GE2025 Sasa Polepole tumeanza kuelewana, Spana ya jana dhidi ya "wanamtandao" imegonga kwenyewe

GE2025 Sasa Polepole tumeanza kuelewana, Spana ya jana dhidi ya "wanamtandao" imegonga kwenyewe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
16,817
Reaction score
62,027
Sasa bwana Polepole umeanza kuongea vitu serious. Zile episode zako mbili za mwanzo zilikuwa hazijaniimpress hata kidogo maana ulikuwa unaongea vitu vypesivyepesi. Ila tu nilikuwa naenjoy unavyovurugana na wanaCCM wenzako, lakini nilikuwa bado sijashawishika kuona unaongea vitu vya maana. Kwa mfano hoja yako ya kutopenda salamu ya "Nawasalimia kwa Jina la Jamhuri ya Muungano , kazi iendelee" eti unataka salamu ya Yesu asifiwe/Tumsifu Yesu Kristo sijui Assalam Aleikum kwa madai kuwa watanzania ni wacha Mungu na eti salamu ni ibada nikaona hoja yako hiyo haina nguvu maana katiba imekataza serikali kufanya mambo ya dini au mambo yanayofanana na hayo. Na pia salamu yenyewe unayoipenda wewe ni controversial maana ni blasphemy kwa watu wa Imani nyingine.

Anyway turudi kwenye mada. Episode yako ya Jana iligusia mambo yafuatayo yaliyonifurahisha sana

1.Ishu ya katiba mpya, na jinsi ambavyo katiba ya warioba ingekuwa mkombozi wa nchi kupitia vitu vya msingi kama vile "Maadili ya Uongozi" lakini ikahujumiwa na wahuni, wanamtandao na wasaka vyeo. Na ukagusia uzalendo wa wazee kama Jaji Warioba walivyopambana kujaribu kunusuru mchakato wa katiba mpya ili kuwapa watanzania katiba bora. Kumbe ilifikia hatua hadi wajumbe wa tume ya Warioba na Wazee wenye maadili walitaka mzee Warioba achukue fomu ya kugombea urais mwaka 2015 ili akiingia madarakani aweze kunusuru katiba mpya, akapigwa chenga ya mwili na JK kwa kutumwa Burundi mpaka siku muda wa kurejesha fomu ulipoisha ndo akarejea. Hapa umenigusa sana

2. Umeongea Jinsi wajumbe wa iliyokuwa Tume ya katiba ya warioba walivyoshukuru na kufurahi pale Tume ya Taifa ya uchaguzi ilipositisha mchakato wa kura ya maoni ya "Katiba Pendekezwa" (Ile ya CCM) kwa sababu katiba pendekezwa ilikuwa mbaya, ilikuwa imetupilia mbali mambo ya msingi yaliyokuwa kwenye rasimu ya Warioba ambayo ndiyo maoni ya wananchi. Na ukaeleza kuwa Hata Magufuli alivyositisha kuita kura ya Maoni ili kuibariki katiba mbovu "pendekezwa" lilikuwa ni jambo sahihi, kwa sababu ile rasimu pendekezwa wasimamia show walikuwa wanamtandao.

3. Nimefurahi ulivyoendelea kuwa consistent na message ya kutaka kanuni na taratibu za CCM ziheshimiwe, ukaonyesha wazi kuwa huna chuko binafsi na Samia, bali kuna genge la wanamtandao ambao loyalty yao imegawanyika mara mbili, upande mmoja wanamtumikia yeye lakini upande wa pili wanatumikia genge lao la wanamtandao. Ukasema hata Idara ya usalama wa Taifa inalijua hili, wanamwambia lakini unfortunately hachukui hatua.

4. Ukakemea chama kuwa kama cha kidynasty, cha kifamilia, cha koo fulani fulani hivi. Na kugeuza ubunge na uwakilishi kama kilindi cha "DILI", Ndugu wa viongozi wamejazana kwenye kugombea ubunge utafikiri hii nchi ya masultani. Kwa kweli hili wananchi tunaliona, linatukera sana. Kiukweli hatuwezi kupata bunge la kuisimamia serikali kama waliojazana bungeni ni ndugu, watoto na mashosti wa watawala. Litakuwa bunge la rubber stamp tu, wagonga meza na wala posho.

USHAURI WANGU WA NAMNA YA KUSONGA MBELE:

1. Komaa na ishu ya Mabadiliko a.k.a REFORMS, wananchi wanataka mabadiliko sana. Endelea kukomaa na ishu ya katiba mpya, tena katiba inayonyoosha mabo siyo katiba vague, bosheni, ambayo itaendelea kulinda maslahi ya magenge kama ya wanamtandao. Tunataka Katiba yeneye maadili ya uongozi ndani na katiba inayocriminalize kuvuruga na kuharibu uchaguzi wa Rais, Wabunge na madiwani. Hii message ukiisimamia itakupa uungwaji mkono sana wa wananchi. Mwalimu alipambana na "UNDUGUNAIZESHENI", lakini cha ajabu CCM ya Samia inaupromote.

