Saudi Arabia bans 50 baby names

Saudi Arabia bans 50 baby names

Bufa

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Posts
13,651
Reaction score
28,822
Wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia imepiga marufuku majina hamsini ambayo yapo kinyume na tamaduni pamoja na dini ambapo kuanzia sasa, wazazi kutoka falme hiyo hawataruhusiwa tena kuwapa watoto wao.Majina hayo ni kama Linda, Alice, Elaine au Binyamin (jina lenye maana Benjamin) ambapo jina la Benjamin (Binyamin) kwa dini ya kiislamu linaaminika kuwa jina la mtoto wa mtume Jacob, yaani Yacoub kwa dini.
Mengine katika orodha hiyo ambayo hayatoruhusiwa ni kwa sababu yanaaminika kuwa yenye kufuru, yasiyo ya kiarabu na yasio ya kiislamu au yenye kupingana na tamaduni na dini ya falme hiyo.
Sababu nyingine ni ya kigeni ama ya ughaibuni yakiwemo yenye maana ya ufalme au ukubwa, cheo flani kama Sumuw (mtukufu), Malek (mfalme) na Malika (Malkia).

Majina mengine hayapo katika jamii hizi hivyo hakuna sababu zilizotolewa juu yake, hii ni sehemu nyingine ya orodha yenyewe ambapo ni Malaak (angel), Abdul Aati, Abdul Naser, Abdul Musleh, Binyamin (Arabic for Benjamin) Naris, Yara, Sitav.
Mengine ni Loland, Tilaj, Barrah, Abdul Nabi, Abdul Rasool, Sumuw (highness), Al Mamlaka (the kingdom), Malika (queen), Mamlaka (kingdom), Tabarak (blessed), Nardeen, Sandy, Rama (Hindu god), Maline, Elaine, Inar, Maliktina
Maya.

My take: Ni wakati sasa na sisi tukaanza kutumia majina yetu ya asili/kiswahili, unakuta mtu anaitwa John Charles Peter, Esther Edward Boniface, au Rashid Mohamed Abdallah yani hana jina linalooonyesha uasilia wake hata moja katika majina matatu. Ni kweli mtu mweupe katushika akili ila mengine tunaweza zuia mbona watu wa west Africa na South Africa wanatumia majina yao ya asili zaidi. Hivi kuna mzungu/muarabu anaitwa Wema Amani au Masanja Mshana au Bahati Upendo.!?
 
Sawa kabisa kwa uamuzi huo!tutumie majina yetu kama Mgulukwenda,Nzasugwaso,Mfutakamba,Mkunde etc
 
Last edited by a moderator:
shout out to NDIMARA TEGAMBWAGE.,KINGUNGE NGOMBARE MWIRU,Dikembe Mutombo Mpolondo Mukamba Jean-Jacques Wamutombo,Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Za Banga AND OTHERS
 
^^
Inapendeza, kuwa na jina usijue maana au asili yake ni jambo linahitaji ufuatiliaji
^^
 
Tunayo mengi tu mkuu na mazuri; kabanga , amani, upendo, mfutakamba, bahati, masanja, mwaitako et cetera et cetera
kuna kama haya: stumai, havijawa, mazoea, havintishi, mkejina, mkegani, mangosongo, kabanga.....
 
Last edited by a moderator:
Wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia imepiga marufuku majina hamsini ambayo yapo kinyume na tamaduni pamoja na dini ambapo kuanzia sasa, wazazi kutoka falme hiyo hawataruhusiwa tena kuwapa watoto wao.Majina hayo ni kama Linda, Alice, Elaine au Binyamin (jina lenye maana Benjamin) ambapo jina la Benjamin (Binyamin) kwa dini ya kiislamu linaaminika kuwa jina la mtoto wa mtume Jacob, yaani Yacoub kwa dini.
Mengine katika orodha hiyo ambayo hayatoruhusiwa ni kwa sababu yanaaminika kuwa yenye kufuru, yasiyo ya kiarabu na yasio ya kiislamu au yenye kupingana na tamaduni na dini ya falme hiyo.
Sababu nyingine ni ya kigeni ama ya ughaibuni yakiwemo yenye maana ya ufalme au ukubwa, cheo flani kama Sumuw (mtukufu), Malek (mfalme) na Malika (Malkia).

Majina mengine hayapo katika jamii hizi hivyo hakuna sababu zilizotolewa juu yake, hii ni sehemu nyingine ya orodha yenyewe ambapo ni Malaak (angel), Abdul Aati, Abdul Naser, Abdul Musleh, Binyamin (Arabic for Benjamin) Naris, Yara, Sitav.
Mengine ni Loland, Tilaj, Barrah, Abdul Nabi, Abdul Rasool, Sumuw (highness), Al Mamlaka (the kingdom), Malika (queen), Mamlaka (kingdom), Tabarak (blessed), Nardeen, Sandy, Rama (Hindu god), Maline, Elaine, Inar, Maliktina
Maya.

My take: Ni wakati sasa na sisi tukaanza kutumia majina yetu ya asili/kiswahili, unakuta mtu anaitwa John Charles Peter, Esther Edward Boniface, au Rashid Mohamed Abdallah yani hana jina linalooonyesha uasilia wake hata moja katika majina matatu. Ni kweli mtu mweupe katushika akili ila mengine tunaweza zuia mbona watu wa west Africa na South Africa wanatumia majina yao ya asili zaidi. Hivi kuna mzungu/muarabu anaitwa Wema Amani au Masanja Mshana au Bahati Upendo.!?

MKUU MAMBO HAYA YANATAKA KWANZA KUJITAMBUA.
MFANO: born Joseph-Desiré Mobutu; NA ALIPOJITAMBUWA AKAWA Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Za Banga
 
kuna kama haya: stumai, havijawa, mazoea, havintishi, mkejina, mkegani, mangosongo, kabanga.....

Itakua kheri kubwa tukianza kutumia zaidi hayo, tumepoteza asili yetu kabisa tofauti na watu wa nchi nyingine nyingi ambao wanatumia zaidi majina yao

Sahizi Tz watu wanashindana kuwapa watoto wao majina wanayosikia kwenye tamthilia na kwenye mipira unakuta mtoto wa kiume anaitwa Angelo sijui Cristiano au Beyonce kana kwamba kuna mtu mweupe anatumia majina ya kiswahili
 
MKUU MAMBO HAYA YANATAKA KWANZA KUJITAMBUA.
MFANO: born Joseph-Desiré Mobutu; NA ALIPOJITAMBUWA AKAWA Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Za Banga

Kweli kabisa mkuu, mods wameondoa kitufye cha "like" nimeshindwa kugonga
 
Ni kweli inahitaji kujitambua kwanza wakuu,,,james ngugi to ngugi wa thiong'o
 
majina kama, mwita, chacha, marwa, bhoke, ghati, maranya, nk hayatokaa yakatike kule kanda maalum...
 
Na huo ndio uzalendo sio kuitana majina kisa umesikia kwenye tamthilia/movies na mipira
 
majina kama, mwita, chacha, marwa, bhoke, ghati, maranya, nk hayatokaa yakatike kule kanda maalum...
ongeza Matiko, Magesa, Malicha Mutatiro, Mwihechi, Rhobi, Mugesi, Chingw'a, Mugendi, Mwisendi, Megera, Werema, Matinde, Warioba, Ryoba need I say more?
 
Back
Top Bottom