"Sauti ya Wanyonge... Ni Wanyonge Wapi Hawa?" 🤔

"Sauti ya Wanyonge... Ni Wanyonge Wapi Hawa?" 🤔

888I

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
445
Reaction score
553
Huwa naliona gazeti Wamachinga likijinasibu na kauli mbiu yake: “Sauti ya Wanyonge.”
Lakini mara nyingi kurasa zake za mbele zimepambwa na sura za viongozi wakubwa wa kisiasa, watu wenye nafasi kubwa serikalini, pamoja na mabwenyenye wenye ushawishi wa kifedha na kiserikali.

Sasa najiuliza: wanyonge gani hasa wanapewa sauti katika gazeti hili?

Je, ni wale mama lishe, machinga mitaani, bodaboda, wakulima na wavuvi wanaotaabika na gharama za maisha?

Au “wanyonge” hawa wanaozungumziwa ni hao wanasiasa waliopo madarakani na matajiri wenye nafasi ya kupiga picha ukurasa wa mbele?

Ikiwa kweli gazeti lina kauli mbiu ya “sauti ya wanyonge,” kwa nini mara chache sana tunaona simulizi za wananchi wa kawaida, changamoto zao, na kilio chao kikipata nafasi kubwa ukurasavwa mbele?

Au labda tafsiri ya “wanyonge” katika uandishi huu imebadilishwa — kwamba mwenye nguvu akijipa taswira ya “mnyonge,” basi ndiye anayepewa kipaumbele?
 
Attachments

  • 20250828_061054.jpg
    20250828_061054.jpg
    160.1 KB · Views: 16
Sijui lakini Hadi kuna miradi ya kuwainua mfano TASAF n.k
TASAF? Tanzania Social Action Fund phase lll ni kwa ajili ya kusaidia kaya zenye uchumi wa chini/hafifu ambao nyakati zingine hata kupata milo mitatu ni changamoto.Basi,ingefaa na kupendeza sana iwapo majarida/machapisho ya TASAF,ambayo huwa yanatolewa bure,ndiyo yawe na kauli mbiu ya sauti ya wanyonge na siyo vinginevyo.Gazeti linaitwa SAUTI YA WANYONGE halafu linahitaji linunuliwe kwa mapesa?Huo siyo unyonge ni usanii.
 
Chombo Cha habari" ni sahihi kabisa kuwa Sauti ya wanyonge kwani Chombo Cha habari ni Sauti kwa wasio na Sauti na wale wasio na Sauti wanakutanishwa na wenye Sauti (wanyonge na viongozi)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom