Sasa sote tunahara

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,284
1467727018182.jpg


Sasa sote tunahara, kufuli ziko chooni,
Kisa ni bwana Uchwara, dikteta aso soni,
Tukifanya masihara, gonjwa hili hatuponi,
Maharage yana nini, mbona sote tunahara?

Jana tena kwa papara, tuliomba siamini,
Tupate aliye bora, mfano Idd Amini,
Tumejibiwa majura, tumepata yu' kazini,
Maharage yana nini, mbona sote tunahara?

Awazalo mtu jura, hulipata niamini,
Kumethibiti kuchura, hufanyika ulimini,
Sasa tuwate kufura, wazo letu limewini,
Maharage yana nini, mbona sote tunahara?

Tusifanye kwa harara, kudai demo' nchini,
Tusijitie hasira, yataka tuwe makini,
Tuongozwe na subira, uzalendo na yakini,
Maharage yana nini, mbona sote tunahara?

Kazi yangu sio chura, BASATA toka shakani,
Imemulika madhara, na njia ya Kaanani,
Tukifa'ta ni busara, kama twataka amani,
Maharage yana nini, mbona sote tunahara?

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatspp 0622845394
 
Itabidi tujisaidie kwenye rambo tuu mpaka funguo wa choo upatikane
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom