Chozi na Damu ya Haki
New Member
- Jan 17, 2026
- 1
- 4
Ee Mungu wa Haki na Amani ya kweli. Tunakupigia magoti. Ninakupigia magoti. Ninasujudu mbele yako ewe Muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo. Ewe mwenye mamlaka pekee ya kutoa na kutwaa uhai wa mwanadamu uliemuumba. Taifa letu limepitia maumivu makali yasiyoisha wala kusahaulika katika uso wa Dunia hii. Waliotekeleza haya bado wameendelea kudhihaki haki na amani kwa kejeli na kiburi cha mamlaka za kibinadamu. Wameshika mpini, sisi tumeshika makali. Mtetezi wetu ni wewe pekee. Ombi ni moja tu kwako Mungu Muumba wetu.
Kwa kuwa wamechagua dhihaka na kufuru. Kwa upofu waendelee kushupaza shingo na kujiinua, wafuje mali na madaraka na kulimbikiza kupita kipimo mpaka anguko lao kuu. Nyoosha mkono wako, ili mzigo huu wa maumivu makali na machungu ya kukosa haki na stahiki za utu, ukandamizaji na uonevu, uovu uliopitiliza ukawatue na kuwaponya wanyonge.
Na Mzigo huu wakaubebe wahusika wa ukatili na uovu huu unaoendelea, wao na vizazi vyao, damu iliyomwagika ikawe laana kuu kwao na vizazi vyao. Haki na stahiki za utu zinazominywa kwa uovu na kiburi ikawe laana kwao na vizazi vyao. Wakamwage damu zaidi, wakateke na kutesa zaidi mpaka watakapokutana na uso wako. Amani yao na furaha isiyodumu ikawe ni kuona wameshinda ilihali maelfu ya wananchi wa Taifa hili wanateseka na kukosa haki na stahiki muhimu ikiwamo huduma bora za kijamii.
Hakuna watakalofanya kuponya nafsi zao na nafsi za raia litafanikiwa kwani damu ya viumbe wako bado inalia ardhini na majini. Wakaisikie harufu hii kali toka ardhi mpaka bahari na mito iliyobeba thamani ya damu hii na machozi ya haki. Wakila nyama waisikie na kuhisi harufu kali ya damu ya haki ikiwadai wao na vizazi vyao, kwenye nafsi zao, kwenye mioyo yao, kwenye roho zao, wakikaa kwenye viti vya enzi na mamlaka, wakihutubia, wakiwa wapweke wakitafakari matendo yao na kujivunia faida waliyovuna, wakifanya maamuzi ya kuumiza na ukandamizaji, wakilala na kupumzika, wakitembea, wakisimama, wakikaa, wakijaribu kujipa furaha na kuitafuta amani ya nafsi, wakikaa kwenye meza kuu na kujipongeza kwa uovu na ufujaji, wakijisifu na kusifiwa, wakijigamba na kukejeli.
Wakasikie sauti za vilio na damu iliyomwagika kila sekunde iendayo kwako. Dunia hii tunapita, mali na mamlaka tutaviacha hapa duniani. Wasiisikie salama hata kama wanalindwa na vifaru. Hatuna pakukimbilia ila katika mikono yako salama Ee Muumba wetu. Hatuna uwezo wa kupigana ila kupitia mkono wako wenye nguvu kuu, jeshi lako lenye nguvu, na hukumu yako ya haki kwani kwako tutashinda kwa wakati. Ikikupendeza, uwape maisha marefu washuhudie Utukufu na Ukuu wako ukishuka katika Taifa hili. Waliotelekeza na walioruhusu haya yatokee, kufunika na kuacha yaendelee katika nafasi zao za kiutawala wakatumikie kifungo hiki na kubeba mzigo mzito uliobebwa katika mioyo na nafsi za wanaokulilia katika unyonge wao Ewe Muumba, Ewe Mwenyezi Mungu, Ewe ulie Ukuu na Mamlaka ya mbinguni na duniani.
Wakafitiniane na kusalitiana wao kwa wao. Wenye hofu ya Mungu wakakiri hadharani na kujiuzuru kuepuka gadhabu yako na manung'uniko ya walioumizwa. Ukasimame na waliotekwa na kuteswa hata kusababishiwa ulemavu, kumbukumbu inayoumiza na kuwekwa gerezani kwa makosa ya kupika, Ee Mungu Muumba ukafanyike faraja, nguvu na uponyaji. Ukawafariji ndugu jamaa na marafiki.
Wasikate tamaa kudai haki, ukabebe mateso yao na maumivu yao. Kila wanapotendewa hayo ukasimame badala yao, kwani wao pekee hawawezi kuhimili mateso na manyanyaso toka kwa watawala na watendaji wadhalimu, waovu wenye tamaa, uroho na ulafi, waliojaa ufisadi na rushwa. Mapenzi yako na yatimie kwa kuwa wewe pekee ulizijua hizi nyakati hata kabla ya uumbaji. Nyakati ambazo zilipaswa kupita ili yapate kutimia.
Amina. Amina. Amina.