Sauti ya wenye viwanda juu ya vikwazo vya biashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sauti ya wenye viwanda juu ya vikwazo vya biashara

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Orton, Jul 19, 2012.

 1. O

  Orton Guest

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sauti ya wenye viwanda juu ya vikwazo vya biashara Ni kweli kwamba sekta za umma na sekta binafsi zinashirikiana kwa karibu sana, na zote zina lengo la kuifanya Tanzania iwe chaguo la wengi katika suala zima la uwekezaji, kwa wawekezaji wote wa ndani na watokao nje ya nchi. Hata hivyo, bado matokeo hayaridhishi kwani ushirikiano unaonyesha kuwa kumekuwepo na mabadiliko madogo kama yanavyoonekana kwenye Ripoti ya Biashara ya Benki ya Dunia ambapo kwa mara kadhaa Tanzania imekuwa ikishika nafasi ya chini. Ripoti hizi zinaonyesha kuwa, Tanzania ni mahali pagumu sana katika kuwekeza na kufanya biashara.

  Ripoti ya Mitazamo ya Viongozi wa Biashara ambayo imetolewa kwa lengo mahsusi la kuchukua maoni ya jumuiya za biashara za Tanzania pia imeainisha ugumu uliopo wa kufanya biashara nchini, na miongoni mwa changamoto zilizoainishwa ambazo ndio zimeonekana kuwa kero kubwa katika kukwamisha uendeshaji biashara ni pamoja na umeme, barabara, maji, na rushwa. Kuna ripoti nyingine pia zimeelezea ujumbe huo huo ya kuwa: sio rahisi kufanya biashara nchini Tanzania. Na Mkrugenzi Mtendaji wa Tanzania Industries(CTI) Christine Kilindu
   
Loading...