mululu
JF-Expert Member
- Nov 7, 2014
- 749
- 406
Kwanza nakupongeza mh Rais kwa jitihada zako za kuendelea kuijenga nchi, sisi wakulima tunakufuatilia kwa karibu sana na tunakutakia kheri uweze kufanikiwa katika yote uliyopanga kulifanyia taifa letu.
Mimi kama mukulima mpya katika sekta hii nimeona ni vema nami nitoe ya moyoni nilichokiona kwakweli. Serikali yako inawahimiza sana vijana kufanya kazi na hasa kilimo, lakini kilichopo huku kinakatisha tamaa kabisa. Ingawaje nimekufatilia mara kadhaa ukizungumzia kero za mkulima kuwa ni ushuru wa mazao na kucheleweshewa pembejeo lakini kwakweli shida yetu kubwa sisi wakukulima ni masoko na bei ndogo ya mazao yetu. Natoa mfano
Wakulima wa Mpwapwa tuna mazao makuu 4 ya biashara ambayo ni Karanga, ufuta, alizeti na vitunguu, naenda kuzungumzia karanga na ufuta kama mazao yanayolimwa zaidi.
Karanga ndilo zao kongwe ambalo wilaya hii inalima toka enzi za mkoloni, kipindi fulani mpaka mwaka 2012 lilichangia kwa kiasi kikubwa sana kukuza uchumi wa wanaberege na mpwapwa kwa ujumla, tuliweza kuuza kg 1 kwa tzsh mpaka 2500 ilishuka mwisho 1520 kwa kg, lakini miaka iliyofatia zao hili limeshuka kabisa bei na kupelekea watu kuacha kabisa kulilima, sisi hatujuwi tunaskia tuu kwamba kuna meli hutoka arabuni kuja kununua karanga, sasa tunaomba hiyo meli kama ipo hapo bandarini tufanyie wepesi iruhusuni ije kuokoa jahazi jamani, tunalima kwa gharama kubwa sana, kuuza kg kwa sh 1100 ni hasara kubwa kwetu sisi wakulima.
UFUTA, zao hili limeibuka na kushika kasi miaka ya 2008/9 na kuinua kabisa vipato vyetu, ukija kijiji cha berege kitongoji cha Vinolo ambako ufuta unalimwa kwa wingi, makaazi ya wananchi yamebadilika kabisa, zimejengwa nyumba bora na za kisasa, vijana wameezeka bati na solar panel kila nyumba, giza liingiapo panakuwa peupe kama mchana.
Mwaka 2012/13 kilo moja ilikwenda mpk kwa sh 3500 kiloba kimoja cha kilo 100 kiliweza kumpatia mtu lak 3.5, aliyelima eka 5 tuu alikuwa na uwezo wa kujenga nyumba na kununua pikipk.
Lakini sasa hali sio hali, soko limefungwa kabisa, badala yake sasa kijjn kwetu wapo tuu walanguzi, wananunua ufuta kwa ujazo, debe moja lenye wastani wa kg 20 wananunua kwa tsh 20000 yaan wastani wa sh 1000 kwa kilo, wakulima tumekata tamaa, tukiulzia dodoma mjini tunaambiwa meli ya kununua ufuta haijafika.
Ushauri wangu kwa washauri wa rais wa uchumi, wakati mnazibiti uingizaji wa meli bandarini, zinazokuja kununua mazao ya wakulima ziruhusiwe hima, mbegu bora ya ufuta LINDI 02 tumenunua kwa tsh 20 elfu kg2 sasa debe la kg 20 linauzwa kwa sh 20 elfu inauma sana.
Mkulima wa Berege
0714174235