Sasa Zitto ana nguvu kama Kingkong-CCM wanatetemeka wakimuona au kumsikia

Kaldinali

JF-Expert Member
May 25, 2012
263
144
It is official kuwa Mr. Zitto Kabwe sasa ana nguvu sana katika duru za siasa nchini Tanzania (i am talking about a different kind of power). Taratibu naanza kuamini kuwa huyu bwana amekuwa - au soon atakuwa - taasisi (institution). Kwanini?

Kumbe huyu bwana alipotangaza kwenda Marekani Chama Cha Mapinduzi ambacho ni taasisi( Chama chote Tanzania bara na visiwani) kilishutka, kutetemeka na kuamua kufuatilia kila nyendo ya safari yake. Not only that wamefuatilia kila neno alilosema (labda na kila mtu aliyekutana nae na kama mama Maajar asingekuwa mwana mtandao angepata matatizo kwakukutana nae kama yaliyomtokea Balozi Nyaki alipompokea Mrema back in the 90's).

Hawakuhishia hapo taasisi hiyo ya Chama Cha Mapinduzi imekaa na kuyachambua maneno aliyoongea Zitto mstari kwa mstari na kuona maneno aliyoongea ni mazito na yanaki-demage chama na hivyo wakaona umuhimu wa kumjibu mstari kwa mstari. Na katika ripoti hiyo ya chama cha mapinduzi hawakuandika jina la Kiongozi wa CCM aliyetoa ripoti ya kumjibu Zitto kwakuwa (1) Walitaka ionekane ni taasisi nzima ya CCM iliyomjibu mtu mmoja Zitto Kabwe (2) Labda wengi wa viongozi wa CCM wanaogopa kuwa na personal beef na huyu KingKong Zitto Kabwe.

This guy Zitto is as strong as Kingkong Now!
 
Huyu jamaa sio tuu Ana nguvu Kama king kong anamzidi king kong na hii imekuwa ni kwa CDM nzima kauli zao zinasubiriwa zitumike kwenye propaganda lakini CDM hawatumii masaburi kufikiri Kama ccm
 
Zitto ni Mbinafsi kweli kama Nape... na tatizo ni Ndumila kuwili anasikiliza ya CCM na kuyafanya akiwa CHADEMA

CCM hamuogopi ZITTO hata kidogo; Nipeni Sababu ya CCM kumuogopa ZITTO
 
Zitto ni Mbinafsi kweli kama Nape... na tatizo ni Ndumila kuwili anasikiliza ya CCM na kuyafanya akiwa CHADEMA

CCM hamuogopi ZITTO hata kidogo; Nipeni Sababu ya CCM kumuogopa ZITTO

wewe mwenyewe unamuogopa tupe sababu ya wewe kumuogopa
 
I have never doubted this guy! nimefanya naye siasa tangu enzi hizo, najua brain yake, caliber yake na mitazamo yake, nipenda tena misimamo yake

Lakini kwa siasa za Tanzania, watu kama yeye ni ngumu sana kudumu, kwani maadui zake wako kila kona, within, outside, kila mahali.

almost all potential and good leaders ambao leo wamerudi nyuma waliangushwa na watanzania wenyewe!!! mi-strust, kusingizia,uzushi, na majungu mengi.......naamini kwa upepo uliopita CCM ambao chadema waliuanzisha kupitia huyu zitto, lazima zitto kama asingekuwa msafi angeangushwa maramoja!! Leo hii akina Maige hawawezi kumsema zitto anamsema Nappe!! unaweza kumkuta mtanzania mwenye akili timamu anasema kwa uchungu kuwa zitto au fulani ni fisadi wakati hana hata chembe ya uthibitisho...kisa...kaaminishwa!!

Yes is good but will he survive?? na kama sio, je wangapi kama zitto ambao watatokea na wataangushwa chini kwa sababu ya wivu wetu, vision zetu na majungu yetu na tabia zetu???
 
Hoja hapa sio zito kuwa na nguvu bali ni chadema ndiyo inafanya kazi hiyo. Hata huko marekani ameenda kwa ajili ya cdm na sio yeye kama zito wananchi waache kupima maneno kana kwamba yeye ndo yeye kama vip ahame cdm aone kama kuna mtu atamfuata. Nguvu aliyoipata inatokana na chadema. Na wananchi wanapenda umoja kwa iyo kusema zito ana nguvu sana ni kujidanganya huku kukiwa cdm ndio inayompa nguvu
 
Zitto ni Mbinafsi kweli kama Nape... na tatizo ni Ndumila kuwili anasikiliza ya CCM na kuyafanya akiwa CHADEMA

CCM hamuogopi ZITTO hata kidogo; Nipeni Sababu ya CCM kumuogopa ZITTO
Akiamua kuivunja serikali anaivunja.
 
Zitto ni Mbinafsi kweli kama Nape... na tatizo ni Ndumila kuwili anasikiliza ya CCM na kuyafanya akiwa CHADEMA

CCM hamuogopi ZITTO hata kidogo; Nipeni Sababu ya CCM kumuogopa ZITTO
Allah! Kumbe nape naye ni mbinafsi!
 
Kaldinali, umeingia JF ili uweke hii post? Pamoja na kuwa ni kweli namkubali Zitto, ila kampeni yako siioni kuwa ina mshiko. Ndo zile za urais wa 2015 nini?
 
Jamani kumjadili kiongozi mmoja mmoja sio tija wala hoja mimi ninachoona hapa ni wananchi sasa wameamka na wanataka mshikamano na umoja ambao unaweza kuyakomboa maisha yao hapa tunavyoongea hivi kule vijijini kuna watu wamemka na njaa hawajala tangu jana ila madini, rasilimali zetu zote zinapewa wajanja wachache kwenye hii nchi. Mimi wakati ninapokwenda nyumbani kijijini likizo ohh my God utafikiri hawa watu hawaishi wanamatatizo yasipimika. Unawakuta vikongwe wameshindwa hata kuamka ndani kisa njaa. Jamani tuamke tuachane na hiki chama cha Mafisadi tukendelea kukibali kushika dola tutapoteza ndugu zetu wengi wasiokuwa na uwezo na MUNGU ATATUULIZA SIKU ZETU ZA MWISHO.
 
zitto ni mbunge makini na chama alichomo ni makini,nitajie mbunge wa cdm asiyekuwa makini ukimuondoa shibuda na selasini.
 
Nafikiri hapa anajadiliwa Zitto kama Zitto kutokana na majibu ya CCM yaliyokuwa yameelekezwa moja kwa moja kwa Zitto juu ya hotuba aliyoitoa uko Marekani.
Kosa ambalo nawaona CCM wanalifanya na inawezekana kabisa hawalijui ni kwamba wanazidi kumpandisha chati wakifikiri wanamuaribia. Kitendo cha wao kutolea majibu kila kauli anayoisema ni dhahiri kwamba ni tishio, na ingekuwa kuna mambo anayoyakiuka amaa hakika wangeshamchukulia hatua.
Alisema kuhusu hazina ya BOT kukauka CCM wakamjibu, sasa tena wamemjibu hotuba aliyoitoa kule marekani. Hata kwenye mchakato wa kudai uwajibikaji (Sahihi 70) CCM walihaha sana kina January Makamba... lakini mwisho wa siku ukweli unaonekana.
In short, Zitto wa CHADEMA yuko ahead of CCM
 
Hahahaaaaa, I like the guy...kuna kipindi sikumwelewa, but now nampata. Ila aache kulewa sifa.
 
Back
Top Bottom