Sassou Ngueso Na Ushindi Wa Ki-CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sassou Ngueso Na Ushindi Wa Ki-CCM

Discussion in 'International Forum' started by Junius, Jul 17, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  [​IMG][​IMG]
  Rais Sassou Ngueso.
  Rais Denis Sassou-Nguesso ataendelea kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mingine saba baada ya kunyakua ushindi mkubwa katika uchaguzi ambao ulisusiwa na vyama vya upinzani ambavyo viliishutumu serikali kwa kujilimbikizia kura.
  Tume ya uchaguzi ilisema Bwana Sassou-Nguesso alikuwa amepata zaidi ya asilimia 78 ya kura na mpinzani wake wa karibu akiwa na chini ya asilimia 10.
  Wafuasi wa upinzani wapatao elfu mbili walijaribu kuandamana kwenye mitaa ya mji mkuu Brazzavile lakini wakasambaratishwa na polisi waliowatimua na gesi za kutoa machozi.
  Polisi walimwandama mwandishi wa BBC mjini Brazzavile, Thomas Fessy na mwenzake wa kituo cha televisheni cha Ufaransa na kuwanyang’anya vifaa vyao vya kazi.
  Fessy alisema “maandamano hayo yalikuwa salama lakini polisi waliwashambulia na kuwatawanya kwa gesi za kutoa machozi.”
  Licha ya malalamiko ya upinzani, kiongozi wa kundi la waangalizi wa Umoja wa Afrika, Dieudonne Kumbo Yaya aliiambia BBC kwamba hawakushuhudia kisa chochote cha udanganya katika upigaji kura uliomalizika Jumapili iliyopita.

  SOURCE: BBC(SWAHILI SERVICE)
   
 2. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #2
  Jul 17, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Huyu na kina Omari Bongo ni walewale tu. Mijitu mingine wanaona kama
  ni lazima kutawala. This keeps Africa stagnant for the longest.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Huyu mwangalizi wa uchaguzi kutoka AU sijuwi hata anasema nini. Ingelikuwa vyema hawa waangalizi wa "maigizo" yetu haya tunayoyaita uchaguzi, wakaja mapema tokea zoezi linaanza katika hatua za matayarisho i.e,, kuanzia uandikishwaji wa wapiga kura mpaka uchaguzi wenyewe. Wasingekuwa wanahalalisha uhuni kama huu wa Sassou Ngueso.
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na ukitazama tokea ampindue Pascal Lisuba, hakuna la maana moja alilolifanya matumizi makubwa ya fedha za wananchi kwenye jeshi lake kujiimarisha tu bas, wananchi masikini wa kutupwa. Huyu sawawa na yule mwenzake kule Uganda ambaye ana miadi na Mungu atamfikisha mpaka miaka 75.
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kama researchers wa bongo. Watu wana tumwa kufanya kazi hawafanyi mwishoni wanaandika tu wanacho jisikia. Usikute huyo "mwangalizi" hata hakufanya uangalizi wowote.

  It is sad that Africa mpaka leo tuna hitaji waangalizi tena kutoka nje kuja kushuhudia chaguzi zetu
  .
   
Loading...