Sasa polisi wanaliogopa neno 'Peoples Power'

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
"Tumelazimika kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi kwa sababu walikuwa wakitoka mahakamani kwa mfumo wa maandamano huku wakisema, "Peoples Power."

"Kama wasingetumia mfumo huo kama walivyoingia sisi tusingepiga mabomu, lakini hatukutumia risasi za moto huo ni uvumi tu,"alisisitiza Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Akili Mpwapwa.

My take: Ina maana kama wangetoka mmoja mmoja kama walivyoingia si ingechukua siku nzima kutoka, basi makanisani na misikitini tuwe tunatoka mmoja mmoja kuepuka maandamano, busara ni kitu muhimu sana.
 
kinachijidhihirisha ni kuwa Polisi wanaogopa nguvu ya CHADEMA but kwenye mazishi ya waliokufa walithibitisha wanaweza kusanyika na kufanya yao kwa amani kidogo
 
Polisi wetu hawana uwezo walau wa kujenga hoja za kutetea udahalimu wao.Ukiwa chadema hata ukitembea peke yako wanaweza kukuambia unaandama kama mwezi na wakakupiga mabomu.
 




Defiant Gaddafi vows to fight on

In televised speech, Libyan leader blames youths inspired by regional events for uprising and vows to die a 'martyr'. ( 23-Feb-2011 )

SWALI HUMU: UTAMADUNI WA KURITHISHA WATOTO WA WAKUBWA
UKUBWA TANZANIA CHANZO CHAKE NI WAPI???


Nani anayejua hasa darasa la huyu King of Kings?

Kwa mtaji wa hutuba aliyoitao hivi majuzi ni mara mia angjinyamazia tu hivyo tungeendelea kumfikiria mstaarabu fulani hivi. Kwa kujiunga kwake jeshini akiwa na umri wa miaka 12 (child soldier) wala hatuhitaji kuuliza kama 'ALIONEWA SANA YEYE', 'AKADHALILISHWA SANA GADDAFI' hivyo kuja kupata kamwanya wa kuongoza nchi kwa mtindo wake mwenyewe hivi sasa anarudishia ngumi kwa jamii nzima ya Libya.

Tujifunze kitu basi na sisi hapa kwamba wale tuliowahi kuwaondoa kwenye nyadhifa fulani hapa nyumbani kufuatia kashfa iliyogoma kwisha katikati yetu hadi leo, nao wakija tu kupata urais wa nchi hii mtindo wao wenyewe na tusifikirie matendo yao kutofautiana sana na ya huyu nduli hapa.

Hakika shule iliomuingia mtu na kutulia ndani mwake ni muhimu zaidi tena sana kuliko shule ya kupitia hata kama madarasa yako ni mengi kimahesabu vidoleni.

Kanali Gaddafi ajikaanga kwa ulimi wake mwenyewe. Na watoto wake , masikini ya Mungu, ndio kabisaa wanaamini taifa zima la Libya ni kama shamba binafsi la ukoo kwa baba yao.

Nikitazama ya Ben Ali wa Tunisia, nikamgeukia Hosni Mubarak wa Misri na kumtaza mzee huyu ambaye kimawazo ni 'chipukizi' tu, na mwenendo mzima wa ushiriki wa familia zao katika mambo ya utawala wa nchi, Wa-Tanzania wenzangu NAPATA MAJIBU KUBWA SANA HAPA HAPA NYUMBANI kwamba ni kwa nini kati ya marais wetu wote wanne ni wawili tu kati yao ambao waonekana kupenda saana KUWARITHISHA UKUBWA WA TAIFA HILI kimtindo!!

Endapo Hussein Mwinyi hatojiuzulu ya Gongolamboto kwa kiburi tu kama ya watoto wa marais niliotangulia kuwataja kaskazini mwa bara hili basi huenda hata UKUBWA WA ZANZIBAR unaotazamiwa kwake ukagoma lakini ya Muungano ndio kabisaaaa wa kusikia tu redioni.

Katika hili tayari Vijana wa Tanzania TUMEWASOMA MCHEZO MZIMA na majibu tunayo!!!​
 
Wacha wajichetue tu, saa inakuja na haipo mbali wao ndiyo wataongoza maandamano ya kuing'oa CCM madarakni.Itafika wakati fahamu zitawarudia na watajua kuwa wananchi wanao wapiga risasi na mabomu ndiyo walionunua silaha hizo kwa kodi zao ili ziwalinde na siyo kuwadhuru, napia watazinduka na kujua ukweli kuwa haki inayotafutwa inawahusu na wao kwani wao siyo sehemu ya wale wateule wachache wanaofaidi keki ya taifa, watafika mahali watajitambua kuwa wao wanatumiwa kama vitendea kazi tu na hawa mafisadi.PEOPLESSSSSSSSSSSS POWERRRRRRRRRRRRRRRRR!
 
peoples power is unavoidable an unequivocal thing atlest for the current time
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom