Sauti inayodaiwa ni ya Mzee Makamba na Mwanaye January Makamba kuhusu Waraka

Mnamshambulia nini wakati clip ipo hapo.!

Ila hii kweli ya kutengeneza, eti Mzee Makamba anamuuliza Januari nani anakupikia hapo nyumbani unamfanyakazi?

Hivi mtu kama Januari atakosa mfanyakazi ama msaidizi nyumbani...

Hii ni Part 4, part 5 lini?


Mzee anajaribu kuchukua tahadhari zote. Hawa wasaidizi wa nyumbani wakati mwengine ni wazembe Aweza kuachia mbwa koko kuzurura ovyoo kama yule wa Kingunge rip.
 
DJ Khaleeeeed, another one...

Sina chama sina kundi, nawakilisha ufundi.

1. Kudukua mawasiliano ya watu kwa sababu za kisiasa ni jambo baya sana.Marekani walimuondoa raiwa wao Nixon kwa kesi iliyohusu mambo haya.

2. Hizi audio zinavyozidi kutolewa ndiyo zitazima lile kanuso la "ni feki hizi". Hii nayo feki?

3. Udukuzi wamefanya wengine, na audio ziko katika public arena, lakini bado nimejisikia vibaya kusikiliza, hususan kwa kuwa hakuna mazungumzo ya kustahili kudukuliwa, watu tu wanapanga kuchapisha habari zao magazetini, kitu ambacho ni haki yao ya kikatiba.

4. Kibaya zaidi ni kudukuliwa kwa maongezi yaliyokaa kifamilia zaidi.
 
Hamna hata sauti moja ya kugushi, ni kwamba watu ni wanaume wameona wanageuzwa warembo na mtu waliyemsadia kushinda kwa kura za wizi. Wameamua kusimama kiume kwani hawako tayari kulambishwa mchanga.
ndo wakaamua kujirecord? Tatizo wanaonekana kuzidiwa nguvu katika mambo ya ushushuu hadi mipango yao inavujishwa kabla haijafika mbali. Mimi nadhani hata hili la kuvujisha voice note zao ni amri kutoka juu. Yani anatafuta uhalali wa wakufanya atakachokifanya kabla hajafanya ya kukifanya.
 
Back
Top Bottom