Wauze tu ilimradi wasiwe na madhara maana wachina akili zao hazina msimamo kabisaa
Samaki hao sina hakika sana kama ni salama kwa afya zetu,hao vibua kuna mchina niko nae ofisin alishanikataza kuwatumia,nilipotaka kuhoji sana aligoma na jibu likabaki hilohilo 'si SAWA!!!
Siku tatu zilizopita nilienda soko la samaki la Kivukoni,Dar es salaam kwa bahati nzuri nilikuwa na expert wa masuala ya samaki.Kuna samaki wengi alinikataza nisiwanunue akaniambia hao wanatoka China na wamewekewa madawa ya kuwazuia wasiharibike kwa kweli nilistushwa sana na taarifa ile ikanibidi niende eneo ambalo wavuvi huwa wanashusha samaki waliotoka kuvuliwa muda huo huo ndo nikawanunua.
umaskini ni ki2 kikibaya sana. Nchi imegeuzwa jalala na watu wachache wachoyo na walafi. Badala ya kusimamia ipasavyo uvuvi nchini wanaudidimiza. Nasikia pia kuna kuku wengi wa nyama kutoka Brazil.Kuna sato na sangara hai na waliogandishwa wanauzwa mwananyamala na Wachina. Bei yake ni poa kuliko Sato na Sangara tika Mwanza. Hao samaki ni zao la vifaranga waliochukuliwa Lake victoria kijanja na kuoteshwa kwenye bwawa kubwa huko Gwanzhu. Sera za Serikali yetu zinatoa fursa kwa wachina/wageni na kudidimiza wavuvi na viwanda vya ndani. Jadili kwa hoja. Hatua thabiti zichukuliwe haswa kuhakikisha Wachina hawa wamefuata taratibu na wanalipa kodi kuwaingiza tz.
Sioni tatizo kwa wachina kuuza sato na sangara kwa bei nafuu,maana inamsaidia mtanzania wa kawaida kupata hao samaki kwa beo rahisi,sio wote wana afford kununua sato kilo kwa 10,000 na sangara kwa 8,000 kama wanauza chini ya hapo sio mbaya.