Sauti za wananchi wa Dar kuhusu tatizo la foleni

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,321
33,125
KWA UFUPI
Foleni za magari katika jiji la Dar es Salaam zimezidi kipimo. Baadhi ya wakazi wanaeleza sababu na dawa ya tatizo hilo

Dar es Salaam. Kwa wakazi wa Dar es Salaam, moja ya kero kubwa ni kukithiri kwa foleni za magari barabarani.

Hakuna asiyeguswa na atizo hilo kutokana na ubovu wa miundombinu na kutokuwepo na miundombinu ya kisasa ya usafiri ikilinganishwa na ongezeko la watu.

Ni mkoa unaoongoza kwa watu kupoteza muda mwingi barabarani, kiasi cha kuzorotesha hata utendaji wa kila siku na kuathiri shughuli za uchumi ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Tatizo hili la foleni linaelezewa na wataalamu kwamba husabisha matatizo mbalimbali ya kiafya, ikiwa ni pamoja na watu kupatwa na ugonjwa wa kurukwa akili. Kisa cha haya yote ni foleni hizo ambazo inaonekana wazi kuwa zimekosa mwarobaini wa uhakika.

Hata hivyo, kama sehemu mojawapo ya kukabiliana na tatizo hilo, Serikali inaendelea na mradi wa mabasi yaendayo kasi. Kukamilika kwa mradi huo kunaelezwa kuwa kutasaidia kwa kiasi kupunguza tatizo la foleni barabarani katika baadhi ya maeneo ambayo mradi huo umeyagusa.

Hata hivyo, baadhi ya wakosoaji wanasema kuwa kuwapo kwa mradi huo wa mabasi yaendayo kasi hakuwezi kusaidia moja kwa moja kuondoa tatizo hilo ambalo limeendelea kuongezeka kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu na kupanuka kwa shughuli za kiuchumi.

Gazeti hili limezungumza na wakazi wa jiji la Dar es salaam wa kada tofauti. Wanaeleza wanachojua kama sababu ya foleni hizo, lakini pia kile ambacho Serikali ina vyombo vyake wanaweza kufanya kupunguza au kumaliza foleni.

Ditto Kitwangwa(30)-utingo wa daladala Temeke-Posta:

Chanzo cha foleni katika jiji hili ni barabara kutokidhi matakwa ya ongezeko la vyombo vya usafiri. Lakini pia askari wa usalama barabarani wamekuwa chanzo kutokana na kutumia muda mwingi kuita magari ya upande mmoja.

Kinachotakiwa kufanyika ni kujaribu kuzuia gari ndogo zinazoingia mijini. Nyingi kati ya gari hizi zinakuwa na mtu mmoja, hivyo akitumia daladala atapunguza foleni kwa sehemu kubwa.

William Hussein-Dereva wa gari:

Tatizo la foleni barabarani linasababishwa na uelewa mdogo wa baadhi ya madereva. Unakuta mtu anasimama katikati ya barabara na kusababisha msongamano kwa kuwa barabara hiyo ina watumiaji wengi. Pia kitendo cha kusimamisha gari eneo ambalo hakuna kituo ni moja ya sababu za foleni. Kinachotakiwa kufanyika hapa ni kutoa elimu ya matumizi sahihi ya barabara sambamba na askari kuzingatia sheria za barabarani.
Khamis Suleiman (26) Mfanyabiashara, Mnazi Mmoja:

Tatizo la foleni ni magari makubwa kuingia mijini. Kuna wakati Serikali ilitangaza kuwa magari makubwa yatakuwa yakiingia mjini kuanzia jioni, lakini sasa hadi nyakati za asubuhi utakuta yanaingia.

Kwa upande mwingine, mikokoteni nayo ni moja ya chanzo cha foleni katikati ya jiji. Kinachotakiwa kufanyika ni wahusika kusimamia kanuni wanazozianzisha ili kupambana na kero hii ambayo imekuwa sugu na kusababisha baadhi ya shughuli kutofanyika kwa wakati.

Optatus Vitus (46)-Dereva Taxi, Posta:

Chanzo cha foleni ni matokeo ya huduma nyingi kuwa katikati ya jiji. Unakuta mtu wa Tegeta, Mbagala, Gongolamboto, Kigamboni au Mbezi wote hawa wanaingia mjini. Lakini majengo yanayojengwa hayana sehemu ya kuegesha magari.

Haya yote ndiyo yanayosababisha foleni. Ili kuepuka adha hizi, Serikali iihamishe ofisi zake zilizo katikati ya jiji na majengo yote yanayojengwa yazingatie uwepo wa maeneo ya kuegesha magari, hapo tutakuwa tumeokoka.

Vicent Yona (23) - Dereva wa pikipiki, Buguruni:

Miundombinu iliyopo imepitwa na wakati. Miaka 10 iliyopita magari yalikuwa machache, lakini hivi sasa watu wananunua magari kwa wingi, jambo ambalo linasababisha msongomano katika jiji hili tofauti na miji mingine.

Kinachotakiwa kuboresha barabara za kandokando au zinazopita mitaani kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa zikapunguza tatizo hili ambalo limekuwa chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi kwa kuchelewa kufika katika shughuli zao.

Bakari Omary-Dereva Bajaji:

Barabara zinazojengwa bado hazionyeshi kutatua tatizo la foleni jijini. Mfano barabara kutoka Ubungo kwenda Manzese; mtu akitaka kuingia upande wa pili hawezi, hivyo tatizo la msongamano haliwezi kuisha.Kinachotakiwa ni kuboreshwa kwa barabara za mitaani kwani zina mchango mkubwa wa kusaidia kupunguza foleni, lakini pia kitendo cha askari wa usalama barabarani kusimamisha magari eneo ambalo hakuna kituo ni chanzo cha foleni na ajali hivyo wahusika wawasimamie askari hao ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha.Sauti za wananchi wa Dar kuhusu tatizo la foleni - Habari Ya Ndani - mwananchi.co.tz

Attachments

  • Dar-traffic-jam.jpg
    Dar-traffic-jam.jpg
    22.9 KB · Views: 116
  • traffic.jpg
    traffic.jpg
    24.4 KB · Views: 101
  • bajaj.jpg
    bajaj.jpg
    20.3 KB · Views: 90
Miundo mbinu mibovu sana na kwa kiasi kikubwa inachangia janga hili, ila kuna kanuni moja ya barabara ambayo kila dereva angekuwa anifuata ingesaidia kwa kiasi fulani kupunguza foleni. Mara ngapi tunajikuta tumekwama kwenye foleni kwa sababu gari moja au magari machache yamefunga intersection matokeo yake magari yote hayasogei directions zote? This has to be my pet peeve kwenye matumizi ya barabara hapa mjini.

Simple rule: DO NOT ENTER AN INTERSECTION UNLESS YOU ARE SURE THAT YOU CAN CLEAR IT.

Tatizo kila mtu ana haraka, mtu anaona heri afunge barabara zote ili wote tusimame kuliko asubiri mpaka ahakikishe ana nafasi ya kutosha kuvuka intersection.
 
KWA UFUPI
Foleni za magari katika jiji la Dar es Salaam zimezidi kipimo. Baadhi ya wakazi wanaeleza sababu na dawa ya tatizo hilo

Dar es Salaam. Kwa wakazi wa Dar es Salaam, moja ya kero kubwa ni kukithiri kwa foleni za magari barabarani.

Hakuna asiyeguswa na atizo hilo kutokana na ubovu wa miundombinu na kutokuwepo na miundombinu ya kisasa ya usafiri ikilinganishwa na ongezeko la watu.

Ni mkoa unaoongoza kwa watu kupoteza muda mwingi barabarani, kiasi cha kuzorotesha hata utendaji wa kila siku na kuathiri shughuli za uchumi ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Tatizo hili la foleni linaelezewa na wataalamu kwamba husabisha matatizo mbalimbali ya kiafya, ikiwa ni pamoja na watu kupatwa na ugonjwa wa kurukwa akili. Kisa cha haya yote ni foleni hizo ambazo inaonekana wazi kuwa zimekosa mwarobaini wa uhakika.

Hata hivyo, kama sehemu mojawapo ya kukabiliana na tatizo hilo, Serikali inaendelea na mradi wa mabasi yaendayo kasi. Kukamilika kwa mradi huo kunaelezwa kuwa kutasaidia kwa kiasi kupunguza tatizo la foleni barabarani katika baadhi ya maeneo ambayo mradi huo umeyagusa.

Hata hivyo, baadhi ya wakosoaji wanasema kuwa kuwapo kwa mradi huo wa mabasi yaendayo kasi hakuwezi kusaidia moja kwa moja kuondoa tatizo hilo ambalo limeendelea kuongezeka kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu na kupanuka kwa shughuli za kiuchumi.

Gazeti hili limezungumza na wakazi wa jiji la Dar es salaam wa kada tofauti. Wanaeleza wanachojua kama sababu ya foleni hizo, lakini pia kile ambacho Serikali ina vyombo vyake wanaweza kufanya kupunguza au kumaliza foleni.

Ditto Kitwangwa(30)-utingo wa daladala Temeke-Posta:

Chanzo cha foleni katika jiji hili ni barabara kutokidhi matakwa ya ongezeko la vyombo vya usafiri. Lakini pia askari wa usalama barabarani wamekuwa chanzo kutokana na kutumia muda mwingi kuita magari ya upande mmoja.

Kinachotakiwa kufanyika ni kujaribu kuzuia gari ndogo zinazoingia mijini. Nyingi kati ya gari hizi zinakuwa na mtu mmoja, hivyo akitumia daladala atapunguza foleni kwa sehemu kubwa.

