Sayansi ya siasa 101: Hakuna aibu katika siasa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,608
46,251
Wakati unamkosoa mwanasiasa yoyote usitumie neno AIBU au HAYA. Mwanasiasa akibadilisha msimamo au gia angani ni kwa sababu ameona hiyo itakuwa na manufaa mkubwa kwake kwa kipindi hicho na alihitajika kufanya hivyo.

Wanasiasa wengi au karibia wote hawajali AIBU, kitu kikubwa kwao ni kuendelea kudumisha madaraka.Na ili kuyadumisha madaraka kubadilika badilika kama kinyonga ni njia mojawapo.
 
Hilo sii lakushanga kwani wametuonyesha mengi,tangu yale ya buguruni,ya mtaa wa kijani na ya waunga juhudi .Yote ni machache Kati ya visa vingi vya kutisha ya anaeitwa mwana sii hasa.
 
Habari hii isiache kuwafikia wafuatao:

IMG_20210507_212540_605.jpg

IMG_20210418_164416_802.jpg

IMG_20210327_064409_035.jpg

IMG_20210502_142635_930.jpg

Bwana Mimacho na binamu zao wote kokote kule mliko.
 
Wakati unamkosoa mwanasiasa yoyote usitumie neno AIBU au HAYA. Mwanasiasa akibadilisha msimamo au gia angani ni kwa sababu ameona hiyo itakuwa na manufaa mkubwa kwake kwa kipindi hicho na alihitajika kufanya hivyo.

Wanasiasa wengi au karibia wote hawajali AIBU, kitu kikubwa kwao ni kuendelea kudumisha madaraka.Na ili kuyadumisha madaraka kubadilika badilika kama kinyonga ni njia mojawapo.
Ni "WAZO" 'complex' sana uliloliweka hapa; na ninakubaliana na nadharia hii kwa kiasi kikibwa.

Ugumu wa kuielezea dhana yako hii unatokana na ugumu wa kujua/kuambua/kutofautisha, mwanasiasa hasa ni nani?

Mtu yeyote anayejihusisha kwenye mambo yanayohusiana na siasa, tumtambue kwamba huyo ni mwanasiasa?

Kwa mfano: hivi tunaweza kumweka kwenye kundi la wanasiasa mtu kama Trump?

Na kwa upande wa pili, watu kama Bashir Ally, au Kabudi Kalamaganda, hawa nao ni wanasiasa? Hilo ni kundi moja.

Nyakati nazo zina uzito mkubwa katika kubainisha uliyoandika hapo.

Nyakati za akina Mikael Gorbachef, au rudi nyuma kabisa kwa akina Winston Churchill na viongozi wengi wa nyakati hizo, nao utawapima kwa vigezo vinavyofuatana na mada yako?

Hebu angalia mkanganyiko na ugumu wa kuwaelezea watu hawa 'wanasiasa' kama kundi - ukiangalia viongozi wa nchi za kiafrika waliopigania uhuru na hawa tulionao leo; kuna kipimo chochote kinachowaweka kwenye kundi moja na kuwazungumzia wote kwa usawa?

Inawezekana nisiwe nimejieleza vizuri hapa kiasi cha kueleza nilivyoielewa mada yako hii ngumu sana kuijadili.

Kiufupi, kwa maoni yangu, mwanasiasa, hasa katika nchi zetu hizi zinazoendelea, na hasa hizi za Kiafrika, ni kiongozi anayesukumwa na ari ya kuwatumikia wananchi na nchi yake ili yawepo mabadiliko chanya katika maisha ya wananchi hao. Mtu anayesukumwa na nia ya kutumikia, na siyo kujitweza na kuburuza anaowaongoza.

Hayo ndiyo niliyonayo akilini, mimi nisiyekuwa na chochote kwenye mambo ya "Sayansi ya Siasa 101."
 
"Kiufupi, kwa maoni yangu, mwanasiasa, hasa katika nchi zetu hizi zinazoendelea, na hasa hizi za Kiafrika, ni kiongozi anayesukumwa na ari ya kuwatumikia wananchi na nchi yake ili yawepo mabadiliko chanya katika maisha ya wananchi hao. Mtu anayesukumwa na nia ya kutumikia, na siyo kujitweza na kuburuza anaowaongoza".

Hayo ndiyo niliyonayo akilini, mimi nisiyekuwa na chochote kwenye mambo ya "Sayansi ya Siasa 101."

Sio kweli haya uliyoyaandika. Siasa Africa ni "ULAJI" "SHAVU" " MCHONGO KWA WANA"
Ni "WAZO" 'complex' sana uliloliweka hapa; na ninakubaliana na nadharia hii kwa kiasi kikibwa.

Ugumu wa kuielezea dhana yako hii unatokana na ugumu wa kujua/kuambua/kutofautisha, mwanasiasa hasa ni nani?...
 
Trump, Bashiru Ally, Kabudi wote ni wanasiasa.
Ni "WAZO" 'complex' sana uliloliweka hapa; na ninakubaliana na nadharia hii kwa kiasi kikibwa.

Ugumu wa kuielezea dhana yako hii unatokana na ugumu wa kujua/kuambua/kutofautisha, mwanasiasa hasa ni nani?

Mtu yeyote anayejihusisha kwenye mambo yanayohusiana na siasa, tumtambue kwamba huyo ni mwanasiasa?

Kwa mfano: hivi tunaweza kumweka kwenye kundi la wanasiasa mtu kama Trump?

Na kwa upande wa pili, watu kama Bashir Ally, au Kabudi Kalamaganda, hawa nao ni wanasiasa? Hilo ni kundi moja.

Nyakati nazo zina uzito mkubwa katika kubainisha uliyoandika hapo.

Nyakati za akina Mikael Gorbachef, au rudi nyuma kabisa kwa akina Winston Churchill na viongozi wengi wa nyakati hizo, nao utawapima kwa vigezo vinavyofuatana na mada yako?

Hebu angalia mkanganyiko na ugumu wa kuwaelezea watu hawa 'wanasiasa' kama kundi - ukiangalia viongozi wa nchi za kiafrika waliopigania uhuru na hawa tulionao leo; kuna kipimo chochote kinachowaweka kwenye kundi moja na kuwazungumzia wote kwa usawa?

Inawezekana nisiwe nimejieleza vizuri hapa kiasi cha kueleza nilivyoielewa mada yako hii ngumu sana kuijadili.

Kiufupi, kwa maoni yangu, mwanasiasa, hasa katika nchi zetu hizi zinazoendelea, na hasa hizi za Kiafrika, ni kiongozi anayesukumwa na ari ya kuwatumikia wananchi na nchi yake ili yawepo mabadiliko chanya katika maisha ya wananchi hao. Mtu anayesukumwa na nia ya kutumikia, na siyo kujitweza na kuburuza anaowaongoza.
Hayo ndiyo niliyonayo akilini, mimi nisiyekuwa na chochote kwenye mambo ya "Sayansi ya Siasa 101."
 
Sio kweli haya uliyoyaandika. Siasa Africa ni "ULAJI" "SHAVU" " MCHONGO KWA WANA"
Mkuu 'Yoda', labda uwe hujanielewa nilichoandika.

Sikuandika kwamba hao ndio wanasiasa tulionao Afrika sasa hivi.

Ninapata taabu sana hata kupata mfano mmoja wa viongozi wa leo ninaoweza kuutoa wenye sifa za namna hiyo.
 
Back
Top Bottom