Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Swali la kujiuliza; nani anaemuogopa Tundu Lissu hata kufikia hatua ya kujaribu kumuua? Kumuua mchana wa Jua kali. Serikali? Magenge ya wahalifu? Wanasiasa wenzake? Lakini Tundu Lissu ametupa majibu ya kila swali ambalo tunaendelea kujiuliza;
Matukio kama haya ya 'kuogofya' na 'kusikitisha' yanapotokea watu huunganisha matukio kadhaa kupata kitu kamili. Tundu Lissu ni 'mwiba mkali' kwa serikali hii. Watu wanaokosolewa nae; hawana uthubutu wa kuvumilia ukosoaji wake.
Kabla ya kupigwa risasi, amekamatwa mara kadhaa na kulazwa mahabusu, amesafirishwa usiku kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kujibu tuhuma za uchochezi. Ameshtakiwa kwa makosa mbalimbali na hawajawahi kumtia hatiani. Tunaunganisha 'dots'
Watu hawa wanaendelea kutuaminisha kwamba hili lilikuwa jaribio hafifu la mauaji kutoka kwa "watu wasiojulikana" dhidi ya Tundu Lissu na Tunaendelea kumshukuru Mungu Tundu Lissu amepona na anaendelea kuimarika kila uchwao.
Shambulio dhidi ya Tundu Lissu lilikuwa jaribio la kuondoa uhai wake. Tazama risasi zilizotumika. Silaha. Sio mchezo wa kuigiza. Tundu Lissu kaumizwa. Mumgu wake ni mwema. Kamfanya kuwa "muujiza unaotembea" na hili limewakera wengi wenye kuhusika.
Unasikia kauli zao, maneno yao yanawahukumu. Ukakasi ni mkubwa. Ni watu wamejawa na ghilba, husuda na chuki dhidi ya Tundu Lissu. Kauli zao hata shetani anaogopa; ni zaidi ya 'ushetani' wenyewe.
Unamsikiliza katibu mkuu wao, unarejea kumsikiliza katibu wao wa itikadi na uenezi kisha unasikiliza wafuasi wao wakisema kwa kupokezana sauti za 'kupayuka' na zenye kujazwa na chuki.
Katibu mkuu wao anasema mwenyekiti wao ndie tiba ya ugonjwa unaitwa 'Tundu Lissu' na kusema Lissu "anajidekeza" na wakati huo "makada" wenzake wanachukizwa nae na hata kusema mbele ya masuala ya 'futiboli' kuhusu habari za mtu huyu.
Katibu wao wa itikadi na uenezi bwana Chakubanga ambaye ni 'spesheli' katika masuala ya "propaganda" anatueleza kwamba Tundu Lissu sio kiumbe wa kwanza kupigwa risasi nchi hii; wapo wengi wa CCM huko Kibiti. Hivyo Lissu asitupigie kelele. Loh!
Kuna kada mwingine kutoka huko CCM nae anatupa simulizi kwamba bwana Tundu Lissu hajashambuliwa kwa risasi za moto isipokuwa kwa vitu vinaitwa "bl(r)anco" ndio maana yupo hai. Hawa watu wamepagawa vibaya.
Waziri nae anayo yake kuhusu hili, wakati polisi walitueleza awali kuhusu uwepo wa kamera za CCTV eneo aliloshambuliwa Tundu Lissu, mwaka mmoja baadae waziri anasema eneo hilo hapajawahi kuwepo 'security cameras' .. inashangaza!
Mkuu wa wilaya huko Kigamboni anasema Askari wa nchi hii hawajawahi kukosa shabaha, hivyo hawawezi kutumia risasi zaidi ya 40 na wasimpate Tundu Lissu; inatia simanzi; nani anawatuhumu askari wetu katika shambulio hilo? Wameanza kujishtukia na 'kuropoka' hapa al'badr inafanya kazi yake.
Wanaonekana ni watu walioumizwa na jaribio la kumuua Tundu Lissu 'kutofanikiwa' na wamechukizwa zaidi baada ya kuona kiumbe huyu amepona risasi 16 na amefanikiwa kutoka kwenye 'operesheni' 23 sasa.. wanashangaa huu muujiza.
