Sataranji ya Sisiemu na Slaa 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sataranji ya Sisiemu na Slaa 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Companero, Jul 28, 2010.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Jul 28, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mada hii inahusu uhusiano kati ya Sataranji na Siasa. Sataranji ni mchezo ambao hutumia fikra nyingi na mipango mingi tarajali kumshinda mpinzani. Katika mchezo huu, ambao vinara wake walikuwa ni Mafia a Sicily, Italia na Warusi kama Gary Kasparov, mtu husoma mchezo wa mpinzani na kutambua njia anuwai ambazo mpinzani huyo aweza kusogeza kete. Lakini mtu haishii kuzisoma tu hizo njia mbalimbali, bali pia hupanga njia anuwai za namna ya kucheza kwa kutegemea na jinsi mpinzani atakavyosogeza kete yake. Hivyo hivyo ndivyo ilivyo katika medani ya siasa zilizokubuhu. Kinara katika medani hii katika siku za hivi karibuni ni Rais Barack Hussein Obama ambaye alitumia mbinu ya Kisataranji kumgalagalaza Hillary Clinton katika uchaguzi wa awali wa Mgombea Urais kwa tiketi cha Chama cha Democrats. Hata Rais wa sasa nchini aliucheza kimahiri mchezo huo 1995-2005 ndio maana magwiji wa siasa walishindwa tena kumchomoa kama ilivyotokea 1995.

  Hapa nchini itakuwa vigumu sana kudai kuwa mbinu hii haitumiki ipasavyo hasa ukizingatia kuwa kuna mitandao lukuki ndani ya chama tawala. Ndio maana ni kujidanganya kudhani Sisiemu imeshtukizwa na kupitishwa kwa Dakta Slaa kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema. Hivyo, cha kujiuliza ni, je, chama tawala kilipanga nini mara baada ya kusoma dalili za nyakati na kuona uwezekano wa mtu huyu mwenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya Sisiemu kupitishwa. Ikumbukwe huyu alikuwa ni Mwanasisiemu ambaye alikigalagaza chama chake hicho cha zamani baada ya kugoma kumpitisha kugombea jimbo la Karatu japo alikuwa anakubalika zaidi kwa maoni ya wanasisiemu wa jimbo hilo.

  Sataranji ina siri nzito - Slaa akiicheza vizuri basi anaweza kuisambaratisha 'Ngome ya Sicily' 2010!
   
 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe mkuu... lakini yabidi tumsadie Mh. Slaa yakhe.... tuseme.... Wananchi wapenda haki tukiicheza vizuri basi tunaweza kuisambaratisha 'Ngome ya Sicily' 2010!
   
 3. Companero

  Companero Platinum Member

  #3
  Jul 28, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu kusaidia kwa kupiga kampeni na kura hakutoshi. Inabidi watu wacheze sataranji hasa. Kumbuka sataranji ina njia mbali mbali - kuna Queen's Gambit, Sicilian Defense na kadhalika. Hapo inapaswa kuchambua kila hatua ambaye mpinzani wako atachukua ama anaweza kuchukua. Kwa mfano, katika jimbo la Ubungo inabidi mtu apange hatua zaidi ya saba mbele kuhusu nini cha kufanya kama:

  (1) Sisiemu itampitisha Shamsa

  na kumpanga hatua zingine (pengine tofauti) zaidi ya 7 kama:

  (2) Sisiemu itampitisha Nape

  Yote hayo si kuwa yatakuwa na matokeo tofauti tu kwa ugombea ubunge wa Mnyika bali pia ugombea uraisi wa Slaa.

  Fikiri kabla hujagusa/hujasogeza kete!
   
 4. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2010
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  akipita shamsa ni ahueni kwa mnyika
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Jul 28, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ukicheza sataranji namna hiyo kamwe huwezi kumshindi gwiji - cheza hivi:

  Kama Sisiemu itampitisha Shamsa itakuwa ahueni kwa Mnyika kwa namna hii (1), (2),..., (n)

  Ili Mnyika ashinde itabidi aitumia ahueni (1),(2),..., (n) hivi (1a),(2a),....,(na)

  Na kama Mnyika atatatumia ahueni hizo namna hii (1a), (2a)...,(na) basi Shamsa aweza kujibu mapigo hivi (1b), (2b),...,(nb)

  Hivyo basi inabidi Mnyika afanye hivi, au hivi, au vile ile ashinde.

  Mchezo Kwisha!
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mimi naona kama vile ili mchezo uishe kwa ushindi ni lazima kuangalia wapi wanaiba kura, Embu niambie umewahi kuona jamaa wanavyokuwa ndani ya chumba cha kula wanalala hapohapo, zikikusanywa wanapanda kwenye gari la mabox na wakati huo wa upinzani wameachwa.

  Sataranji ya muhimu ni kuangalia wakati wa kupiga kura, wale wasimamizi waangaliwe, kuchambua na kuhesabu, vinginevyo utaniambia come November.
   
 7. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Santaranji nyingine,
  wafanyakazi mara nyingi ndo huwa wanaenda kusimamia kura, hasa walimu n.k, JK kasem hataki kura zenu, msiishie hapo kumnyima kura zenu, hakikisheni hamkubali kutumika kuiba kura za wengine! Abaki na hizo hizo za hao watakao mpigia! Tatizo ni pale wasimamizi mnapo kubali kutishiwa nyau mkakubali mabox yakabadilishwa, Mbona Tarime waliukataa upuuzi huo? kila mtu asimame kidet kuukataa wizi wa kura kwa nafasi yake, hapo Slaa ata win tu!
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe kuwa Chess hapa kwa upande wa wadanganyika ni kusimamia kwa makini tangu watu wanapoanza kupiga kura mpaka pale masanduku yanapofunguliwa na kura kuhesabiwa. Masanduku ya kura yasitoke nje ya kituo cha kupigia kura na kura zihesabiwe hapo hapo kituoni mara tu baada ya vituo kufungwa; karabai ziwe standby kila kituo just in case watazima umeme kwani ccm wanambinu za limafia pale wanaposhindwa. Inabidi pia kuwathibiti vijana wa CCm wasifanye fujo na kuharibu uchaguzi pale wanapoelekea kushindwa kama walivyofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa pale KAWE UKWAMANI!! wANANCHI WASITEGEE SANA VYOMBO VYA DOLA KUPATA HAKI YAO YA KUCHAGUA MTU WAMPENDAE; kwani vyombo hivyo ni watetezi wa chama tawala!!
   
Loading...