“scenes za mapenzi kwenye filamu zinawaumbua wasanii wanaonuka midomo” – irene uwoya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125



MSANII wa filamu anayejichukulia umaarufu bongo Irene Uwoya,amedai kuwa kuna baadhi ya wasanii wenye majina makubwa wanapenda kucheza filamu za mapenzi na uchezeana huku wakishindwa kuelewa kuwa wananuka midono na mara nyingine huwa wanavumulia pasipo kutoa ukweli huo.

Kauli kama ya msanii huyu iliwahi kutolewa na Janet Jacksonkwenye filamu ya ‘Poetic Justice’ iliyozinduliwa mwaka 1993 akimtaka Tupac Shakur kupima vizuri vya ukimwi kwani kuna kipande walitakiwa kuonekana wakipeana midomo kwani walicheza kama wapenzi ndani ya filamu hiyo, ndiyo kitu ambacho hata kwa wasanii wa kitanzania wanatakiwa kujifunza na si kukurupuka kupeana midomo..


Uwoya alisema kuwa kuna sehemu huwa wanakosea na kupeana midomo bila kupima afya kwani wapo wasanii wengine si wasafi na wananuka midomo huku wengine wakiwa wanatumia sana dawa za kulevya hivyo kuna hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa endapo wasipo chukua hatua.

Alisema kuwa wengine wanajijua walivyo lakini wanashindwa kujisafisha na kuwa katika hali nzuri badala yake ndani ya filamu wanaanza kupeanda kiss na kuchezeana bila kujua afya ziko vipi.


“Sasaivi naanza kuwa mkali kwa sababu endapo tukiendelea kuwa kimya tunaweza kujikuta magonjwa yanatukuta hivi hivi” aliongeza.

Hata hivyo msanii huyo aliwashauri baadhi ya wasanii wenye tabia za kupenda kupeana midomo ndani ya filamu wawe makini kwani huwezi jua ni ugonjwa gani anaoweza kupata, na kikubwa zaidi ni kupima kabla ya kazi kuanza ili kama kuna mtu mwenye tatizo apewe tiba mapema.



 
[h=2]irene uwoya Ataka watu kabla ya kulana denda katika Filamu wakapime Ukimwi na Wengine Midomo yao inanuka hawafai kuwapiga Denda saudari upo lakini?[/h]
 
Last edited by a moderator:
irene uwoya Ataka watu kabla ya kulana denda katika Filamu wakapime Ukimwi na Wengine Midomo yao inanuka hawafai kuwapiga Denda saudari upo lakini?

Aaaaaah! Si aseme anataka kupigwa denda maana itafikia muda atasema wakitaka kuigiza wanaDO lazima wakapime.
Sasa wewe utalifikiriaje hilo kama wewe ni Mchambuzi wa mambo, si amuambie ukweli mumewe kwamba amemchoka.
 
Ni kweli watu wengi ni nadhifu kimwonekano wa nje lakini akiongea utadhani bomba la maji machafu limepasuka.
 
HIi kali sana, inaonesha huaga matukio hayapangwi na waigizaji wanatengeza scenes bila direction, unakuta tu njemba inaanza kulazimisha denda kwa demu, hahaa wabongo kwa upekupeku siwawezi/
 
kama ambavyo wanaji make up sura wakumbuke na kinywa................Mzizi tupe dawa hapo kwenye lile jukwaa letu
 
Hilo halitakaa litokee, hakuna hata msanii mmoja atakayekuwa na ujasiri wa kwenda kupima Ukimwi, labda kama atahonga ili apate majibu safi, vinginevyo ni sawa na simulizi za kufikirika...................
 
Hilo halitakaa litokee, hakuna hata msanii mmoja atakayekuwa na ujasiri wa kwenda kupima Ukimwi, labda kama atahonga ili apate majibu safi, vinginevyo ni sawa na simulizi za kufikirika...................

Kwa tulivyo sie binadamu na wasanii wetu wakiwemo . . . . lazima kutatokea uhasama hata kama mtu kaambiwa ukweli!
Labda waanzishe kautaratibu kawe general.
 
ameongea point ya muhimu sana na namsifu kwa kufunguka kwa uwazi.
Anazingua mi sio MTU wa bongo movie
ila kuna moja nilibahatika kukutana nayo azam TV na
Kuichek inaitwa DJ Ben. Ambaye ni Jb,mke wake ni wema,uwoya alikua Demu wa
Jb ila zile kiss azikua kiss zilikua n denda sasa anauakika Jb amepima
 
Back
Top Bottom