SoC02 Sayansi na Teknolojia

Stories of Change - 2022 Competition

Nasherah bajah

New Member
Aug 16, 2022
1
0
Ukuaji Wa Sayansi Na Teknolojia.

Awali ya yote tunatakiwa tujue nini maana ya Sayansi na Teknolojia,na ndani ya Sayansi na Teknolojia Kuna kitu gani na kitu gani na vina umuhimu gani ama na mchango katika maisha au mfumo mzima wa maisha ya binadamu.

Tukianza na Sayansi kiujumla ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa. Hii inamaana ya kwamba kufanya vitu kwa vitendo zaidi Ili kuleta uelewa uliowajua na kumfanya mtu kupata utambuzi wa jambo kwa haraka na uelewa.

Tuna aina nyingi za Sayansi mfano bailojia, fizikia, astronomia,jiolijia na nyingine kibao..Aina zote hizi zinaelezea mambo yanayozunguka jamii kiujumla na hutupa mwangaza mkubwa sana katika maisha kujua yanayojiri,yaliyojiri na hata yanayotaka kujiri kwenye dunia.

kwa upande wa Teknolojia ni vifaa na mashine zinazotumika katika matengenezo au uzalishaji wa vitu,ama kwa uwepesi zaidi ni ujuzi wa kutumia vyombo ili kurahisisha kazi.

Teknolojia imetoa mchango mkubwa sana katika urahisishaji wa kazi ingawa imekuja kuleta athari nyingi katika maisha ya kila siku Kwani kila chenye faida hakikosi hasara.

Sayansi na Teknolojia imeleta mabadiliko makubwa sana katika jamii ya Tanzania ilhali na changamoto za hapa na pale lakini imeweza kuleta mafanikio makubwa katika nyanja tofauti katika elimu, afya,na hata kwenye sekta ya biashara.

Tuangalie mchango wa Sayansi na Teknolojia katika maisha yetu ya sasa:


1- Mchango Katika Mawasiliano
kwa sasa Tanzania tunapashana ama kupeana habari kupitia adha mbali mbali mfano simu, kompyuta nakadhalika tofauti na zamani ambapo watu walikuwa wanapeana hapari kupitia habari ambazo zinaweza kuchukua zaidi ya mwezi kupata ujumbe fulani lakini Sayansi na Teknolojia ya Leo imeweza kutusaidia mtu kupata taarifa kiurahusi ndani mda mchache sana katika siku.
Pia imeweza kusaidia ukuaji wa biashara kwani imefanya kuwa na upana mkubwa na hata kujulikana katika mataifa ya nje kwani matangazo yanayofanyika kupitia simu ama kompyuta huleta wadau mbalimbali na kutaka kujua zaidi juu ya bidhaa ama biashara ama soko.

2-Ukuaji wa kilimo na mifugo.
kwa upande wa kilimo Sayansi na Teknolojia imeweza kuleta matrekta ambayo yamekuwa kama saidizi katika suala Zima la kilimo na kwa haraka zaidi.Pia imeweza kuleta baadhi za vimwagilizia kama mabomba yanayopitishwa katika mashamba kurahisisha umwagiliaji maji kwa mimea .
kwa upande wa mifugo imetusaidia mashine za kukamulia maziwa,mashine za kuogeshea mifugo nahata pia vifaa vya kulishia mifugo na hata upande wa antibiotics kwa mimea na wanyama.
Sayansi ilileta maendeleo katika maendeleo ya mazao ya maumbile, ambayo ni sugu zaidi kwa wadudu, na pia mbolea.

3-Mchango katika sekta ya elimu
kwa upande wa elimu imerahisisha watu kusoma kwa vitendo zaidi ilikuleta uelewa kwa wanafunzi hasa kwa masomo ya Sayansi nikiwa na maanisha fizikia,biolojia,kemia na hata jiografia.Kwa asilimia kubwa imetusaidia katika takwimu ya ufaulu wa wanafunzi mashuleni tofauti na hapo awali.Vitu kama kompyuta, projekta, mtandao, na hata simu za rununu hutumiwa katika madarasa ili kuwachochea wanafunzi.
Pia imeweza kuwezesha elimu kwa walemevu kwa maana viwete ,vipofu mabubu na hata viziwi kwani imeleta vifaa vitakavyowawezesha hata wao kupata haki yao ya msingi ilikutimiza ndoto na malengo yao.

4-Mchango katika sekta ya afya.
Hii ni sekta nyeti sana kuliko zote kwani tukiongelea tunaongelea maisha ya mtu kiujumla sababu shughuli bila afya Bora ama imara ni jambo gumu sana.
kwa upande wa afya Sayansi na Teknolojia imetuletea vifaa mbali mbali kama mashine ya moyo,ambayo ilikuwa ni changamoto kubwa sana hapo awali.Hivi sasa kliniki na hospitali zina vifaa bora, ambayo inaruhusu utunzaji bora wa mgonjwa.Pia kupitia Teknolojia ya sasa imeweza kuifanya Tanzania kuinuka tangu upasuaji wa watoto waliogandana kufanikiwa salama salmini kwani ni upatikanaji wa vifaa Bora na madaktari bingwa hadi jambo Hilo kufanikishwa.

5-Mchango katika miundo mbinu na utunzaji wa rasilimali malighafi zipatikanazo katika nchi yetu.
mfano utengenezaji wabarabara umeleta urahisi wa usafirishaji wa bidhaa na hata watu pia.
utunzaji wa rasilimali malighafi imeweza kusaidia kuzuia namba za wizi wa Mali ya Tanzania na kulinda katika mfumo uliobora na hata kupunguza upoteaji wa maliasili za Tanzania.
Nini kifanyike na kipi kisifanyike Ili kuleta mabadiliko zaidi katika Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya maendeleo zaidi ya nchi:

✓ Watu wanatakiwa kuwa na uwezo mkubwa na maamuzi makubwa yatakayowezesha urahisi wa vitendo nasikitegemea Teknolojia muda wote Kwan Kuna vitu vingine hutegemea zaid akili na kisha vitendo, uamuzi mdogo na ufahamu, mdogo unaweza kuleta udhohofishaji wa Teknolojia.

✓ Michakato ya hisabati haifanyiki kiakili Kwan wanafunzi wengi hutegemea kalkuleta ambayo kwa sasa wanafunzi wengi hutumia kama chanzo Cha urahisishaji katika hesabu ,hii huleta uvivu wakufikiria .haikatazwi Bali tunatakiwa tuwe na uzoefu katika pande zote mbili Kwan itatusaidia zaidi katika kuleta maendeleo.

✓ Mtaji wa kibinadamu umepungua, kwa hivyo ukosefu wa ajira umeongezeka katika maeneo ambayo mkono mkubwa wa uzalishaji ulihitajika hapo awali.
Sayansi na Teknolojia imefanya ajira kuwa ngumu licha ya kurahisisha kazi.hali hii imepelekea ukosaji wa ajira na hata kuleta ugumu wa maisha kwa binadamu hivyo basi Sayansi na Teknolojia inatakiwa isipunguze nguvu kazi ya watu kwani inaweza leta athari nyingi baadae Kwani tegemezi la ukuaji ama maendeleo ya nchi. ni watu.

✓ Uharibifu wa mazingira kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya nishati ya viwanda vingi vya kufanya kazi, ambavyo vimechafua maji na bahari.

kutokana halii hii tumekuwa na uharibifu wa hali ya hewa nikiwa na maana hatuna mvua iliyosawia kama zamani mfano mvua zisizonampangilio,joto kuwa Kali sana kutokana na uharibifu wa ozone layer ambao unesababishwa na chlorofluorocarbons na baadhi za mchangamyiko wa gesi zinazotoka viwandani kwa mfumo wa Moshi.

Hitimisho; Ili kupunguza adha zote hizi tunatakkiwa tuwe na mifumo Bora yenye asilimia kubwa ya faida kuliko hasara ..hii itatusaidia kutimiza na kuongeza life expectancy za watu na kukuwa kimaendeleo.
 
Back
Top Bottom