Saud Arabia na Qatar Zimemruhusu Iran Apige Base Za USA Kwenye Ardhi zao

Adiosamigo

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
10,596
Reaction score
13,980
Kwa Sasa ni kichaa pekee atakayekubaliana na propaganda za Marekani

Miaka ya nyuma alikuwa anajificha katika kivuli Cha kupambana na ugaidi na mijitu vilaza ilikuwa inakubali
 
Jifurahishe angalau upate usingizi
 
hiyo title haileti mantiki
 
Saudi inalindwa na US,akiruhusu hiko kitu. Basi Saudi wakae tayari kwa mashambulizi toka Yemeni.
 
Kamwe hilo haliwezekani wote ni vibaraka wa marekeni
 
Unajitekenya halafu unacheka mwenyewe.
 
Kwa Sasa ni kichaa pekee atakayekubaliana na propaganda za Marekani

Miaka ya nyuma alikuwa anajificha katika kivuli Cha kupambana na ugaidi na mijitu vilaza ilikuwa inakubali
Marekani sahizi hawapigi tu propaganda
Wakiona umeshindikana wanafanya la maduro
 
Kitakachoifanya marekani isiingie vita na nchi yoyote duniani ni 1. Kuharibu mauzo ya mafuta duniani (kitu ambacho Iran inaweza kwa sababu njia ya bahari inapita kwake)
2. Kuwaweka washirika wake wa ulinzi na uzalishaji mafuta kwenye hali ya vita, kama Saudi Arabia, Qatar, UAE, Israeli etc kitu kitakachofanya uchumi wa dunia kushuka na marekani itapoteza zaidi.
3. Kusababisha wamarekani including wanajeshi wake ambao wako nje ya Marekani kuwa kwenye hali ya hatari ya kushambuliwa.

Kuna vigezo vingi ila hivyo vigezo vyote vikitokea kwa mara moja kwenye vita, bunge la Marekani litaweka pingamizi kwenye vita isiendelee.

Hii haimaanishi kwamba US inashindwa vita, Ila US wanaangalia zaidi maslahi ya biashara kuliko kushinda vita na kupoteza biashara...

Kitu kingine US anapata kigugumiz sana kushambulia Iran japo wana uadui kwa sababu Iran chini ya Utawala wa ki Shia ndio uliosaidia ISIS (sunni) wasijipenyeze mashariki ya kati... Ayatollahs akitoka melinza mizigo hazitakua na usalama na Marekani itapoteza kikubwa sana.

Qatar , Saudi Arabia na UAE ni mahasimu wakubwa wa Iran kuliko hata Israeli kwa sababu ya itikadi tofauti za kidini(shia vs sunni), kiushawishi Saudi vs Iran pamoja na kijeshi kwa sababu vikindi vyote vinavyopewa silaha na iran nje ya Hamas ni adui wa nchi nyingi za kiarabu. ni furaha kwa hizi nchi marekani ikishambulia Iran, ila wao hawataki kuingizwa kwenye vita.


Kama zimekubali Iran kushambulia kambi za Marekani maana yake ni 1. Hizi nchi zimejitoa uhusika wake na US kwenye vita , so kama Iran itashambulia kambi peke yake basi wao nao hawatakibu mashambulizi.

Hii kwa upande mwingine nintaarifa nzuri kwa Marekani, anajua hatapoteza rafiki wa kiarabu hata akishambulia Iran
 
Kwa Sasa ni kichaa pekee atakayekubaliana na propaganda za Marekani

Miaka ya nyuma alikuwa anajificha katika kivuli Cha kupambana na ugaidi na mijitu vilaza ilikuwa inakubali
Wakati kumbe hayo makundi ya ugaidi Anaya recruiting yeye
 
Hii ni Propaganda ๐Ÿšฎ
Saudi Arabia ni chawa wa USA hivyo hawezi kubali base za USA kushambuliwa.
Yaani ni chawa Tena mkuu , hawezi kukubali Hilo Maana hatoweza kuwa salama ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