William Hussein-Dereva wa gari:

Tatizo la foleni barabarani linasababishwa na uelewa mdogo wa baadhi ya madereva. Unakuta mtu anasimama katikati ya barabara na kusababisha msongamano kwa kuwa barabara hiyo ina watumiaji wengi. Pia kitendo cha kusimamisha gari eneo ambalo hakuna kituo ni moja ya sababu za foleni. Kinachotakiwa kufanyika hapa ni kutoa elimu ya matumizi sahihi ya barabara sambamba na askari kuzingatia sheria za barabarani.
Khamis Suleiman (26) Mfanyabiashara, Mnazi Mmoja:

Tatizo la foleni ni magari makubwa kuingia mijini. Kuna wakati Serikali ilitangaza kuwa magari makubwa yatakuwa yakiingia mjini kuanzia jioni, lakini sasa hadi nyakati za asubuhi utakuta yanaingia.

Kwa upande mwingine, mikokoteni nayo ni moja ya chanzo cha foleni katikati ya jiji. Kinachotakiwa kufanyika ni wahusika kusimamia kanuni wanazozianzisha ili kupambana na kero hii ambayo imekuwa sugu na kusababisha baadhi ya shughuli kutofanyika kwa wakati.

Optatus Vitus (46)-Dereva Taxi, Posta:

Chanzo cha foleni ni matokeo ya huduma nyingi kuwa katikati ya jiji. Unakuta mtu wa Tegeta, Mbagala, Gongolamboto, Kigamboni au Mbezi wote hawa wanaingia mjini. Lakini majengo yanayojengwa hayana sehemu ya kuegesha magari.

Haya yote ndiyo yanayosababisha foleni. Ili kuepuka adha hizi, Serikali iihamishe ofisi zake zilizo katikati ya jiji na majengo yote yanayojengwa yazingatie uwepo wa maeneo ya kuegesha magari, hapo tutakuwa tumeokoka.

Vicent Yona (23) - Dereva wa pikipiki, Buguruni:

Miundombinu iliyopo imepitwa na wakati. Miaka 10 iliyopita magari yalikuwa machache, lakini hivi sasa watu wananunua magari kwa wingi, jambo ambalo linasababisha msongomano katika jiji hili tofauti na miji mingine.

Kinachotakiwa kuboresha barabara za kandokando au zinazopita mitaani kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa zikapunguza tatizo hili ambalo limekuwa chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi kwa kuchelewa kufika katika shughuli zao.

Bakari Omary-Dereva Bajaji:

Barabara zinazojengwa bado hazionyeshi kutatua tatizo la foleni jijini. Mfano barabara kutoka Ubungo kwenda Manzese; mtu akitaka kuingia upande wa pili hawezi, hivyo tatizo la msongamano haliwezi kuisha.Kinachotakiwa ni kuboreshwa kwa barabara za mitaani kwani zina mchango mkubwa wa kusaidia kupunguza foleni, lakini pia kitendo cha askari wa usalama barabarani kusimamisha magari eneo ambalo hakuna kituo ni chanzo cha foleni na ajali hivyo wahusika wawasimamie askari hao ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha.Sauti za wananchi wa Dar kuhusu tatizo la foleni - Habari Ya Ndani - mwananchi.co.tz

Kwa Morogoro road ndiyo more worse, kwa muda wa asubuhi madereva wawili wanaweza kuondoka muda mmoja Mbezi, mmoja akaelekea mji kasoro bahari, Morogoro na mwingine akaelekea katikati ya jiji posta, lakini ajabu na kweli ni kuwa yule anayekwenda Morogoro atatangulia kufika round about ya Msamvu kabla ya yule anayekwenda maeneo ya katikati ya jiji posta hajamaliza hata kuvuka maeneo ya Akiba!!!
 
Foleni ni majanga na ni talk of the day everyday. Hayo yaliyosemwa na wadau wa sauti ya wananchi wa dar kuhusu tatizo la foleni ni kweli yanachangia sana tatizo la foleni. Tukijaribu kurekebisha hayo foleni itapungua kiasi chake. Kuongeza Kujenga barabara mpya na kupanua zilizopo si suluhisho la kudumu kama hakutakuwa na projection la ongezeko la traffic kwa miaka labda 50 ijayo, kwani traffic huendelea kuongezeka mpaka ile peak congestion inarudi kama ilivyokuwa mwanzo. Ikumbukwe pia kuwa si kila mtu anapenda kwenda na gari kwenye shughuli zake za kila siku, hii ni kwakuwa tu public transport yetu ipo ovyo sana. So, iwapo public transport itakuwa nzuri na ya uhakika (kufika kwa muda na usalama toka kwa vibaka), watu wengi watapaki magari yao nyumbani na traffic jam itapungua kwa kiasi kikubwa. Kwakweli foleni ni majanga.
 
Barbara za pembeni zote ziwe na lami.mfano sinza/kijitonyama zote za pembeni hazijaboreshwa.ni tofauti sana na ilala au temeke.kumzuia mtu kutumia gari lake eti apande daladala si sawa.ifike hatua serikali ijenge flyovers.
 
Back
Top Bottom