sana kutoka Tanzania tofauti na wale wa nchi nyingine za Ukanda huu
(2) Hata kwa maombi yanayowafikia, ujazaji wa fomu za maombi unaonekana kuwasumbua na hata majibu ya maswali mepesi sana yanaonekana kuwa tatizo kwa watanzania.

Chukua Hatua Sasa!
Watanzania wenzangu, tusikasirike wala kuanza kuwatukana wenzetu kama ilivyo kawaida yetu humu ndani. Tumembiwa ukweli, tuutumie ili kupona. Mimi nimechukua hatua kama ifuatavyo. Nakuhamasisha usambaze taarifa hii vijana wenye vigezo vya umri, degree na uzoefu wa walau miaka 3 kwenye sekta yoyote ile, binafsi, serikalini, NGO, voluntarism, self employed waangalie website ya Australia Gov. Scholarships, watakuta fomu ya maombi watoe nakala safi moja na kopi, wanitafute maana ninaandaa siku maalumu waje chuoni kwangu EABMTI tutakaa na kujaza hizo fomu pamoja, nitawafundisha kujibu maswali ya msingi ya vigezo na masharti kutokana na uwezo wao, nitawaelewesha juu ya viambatanishi, na tutakua na siku maalumu ya wote kuleta viambatanishi, nitavipitia, watavi pack pamoja na kwenda kuvituma. Lazima tupambane kwa mbinu za kisasa, hakuna uchawi ni elimu na mitazamo chanya tu. Kwa sisi tuliokwisha ono mwanga, tujitoe kwa ajli ya vijana wetu, hakuna malipo ni mojawapo ya huduma zangu kwa jamii na shukurani zangu kwa muumbaji kwa neena hii ya pumzi na uhai. Kwa wale vijana unaweza kuwasiliana na ofisi yangu kupitia info@eabmti.org
 
Ahsante sana Mama tayari nshaisambaza kwa watu wangu muhimu hasa wale nnao jua wanaitafuta hiyo Fursa.
 
Umenena vema ndugu Mtanzania mzalendo,tunahitaji vijana wetu wasome vizuri nitaisambaza.Shime kwa vijana wa kisasa wenye vigezo sisi wengine umri ushatutupa mkono.Kila laheri.Angalau ungeweka kigezo cha umri unaotakiwa ili iwe rahisi kwa wenye sifa kuchangamkia.
 
Hiyo huduma mleta maada unaitoa bure au kuna gharama? Kama ipo ni shilingi ngapi?
 
Mkuu mtoa mada ofisi zenu kwa Dar ziko wapi?Je mnafanya kazi hadi siku za Jumamosi?Nahitaji kufika hapo
 
K
Ahsante sana Mama tayari nshaisambaza kwa watu wangu muhimu hasa wale nnao jua wanaitafuta hiyo Fursa.
pasto tafadhalini Julisha mtandao wako Kuwa tarehe 9 ni kesho watumia thread niliyotuma Leo mtandao Ili kesho wafike bila kukosa
 
Back
Top Bottom