sauti za mungu..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sauti za mungu.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by M4C ARUSHA, Apr 30, 2012.

 1. M

  M4C ARUSHA Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SAUTI ZA WABUNGE HAWA NI SAUTI ZA MUNGU
  HUWEZI KUWA MASKINI KWA KUKATAA SERIKALI ‘TATA”
  NA Gift Mongi

  KAMA kweli wabunge ndio wawakilishi wa wananchi, serikali sasa itaondoa pamba masikioni, itawasikiliza na kutekeleza wanachopendekeza kwani mbunge ndio mwakilishi wa wananchi katika jimbo husika.

  Kwa siku nyingi sasa, kilio cha wabunge kuhusu mikataba ya madini na mikataba mingine mikubwa, kimezidi kiwango huku serikali inayoongozwa na chama cha mapinduzi ikiwa inajidai kuweka pamaba masikioni.

  Kilio chao kimevuka mipaka ya kawaida. kimewagusa hata wale ambao hawakuwa na shauku ya kukisikia hii inatokna na wizi uliokithiri kwani ulianza mamilioni ,ukaja mabilioni msasa tupo katika matrilioni.
  .

  Wabunge wanataka mikataba ipitiwe wanataka kujua kilichomo kwenye mikataba hiyo. Serikali haiwakilishi wananchi. bunge ndicho chombo cha wananchi sasa sisi wananchi wa chini tuende wapi?.

  Wabunge wanapojadili jambo lenye manufaa kwa nchi, wanafanya hivyo kwa niaba ya wananchi wao huku wachache wao wasiojua wakibaki kuguna na kutoa minong’ono isiyokuwa na tija.

  Haiwezekani wabunge wapige kelele za kutaka kupitiwa mikataba, lakini serikali iendelee kuwa jeuri huku ikiendelea kuwakingia vifua watu wanodaiwa kuhusika katika mikataba tata.

  Awamu ya Tatu ya uongozi wa taifa hili ilitamba kwa kaulimbiu hewa ya uwazi na ukweli japo hapakuwa na uwazi wala ukweli hii vipi sasa mbona mnatofautiana nyie viongozi wa chama cha mapinduzi.

  Mikataba ilisainiwa wageni wakamilikishwa mali za taifa mikataba mingi ya kipuuzi kabisa ikasainiwa mzigo wa mikataba hiyo sasa unabebwa na walipa kodi wa nchi hii ambao wengi wanaishi chini ya dola moja.

  Serikali haikuwa wazi ilipuuza maoni ya wananchi, na hata ikafikia hatua ya kuwatisha wabunge waliosimama kidete kuhoji uozo fulani Fulani huku nguvu nyingi zikitumika katika kuhakikisha kuwa hawatashinda katika uchaguzi mkuu.

  Inasikitisha, na kwa kweli inakasirisha, kumsikia leo Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, akiunga mkono kupitiwa upya kwa mikataba ya madini inamaana wakati wa uongozi wake ilisainiwa bila kusomwa au lugha leo hii imebadilika?!

  Yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kuponda wote waliohoji mikataba hiyo, hata akafikia hatua ya kuwaita waliohoji kuwa ni wavivu wa kufikiri eti akili zao ni Ndogo kamwe hawawezi kujua.

  Waandishi wa habari walioandika au kuhoji mikataba hiyo, walionekana si wazalendo, na ni watu wasiokuwa na maarifa yoyote kwani huenda kwa sababau anko Ben alikuwa na taaluma hiyo ya uandishi.

  Serikali ya Awamu ya Tatu ilijaa ujuaji na ubabe. Net Group Solution walipingwa mno. Watanzania wengi walisimama kuipinga kampuni hiyo na hata wakurugenzi wake ambao wengi walikuwa ‘vihiyo’.

  Lakini kilichofanywa na serikali ni kuwaita FFU wenye bunduki na gesi za kutoa machozi, kuwasindikiza Wazungu hao hadi ofisini eti waliitwa na bosi tayari kwa kwenda kusaini mikataba hiyo na kuanza kazi.

  Kimsingi yamefanyika mambo mengi ya ajabu katika nchi hii ndiyo maana tunasema kilio hiki cha wabunge sasa, lazima serikali ikifanyie kazi tena kwa wakati ili tuweze kuwa na viongozi ambao ni waadilifu.

  Miktaba ya kipuuzi, kwa mfano ya kuukodisha Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwa dola 1,000 kwa mwaka, ni laana isiyosameheka mbele ya Mola au hata mara nyingine shetani anaweza kuikimbi dhambi hii iliyokithiri

  Hivi kweli Tanzania kwa utajiri wake ina sababu ya kuomba misaada mingi kama ilivyo sasa? Je, kwa ukwasi uliopo, kuna sababu ya watu kufa kwa magonjwa kama malaria?au wanawake wajawazito kulala chini?

  Laana ya Tanzania ni nini? Je, si kweli kwamba laana ya Tanzania ni viongozi jeuri na wasioambilika? Kama kweli sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, basi sauti hii ya wabunge lazima iheshimiwe. Serikali ipeleke mikataba bungeni ijadiliwe.

  Nchi inashuhudia ufisadi kila kona, zimeibuka kashfa nyingi, mara Richmond mara EPA (Akaunti ya Madeni ya Nje) na nyinginezo. Kabla ya kufika kwenye hiyo ya EPA, huu msamiati mpya wa ufisadi wewe unakugusa vipi?

  Ndio, nasema wananchi sasa tunataka majibu ya ki-uchunguzi juu ya Richmond, Dowans, Meremeta, IPTL na nyinginezo ili sote tupate kuanza upya katika ukurasa mpya kama taifa.

  Ndio,pale ambapo vyama vinavyowafadhilini kushika nyadhifa za umma zinaposhindwa kutolea maamuzi mambo nyeti na kero kubwa kama haya kwa taifa maana yake ni kwamba sasa maamuzi lazima yapatikane toka nje ya hicho chama fadhili.

  Mwisho…….
   
Loading...