Hii niliona ITV jana kwenye taarifa ya nabari. Kilichonishangaza ni mtangazaji kusema kuwa sasa watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa wataweza kutibiwa nchini kwa kuwa Muhimbili wamepata msaada wa vyombo vyenye thamani ya kama dola laki moja na kitu. Kushangazwa kwangu kunaaanzia kwa kujiuliza kuwa kweli serikali ya Tanzania ilikuwa imeshindwa kupata dola hizo na kununua vyombo hivyo? Ina maana hawa watoto walikuwa wanakufa kwa kukosa vyombo vya upasuaji/matibabu vya dola laki moja? Kwa mawazo yangu, serikali inatumia zaidi ya hizo fedha kwenye mambo mengine yasiyo muhimu. Ni jambo la aibu kuwa kwa sababu tumepokea msaada huo, watoto wetu hawatakufa tena. Pale ambapo tuna uwezo wa kujitegemea tufanye hivyo, ama sivyo tutakuwa tunadharauliwa siku zote!