SAUT main campus inaongoza kwa kuwa na Wanafunzi wasio na sifa

Nibozali

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
572
1,055
Ukiangalia orodha iliyotolewa na TCU Saut mwanza ina idadi kubwa ya wanafunzi ambao wanaosoma bila sifa.

Angalia orodhayao hapa chini inatisha
 

Attachments

  • SAUT.pdf
    292.5 KB · Views: 175
Nibozali labda huijui SAUT vizuri, hata kama kuna majina mengi, nakwambia vyuo vya SAUT bado havijafikia kiwango cha kudahili wanafunzi unaowaita "vilaza"
 
Hiyo lugha ya vilaza si nzuri mkuu na pia ukumbuke udahili wa mwanafunzi yeyote kuchaguliwa chuo hufanywa na hao hao TCU.
Udahili unafanywa na TCU ila mandate kumkubali au kumkataa mwanafunzi wanayo Chuo kwan huon muhimbili hia wanafanyaje???? Kwahiyo usitetee ujinga
 
Wanafunzi zaidi ya 7000 katika vyuo vya elimu ya juu mbalimbali hapa Tanzania wanakabiriwa na hatari ya kufutiwa udahili katika vyuo hivyo iwapo watashindwa kuthibitisha sifa zao za kitaaluma zilizowawezesha kupata udahili katika vyuo hivyo.
kamisheni ya vyuo vikuu (TCU) imetoa orodha ya Wanafunzi hao na kuwataka kuthibisha sifa zao kitaaluma ndani ya siku saba au watafutiwa udahili katika vyuo wanavyosoma.
Hilo linatokana na kukamilika kwa uchunguzi ili kuthibisha na kujiridhisha kuhusu sifa za kitaaluma za wanafunzi katika vyuo vikuu.
Idadi ya wanafunzi na chuo wanachotoka ni kama ifuatavyo:
St Agustine University 1064
St John university 968
State University of Zanzibar 966
Mzumbe university 639
Iringa university 522
Sumait university 552
IRDP 431
CBE Dodoma 375
IFM 305
Arch James University 27
Arch Mihayo University 33
Ardhi University 23
College of Wildlife Management 6
CBE Mwanza 101
COMMUNITY DEVELOPMENT TRAINING INST. 14
Tanzania centre for foreign relations 8
Catholic University 36
DIT 61
Dmi 4
EAsTC 20
EckenfordeTanga 3
HUBERT KAIRUKI 12
IAA 56
IMTU 49
ISW 116
Institute of Tax Adminstration 6
Jordan University 186
UDSM 224
UDOM 52
St Joseph 1
Sebastian Kolowa 150
KCMUC 55 na vingine vingi (soma Daily News la 23 February

Aidha TCU imesema pia orodha ya majina ya wanafunzi walio na shaka imetumwa kwa vyuo husika ili wanafunzi hao waone majina yao.

Source: Daily News 23 FEBRUARY 2017
 
Naona kunguru wanajitenga na njiwa, hapo UDOM na UDSM hazipo. Siamini kama kwenye "na vingine vingi" kwa materiality and brand zitakuwa zimefichwa humo!
ingelikua vyema na wewe ungefanya utafiti wako ili uwaumbue kwani Tafiti hupingwa kwa tafiti
 
Nimesikia wanafuatilia na wale waliohitimu tayari...!!

Hivi hii Awamu kwa nn inachimbua makaburi?

Ukimfutia mtu aliyehitimu tyr lazima aende mahakamani maana hakujipeleka mwenyewe huko chuoni.

Wanafunzi wanaoendelea na masomo kwa sasa wapo kwenye mtihani, sasa TCU hawaoni kuwa Tangazo lao lita-wafrustrate wanafunzi wengi waliopo kwenye mitihani?

hatukatai hili zoezi kufanyika, ila lazima busara, utu, na ubinadamu kama upo utumike.
 
Back
Top Bottom