Saudi state-owned media warns Russia will exploit vacuum if US imposes sanctions

UAE imeingiaje hapa,mbona ni vitu viwili tofauti kabisa na saudi arabia?
Thanks mkuu kwa kunirekebisha. Nimesha-edit kosa mkuu. Nilimaanisha SAUDIA-ARABIA na siyo UAE. Nilikuwa nacheki CNN walikuwa wanaonyesha documentary moja kuhusu UAE. So nikatekwa akili na roho (Kidding bro)
 
Wakati wa marekani wa Manzese wakipambana mitandaoni kuonesha Marekani hatishwi na tamko la Saudia,
Wamarekani wenyewe wanaelekea Saudia kubembeleza mambo yasifike mbali
 
Thanks mkuu kwa kunirekebisha. Nimesha-edit kosa mkuu. Nilimaanisha SAUDIA-ARABIA na siyo UAE. Nilikuwa nacheki CNN walikuwa wanaonyesha documentary moja kuhusu UAE. So nikatekwa akili na roho (Kidding bro)
poa poa,na wala nafikiri mafuta yame run out pale na ndio maana mkuu wa nchi yao aliamua wawekeze kwenye utalii ikiwa kama mbadala wa oil economy na ndio maana umeona jamaa wana ndege ndege za kutosha za emirates hata vile visiwa vya umbo la dunia walijenga kwa ajili hiyo
 
Wakati wa marekani wa Manzese wakipambana mitandaoni kuonesha Marekani hatishwi na tamko la Saudia,
Wamarekani wenyewe wanaelekea Saudia kubembeleza mambo yasifike mbali
hapo sasa ndio ushangae mkuu,pompeo katumwa kule akarekebishe mambo,marekani anajua athari za kumpoteza saudia na akimpoteza kwa jinsi ninavyowajua waarabu watachukua maamuzi magumu sana na petro dollar itakufa kabisa

Trump sio mjinga wa kuruhusu hili na alisema kabisa juzi kwamba hawezi kuacha dili la silaha la kuwauzia saudia kwa maana wapinzani wake russia na china watalichukua
 
Hizi ni fictions tu na propaganda za IMF ili China waendelee kuwekeza kwao. Yuan hii ambayo sasa hivi inashuka thamani kufuatia effects za zile US trade tariffs eti ndio iwe "Reserve Currency".!! Acheni utani bwana.
 
marekani akivuruga bei ya mafuta shida itakua kwake,mafuta huwa yakipanda bei dollar huwa inashuka chini ndio maana kama umeona siku za hivi karibuni trump analalamika mafuta ni bei ghali na wakati yeye ndio kasababisha iwe hivyo sababu kawawekea vikwazo moja ya wazalishaji wakubwa ikiwapo iran na venezuela

kwa hiyo hata kama akapandikiza islamic state pale na kukatokea vurugu hapa marekani in longrun atapata hasara na yeye pia sababu atakua kawazingua karibia wazalishaji wakubwa wote wa mafuta duniani

na hawa atakao wazingua kuanzia huyo saudia,Venezuela, russia,iran na iraq wote hawa wataenda kwa china na ndio hapo sasa china atapata energy kiulaini kabisa na kukuza uchumi wake vizuri zaidi

hivi vikwazo mzee baba in longrun vitamfaidisha mchina kwa kiasi kikubwa sababu atakua anazoa tu marafiki waliozinguliwa na marekani
 
bora uwaaambie mkuu na saudia kasema yeye ana influence kubwa sana kwenye muslim world ambao inturn ndio opec members wenyewe ukimtoa russia na russia mwenyewe haziivi na usa

kwa ujumla anayeshikilia vizuri petrodollar ni saudi arabia wengine waliobaki wote wameanza kuacha kutumia dollar kwenye oil trade,kama ikitokea saudia nae aka ditch dollar itakua ni hasara kubwa sana kwa USA na faida kubwa sana china
 
Ndio maana tunasema USA uchumi wake unategemea sana ishu ya dollar kutumika kwa wingi duniani,nchi yeyote inayotaka kuacha kutumia dollar lazima ipigwe ila sasa hii kitu nayo ina ukomo wake wa kipigo,this time wameacha kutumia wakubwa wenzake china na russia,je ataweza kwenda kuzipiga hizi nchi?
 
mkuu unaonekana mtupu sana kwa kweli hebu naomba nitajie hata bidhaa tano tu zinatoka china kwenda marekani,hivi unadhani zile tariffs alizoweka trump kwa china kwenye bidhaa zilizokua zinatoka china zilikua ni bidhaa gani au unafikiri zilikua zinaishia kwenye bahari ya Atlantic na kutupwa humo

unaambiwa china ana trade surplus ya zaidi ya dollar billion 300 kwa USA kwa hiyo surplus hapo unafikiri anaingiza ana export maembe USA?

kabla ya kuja hapa jitahidi basi uwe una soma makala mbali mbali za kimataifa hasa za kiuchumi ila kupata walau elimu kidogo

USA is china's largest business partner na china ndio nchi inayo import bidhaa nyingi USA
 
Hizi ni fictions tu na propaganda za IMF ili China waendelee kuwekeza kwao. Yuan hii ambayo sasa hivi inashuka thamani kufuatia effects za zile US trade tariffs eti ndio iwe "Reserve Currency".!! Acheni utani bwana.
unafikiri IMF ni BOT heeeh,imf ifanye propaganda kwa ajili ya mchina ili iweje na wakati ni kibaraka mzuri tu wa marekani sema ni kwamba inafikia kipindi inawabidi kufanya hivyo kutokana na hali halisi ya uchumi wa dunia unavyoenda
 
unafikiri IMF ni BOT heeeh,imf ifanye propaganda kwa ajili ya mchina ili iweje na wakati ni kibaraka mzuri tu wa marekani sema ni kwamba inafikia kipindi inawabidi kufanya hivyo kutokana na hali halisi ya uchumi wa dunia unavyoenda
I beg to differ.
 
Saudi Arabia wameshamnyonga yule Mwandishi na bila shaka Trump analijua hilo ila tamaa ya fedha na potential lucrative business deals zinawafanya wazibe midomo yao
Lakini hawa watu si ndio ujifanya vinara wa kutetea haki za binadamu??

Juzi hapa Uingereza ilifanya usanii kwa kudai former double Agent wa Urusi alilishwa sumu,sasa nini kilifatia baada ya madai hayo potofu Trump alifukuza zaidi ya wanadiplomasia 30 wa Urusi,walishawishi Mataifa mengine ya magharibi kifanya hivyo, Trump hakuishia hapo aliwekea vikwazo Urusi kwa madai kwamba inakihuka haki za binadamu,yaani Trump anajifanya aliguswa sana na tukio hilo LA kuchonga tu kuliko Uingereza ambako jasusi alikuwa anaishi, mpaka leo Dunia haijawahi kuonyeshwa picha ya Jasusi akiwa amelazwa Hospitalini.

Sasa huyu Msaudia aliye kuwa anaishi na kufanya kazi Marekani kauwawa kikatiri kwa kutumia "CHAIN SAW" kakatwa vipande vipande ili kupoteza ushahidi, Trump anajua ukweli huo baada ya kutonywa na Uturuki lakini hapa anajifanya as if Ufalme wa Saudia hawahusiki moja kwa moja na mauuaji hayo, tukio hilo lingetokea kwenye Balozi za Syria saa hizi Trump na washiriki wake wangekuwa wamekwisha ishambulia Syria kwa kutumia ndege na makombola.
 
Ufalme unahusika moja kwa moja kwa mauuaji hayo ya kikatiri, hapa wanataka ku-blackmail Trump ili wasichukuliwe hatua kali. Nina hakika Trump atanywea kazi kukoromea Iran,Syria,Korea Kasikazini,Urusi na China hana ubavu was kuifanya lote uongozi wa Saud Arabia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…