TANZIA Mwanafunzi SAUT afariki akiwa ameenda kuogelea ziwani

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
220
495
Mwanafunzi Wa Chuo kikuu Cha SAUT Campus ya Mwanza Amefariki Dunia Alipokuwa Ameenda kuogolea Kando Kando Kando ya Ziwa Victoria Maeneo ya Sweya Beach.

Taarifa hiyo ilitolewa Na Wenzake Ambao walikuwa wameenda Nao kuogolea katika Maeneo hayo ya Kando kando ya Ziwa Na Na Kifo hicho kimetokea Jana Siku ya Mei Mosi Ambako Wanafunzi walikuwa Hawana vipindi Madarasani.

Boaz Sanga Alikuwa Mwanafunzi Anayesoma Shahada ya Kwanza katika Fani ya Ualimu Kwa Mwaka wa Kwanza (BAED 01)

Katika Hatua Nyingine Mwili wake Ulitolewa Ziwani Leo Na Jeshi La Uokoaji Kanda Ya Mwanza Mara Baada ya Jana Kuzama na Kushindwa kupatikana kutoka Na sababu Zilikuwa kuwa Nje ya Uwezo.

Baadhi ya Wakazi katika Maeneo ya Sweya Wanasema Kuwa Imekuwa Ni Desturi kwa Wanafunzi wanao Soma SAUT kuja Kuogelea Katoka Hayo Maeneo kipindi wawapo masomoni Wakirejelea Kipindi Cha Mapumziko Ama Siku za Mwisho wa juma (Week end) huwa kuna Idadi kubwa ya Wanafunzi.

Vile vile Wanasema Wanafunzi wengi hupendelea kuja Kupiga Picha Na Kukaa Nyakati za Jioni
Taarifa iliyochapishwa leo na akaunti ya mtandao wa Instagram ya chuo hicho @sautv_ imeeleza kuwa, Sanga alikuwa mwanafunzi wa kitivo cha Elimu SAUT.

“Taarifa za awali zilizotelewa, zoezi la kumtafuta lilianza jana usiku bila mafanikio,” imeeleza taarifa hiyo.

Akielezea namna mchakato wa uokoaji ulivyofanikiwa, Kamanda Zimamoto na Uokoaji jijini Mwanza, Kamila Laban amesema maaskari wabobezi wa uzamiaji wa jijini humo walipata mwili wa Sanga katika ukiwa umekwama katika mapango ya ziwa hilo.

Chanzo:Taarifa Na ME
 
Alishindwa kutulia hostel au ghetto kwake? Hao wenzake walishindwa vipi kumuokoa akiwa anapigania uhai wake?

Mambo mengine mbona yanaepukika kabisa!! Polee kwa wafiwa.

Rip dear!!
Umejuaje kuwa alikuwa na wenzake au alikuwa mwenyewe ziwani.
 
View attachment 2978800 Mwanafunzi Wa Chuo kikuu Cha SAUT Campus ya Mwanza Amefariki Dunia Alipokuwa Ameenda kuogolea Kando Kando Kando ya Ziwa Victoria Maeneo ya Sweya Beach.

Taarifa hiyo ilitolewa Na Wenzake Ambao walikuwa wameenda Nao kuogolea katika Maeneo hayo ya Kando kando ya Ziwa Na Na Kifo hicho kimetokea Jana Siku ya Mei Mosi Ambako Wanafunzi walikuwa Hawana vipindi Madarasani.

Mwanafunzi Aliyefariki Anasoma Shahada ya Kwanza katika Fani ya Ualimu Kwa Mwaka wa Kwanza (BAED 01)

Katika Hatua Nyingine Mwili wake Ulitolewa Ziwani Leo Na Jeshi La Uokoaji Kanda Ya Mwanza Mara Baada ya Jana Kuzama na Kushindwa kupatikana kutoka Na sababu Zilikuwa kuwa Nje ya Uwezo.

