Sayansi ya upendo, jinsi mtu anavyoweza fall in love na wewe

Dead Man

JF-Expert Member
Jul 17, 2021
709
826
Watu wengi wamekuwa wanatamani kupata nafasi ya kupendwa na watu wanaowapenda, wahitaji, lakini wamekuwa hawajui njia za kufanikisha hayo yote.

Leo nataka nikupe siri moja.
Ili umvutie mwanadamu yeyote yule basi sharti ujue udhaifu wake uko wapi.

Udhaifu mkubwa wa mwanadamu uko katika mwili wake, kama ifuatavyo:
1: Milango ya fahamu(Macho, masikio, pua, ngozi, ulimi)
-->> Kibailojia hii hutumika kumfanya mtu atambue mazingira yake.
Lakin kimahusiano, hii hutumika kuushawishi moyo kumpenda mtu, kushawishi ubongo kutunza kumbukumbu za mtu, kumuwazia mtu.
  • Mtu anaweza akaanza kukupa attention pindi tu alipokuona.
  • Au aliposikia sauti yako, au kitu chochote kuhusu wewe.
  • Au aliposikia harufu iliyompendeza kutoka kwako.
  • Au alipopata msisimko wa ngozi yake, baada ya mguso au chochote kilichomsisimua kutoka kwako.
  • Au baada ya kuonja kitu kutoka kwako, au kuwa na tabia ya kukuzungumzia mara kwa mara.
.
2: UBONGO.
- Kazi ya ubongo ni kutafsiri mambo, pamoja na kutunza kumbukumbu.
*Inshu ni simple tu, unaposhawishi milango ya fahamu ya mtu, ni wazi kuwa tayari ushapata nafasi ya kuwa katika kumbukumbu za huyo mtu.
#Inafanyaje_kazi_
Ulipita karibu yake, pua ikasikia harufu nzuri kutoka kwako.
Pua ikatuma taarifa kwenda kwenye ubongo, ubongo ukatafsiri na kutuma majibu kwenye macho.
Anageuza shingo ili amtazame nani huyo anayenukia vizuri, macho yanakumbana na mrembo.
Process inajirudia kwenye ubongo na kujikuta majibu yanatoka kwenye mdomo, ulimi unatamka...."Daaaamn, bonge la mtoto.
.
siku zinapita, mawazo yake yote juu yako, kila muda anazungumza kuhusu wewe na uzuri wako. Anaikumbuka ile harufu.
Lakini kianzilishi cha yote hayo, ilikuwa ni pua tu.
.
Story itaendelea
.
3: MOYO:
-->> Kibailojia, kazi ya moyo ni kusukuma damu.
Lakini kimahusiano tumeipa nafasi kubwa moyo kuwa ndio wenye nafasi ya kupenda.
*Ukitaka kujua kuwa moyo uko connected na mapenzi, hebu fikiria siku ya kwanza kabisa uliotaka kumsalimia mtu unayempenda, na siku ambayo uliyempenda alitamka kukuacha, HUKUSIKIA MAPIGO YA MOYO YANAENDA MBIO???
Moyo kuuma???
- Baada ya ubongo kutunza kumbukumbu na kumtafsiri mtu fulani kwa muda mrefu, ndipo moyo huamua kutunza nafasi kwaajili ya huyo mtu.
*UBONGO na MOYO ndio udhaifu mkubwa zaidi wa mwanadamu.
.
4: VIUNGO VYA MWILI(Miguu, shingo, mikono, kiuno).
  • Hizi ni sehemu za mwili ambazo hufanya kiumbe kijongee(kusogea kutoka sehemu moja kwenda kwingine).
  • Kwenye mahusiano hizi ni sehemu ambazo humfanya mtu afate vile moyo na ubongo unavyomwambia.
  • Ukitaka kumfanya mtu awe mtumwa wa mapenzi basi sharti uuchanganye ubongo wake na moyo wake, na huo ubongo*moyo utatumika kuzitumikisha hizi sehemu kufata vile unavyotaka.
* Mtu anaweza toka Tazara mpaka Tabata kwa kwaajili ya kwenda kumuona ampendae.
*Hiki ndo kipindi ambacho miguu inasema nimechoka nataka pumzika, ubongo unasema hapana tukichelewa kufika tutamkosa...we jikaze tu.
.
5: VIUNGO VYA UZAZI:
- Hutumika kwaajili ya tendo la ndoa, kuzalisha, au kuzalishwa.
*Ukishawishi milango ya fahamu, ubongo, moyo, viungo vya mwili vya mtu basi ni rahisi kumfanya akupe utumie sehemu zake za siri, tena kiulaini sana kama unamsukuma mlevi.
.
MAMBO YA KUZINGATIA KAMA UNAMPENDA MTU, NA UNATAKA AKUPENDE.
- Mfanye mtu asikie kauli nzuri, sauti nzuri, nyimbo nakadhalika.
Mfano: Nakupenda sana, nakumiss, umependeza.
.
-Mfanye mtu aone kitu kizuri, muonekano wako, mandhari ya vitu vya kushangaza. Mfano: Pendeza, mtoe out, surprise.
.
Mfanye mtu anuse harufu mzuri, ya mwili wako, vyakula, manukato na mambo mbalimbali.
.
- Mfanye mtu aonje, au awe anazungumza sana kuhusu wewe.
Mfano: Mtoe out penye chakula kitamu, kesho akikumbuka kile chakula basi lazima atakukumbuka pia, mfanyie mambo mazuri, mfurahishe, mfunze, mshauri basi lazima ataongea kuhusu wewe.
.
Mfanye mtu asisimuke. Mfano: Penda uchokozi, kuwa romantic mara umemshika mkono, ukimkombatia hakikisha miili yenu iko "ZERO DISTANCE", mbusu, mpapase basi lazima atapata feelings za ajabu atakazozikumbuka.
.
- Mfanye mtu akuweke akilini mwake/mawazoni mwake: ili mtu akukumbuke basi fata hizo hatua za hapo juu, lazima atakuwaza tu.
.
- Mfanye mtu akupende: Kuwa na tabia zinazompendeza, fanya mambo ambayo alitaman kufanyiwa, mvutie kwa muonekano, nakadhalika.
.
- Mfanye mtu awe anapata sababu ya kukufata, au kukusubiri sababu viungo vyake ndo vinaweza kumfanya aondoke usimkute au akufate uliko.. Changanya moyo na ubongo wake kwanza.
.
- Mfanye mtu awe na hamu ya kufanya tendo la ndoa na wewe: Hapa ndo penyewe, ukimchanganya huko juu, ukapewa hii nafasi...
hakikisha unaitumia vyema kabisa maana hiki ndo kibeba upendo.
.
Mpaka hapo nahisi tutakuwa tumeelewana.
Upendo huanzia kwenye milango ya fahamu, mpaka kwenye ubongo, ubongo mpaka kwenye moyo, moyo mpaka kwenye viungo, viungo vya mwili mpaka kwenye viungo vya uzazi.
.
Formular hii hutumika kokote pale.
Ukitaka kuwa mwanamuziki, muigizaji, au mtu yeyote ambaye atahitaji mashabiki wa kweli basi ana ondoa namba "5" tu, neno "VIUNGO VYA UZAZI".
Ila hiyo 1-4 anazitumia vizuri.
Mfano: Mashabiki wa Diamond,
walimpenda baada ya kumsikia, sasa hivi kawa mtu wanaye muwazia, wanaye penda kumuona, waliyemuweka ndani ya ubongo wao na mioyo yao.
Viungo vyao vya mwili vinamfata kokote pale atakaposema anafanya show.
 
Back
Top Bottom