Hawa watu walitamaani maiti ya Tundu Lissu isiagwe DSM au Dodoma. Ipelekwe kuzikwa mara moja Ikungi, pahali alipozaliwa 'mtanzania' huyu. Tundu Lissu anatueleza kwamba watu hawa hawakupenda kuona anapewa heshima ya 'kibunge' hata kidogo.
Ukiwatazama, unarejea maswali ya awali, kwanini watu hawa walikuwa wanashinikiza apelekwe Muhimbili kupata matibabu na sio nje ya nchi? Kwanini watu hawa waliumizwa na Tundu Lissu kupelekwa Nairobi, Kenya kupata matibabu?
Wapo wengine wenye kusema akirejea auwawe kwa kupigwa risasi. Wanaandika hayo mtandaoni. Tena kwa kurudia-rudia; Polisi wanaona. Wamefumba macho. Hawachukui hatua za kisheria dhidi yao. Hii ni ishara kwamba mtu huyu anawatikisa ipasavyo.
Wameshindwa kujibu hoja zake, Wakampiga risasi nyingi. Wameshindwa kujibu hoja zake, sasa wanapanga kumuua kabisa kama akirejea Tanzania. Tundu Lissu amewashinda mahakamani; amewashinda jukwaani sasa wanataka uhai wake.
Sasa wamepanga kumfunga magereza. Wanaamini ndio njia sahihi ya kumtuliza na kumfanya atulie. hawana hoja jadilifu. Wanatumia 'magereza' kukandamiza yoyote wanaemchukia. Wamekwenda mahakamani kuomba mahakama imfutie dhamana yake; awekwe mahabusu kama Mbowe na Esther Matiko.
Wamejaribu na wamefanikiwa. Walimpeleka Lema mahabusu. Wamempeleka Mbowe/Matiko mahabusu sawa na mtu aliyefungwa miezi mitano. Sasa wanataka mahakama impeleke Tundu Lissu huko, akiwa na matundu 16 ya risasi na operesheni 23 katika mwili wake.
Mawakili wa serikali kupeleka ombi la mahakama kumfutia dhamana Tundu Lissu, 'kisheria' wanaweza kuwa sahihi, lakini uungwana na UTU ulipaswa kuwa busara yao. Hapa ndio naamini ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali inabeba taswira nzima ya serikali katika hili.
Unaweza vipi kuomba mahakama imfutie dhamana mtu ambaye anaendelea kupata matibabu nje ya nchi? Majeraha ya risasi na operesheni nyingi mwilini? Tena wadhamini wake wakiendelea kufika mahakamani; pia mawakili wake. UTU ndani yao haupo? Wametumwa na serikali, hawajajituma!
Mwili wa Tundu Lissu umechanwa'chanwa kwa risasi lakini mawakili wa serikali wanataka akauguze majeraha hayo magereza na sio hospitali. Wanachukizwa wakiona anaendelea kupata nafuu. Walitamani kuona anapelekwa Ikungi akiwa marehemu.
Tundu Lissu huyu ambaye kapigwa risasi 16 mwilini kwake; katibu mkuu wa CCM anasema Tundu Lissu 'anajidekeza' na hajawahi kushika jembe, looh! Hivi kujidekeza mbele ya bunduki ya 'kivita' inawezekana vipi? Bashiru rudisha akili ulipoazima, chutama!!
Wakati huo spika wa bunge nae anasema anaufunga mshahara wa Tundu Lissu. Spika wa bunge ambalo halijawahi kujadili taarifa ya hali ya afya ya Tundu Lissu anamtaka Lissu arejee jimboni bila ruhusa ya madaktari.
Kauli zao zinatuonesha matendo yao. Hizi hasira zao ni sehemu tu ya maumivu yao kwa kumuona Tundu Lissu amesimama wima. Wamejawa na hofu katika vifua vyao. Wameshika dola lakini wanakerwa na 'msingidani' huyu. Hofu ni kubwa juu yao.
Kauli hizi za viongozi na wanachama wa CCM zikiendelea kuachwa kwenye matukio kama haya, Nchi yetu itaendelea kuwa sehemu yenye kuogopesha; sifikirii kama tunapaswa kuiweka nchi yetu huko, haiwezekani.
Tuendelee kuombea akili za hawa watu; wamevurugwa; wanateseka; wanapita wakati mgumu kuliko hata Tundu Lissu aliyepo hospitali katika matibabu.
MMM, Martin Maranja Masese