Baadhi ya Wakazi katika Maeneo ya Sweya Wanasema Kuwa Imekuwa Ni Desturi kwa Wanafunzi wanao Soma SAUT kuja Kuogelea Katoka Hayo Maeneo kipindi wawapo masomoni Wakirejelea Kipindi Cha Mapumziko Ama Siku za Mwisho wa juma (Week end) huwa kuna Idadi kubwa ya Wanafunzi.

Vile vile Wanasema Wanafunzi wengi hupendelea kuja Kupiga Picha Na Kukaa Nyakati za Jioni
Chanzo:Taarifa Na ME
Hao wenzake walikuwa wangapi na walikuwa wapi wakati mwenzao anazama? Maeneo hayo hapakuwa na watu wengine zaidi wakati wa tukio lilipotokea? Walipiga yowe ya kuomba msaada? Wanafunzi hao ni wa jinsia gani kwanza?
Isije ikawa kazamishwa makusudi kwa ajali ya kutengenezwa ktk harakati za vijana za kugombea Wanawake au Wanaume huko vyuoni, Kama ilivyotokea kwa kijana fulani hivi huko mwanzoni mwa miaka ya 2000's! Ukweli wa tukio hilo ulikuja kujulikana baadaye Sana.
 
Alishindwa kutulia hostel au ghetto kwake? Hao wenzake walishindwa vipi kumuokoa akiwa anapigania uhai wake?

Mambo mengine mbona yanaepukika kabisa!! Polee kwa wafiwa.

Rip dear!!
Ziwani na kwenye mabwawa ya maji huwa Kuna majini na mashetani ambayo Kuna muda ukifika lazima yaondoke na damu.

Miezi miwili nyuma Kuna rafiki yangu alikufa baada tu kuingia kwenye bwawa kuogelea yaani ile kujilusha kwenye maji hajaibuka tena.
 
Hao wenzake walikuwa wangapi na walikuwa wapi wakati mwenzao anazama? Maeneo hayo hapakuwa na watu wengine zaidi wakati wa tukio lilipotokea? Walipiga yowe ya kuomba msaada? Wanafunzi hao ni wa jinsia gani kwanza?
Isije ikawa kazamishwa makusudi kwa ajali ya kutengenezwa ktk harakati za vijana za kugombea Wanawake au Wanaume huko vyuoni Kama ilivyotokea kwa kijana fulani hivi huko mwanzoni mwa miaka ya 2000's!
Hakika uchunguzi ufanyike, hao wenzake wabanwe waeleze ukweli.
 
Ziwani na kwenye mabwawa ya maji huwa Kuna majini na mashetani ambayo Kuna muda ukifika lazima yaondoke na damu.

Miezi miwili nyuma Kuna rafiki yangu alikufa baada tu kuingia kwenye bwawa kuogelea yaani ile kujilusha kwenye maji hajaibuka tena.
Duuuh inaumiza sanaa!! Nilishataka kufa na maji.
Naheshimu sana vyanzo vya maji yanayotiririka.
 
Alishindwa kutulia hostel au ghetto kwake? Hao wenzake walishindwa vipi kumuokoa akiwa anapigania uhai wake?

Mambo mengine mbona yanaepukika kabisa!! Polee kwa wafiwa.

Rip dear!!
We nae sasa atulie Hostel kufanya nini aache kurelax beach. Mbona wewe kuna muda humu unachangia mada kwenye thread za kukulana unaacha kutulia jukwaa la thread serious
 
Alishindwa kutulia hostel au ghetto kwake? Hao wenzake walishindwa vipi kumuokoa akiwa anapigania uhai wake?

Mambo mengine mbona yanaepukika kabisa!! Polee kwa wafiwa.

Rip dear!!
Siku yake ya kufa ilishafika kusingekuwa na namna yoyote ile yakubailisha ilo

Na sio kila anaezama kwenye maji huzama kwa pupaa mda mwingine mtu anaweza kuzama na msiwe na habar mpk ule mda wa kutaka kuondoka ndo mnajua kuwa fulani mbona hatumuoni kumbe alishazama kitambo sana
 
Mmmh bas sawa.
 
Back
Top Bottom