2. Endelea kupiga nyundo spana kuhusu ulegelege wa serikali hii hasa katika huduma za msingi za wananchi, Maji, Umeme, Afya. Yaani hivi ndo vitu tunavyotaka kuvisikia.

3. Gonga spana kuhusu ufisadi, rejea ripoti za CAG, piga nyundo kuhusu utajiri wa viongozi, Yaani wachape kisawasawa

4. Kuna ishu ya rasilimali zetu, komaa na ishu za madini, bandari misitu na mamikataba mabovumabovu wanayoingia. Ili ueleweke zaidi kwa umma. Kama una ushahidi vijana wa kileo wanaita "receipts“ lete

5. Na ishu ya kanuni, katiba na utaratibu ndani ya CCM usiiache, komaa nayo mpaka message ifike kwa wanaCCM. Hii message inabidi irudiwe mpaka chama kione kuwa kimekosea na ili kiogope siku nyingine kuvuruga utaratibu kwa ajili ya maslahi ya watu wachache.

6. Wanamtandao usiwaache, na huyu mstaafu ambaye naye anajifanya Mwambata wa rais endelea kumpa za uso ili akalee wajukuu zake, Japo sisi wengine tunampenda kwa sababu ya uungwana wake, na freedom of spaech enzi zake lakini hii ya kujifanya ni kumbikumbi mwenza warais inatuput off, Naye apigwe "spana" ili akaandike kitabu cha utawala wake kama wenzie, au angalau ajikite huko kwenye mambo ya kimataifa lakini mambo ya kila siku ya uendeshwaji wa nchi yetu hatutaki kumuona mbelembele.

7. Komaa na matendo ya utekaji watu, upotezwaji watu, hapa utasaidia watu wengisana ambao wako kwenye rada ya kutekwa na kupotezwa. Ninajua fika kuwa enzi zenu za utawala wa JPM hamkuwa safi hata kidogo kwenye hii angle, lakini jibu lako kila ulipoulizwa kuwa ulikuwa wapi wakati haya yanatokea enzi za JPM japo si zuri sana lakini angalau umejibu. Hata hivyo ili kuwanusuru Wabongo na kunusuru freedomof speech anza kuwasemea watu wanaotekwa, waliotekwa na ambao wako katia radar ya kutekwa na kupotezwa sababu ya maoni yao. Sasa imagine unamteka na kumpoteza mtoto kama Deusdedith Soka ili iweje?

8. Usisahau kusemea jambo la kuminya uhuru wa wa maoni ya watu, Hii Tabia ya kufungia mitandao eti kwa sababu Gwajima ana press conference,au kufungia mitandao kwa sababu Polepole anaongea. Itake serikali iache uoga, iache ukunguru wa kuharibu maisha ya watu kwa sababu ya uoga wa kisiasa. Waache kukwepa hoja kwa kufungia mitandao bali wajibu hoja za wananchi

Ebwana kiufupi next episode tunataka kusikia vitu vzitovizito, tuchomekee zile za "ndanindani" sometime, achana na kuongea vitu abstract!
 
Huyo mjinga hana muda na mabadiliko ya kweli
Yeye amekomaa na katiba ya ccm kwahiyo sahau yuko mitandaoni kwa maslahi mapana ya wananchi
 
Ameanza kuzungumza vitu vya kitaifa na hapo kanifanya nimuone kuwa ameanza kuwa serious
Anaenda na upepo
Ameona waliianza kumgeuka kila siku kuongelea sijui mila na desturi za chama baada ya kupigwa spana kuwa katiba ya ccm inaruhusu makamu wa raisi kugombea uraisi hapo akapoteza mashiko kama sasa anaongelea mabadiliko kwa ujumla huu ni unafiki na sio sababu ilifanya ajiuzulu
Anatafuta pa kushika….
 
acha kutetea ujinga basi ndugu yangu, you better shut up basi hata kidogo
 
Makubwa tena haya, kuwa PolePole anachoongea hakina maana ila mwenye maana ni wewe sio?
Tatizo la wabongo mnapenda kusikia mnayotaka kusikia hamtaki kusikia tofauti
Hata kama mna mawazo toafauti na ccm lakini kasumba ya kutotaka maoni mbadala mmetoka nayo ccm kama walivyo kawaida yao
 
Sasa bwana Polepole umeanza kuongea vitu serious. Zile episode zako mbili za mwanzo zilikuwa hazijaniimpress hata kidogo maana ulikuwa unaongea vitu vypesivyepesi. Ila tu nilikuwa naenjoy unavyovurugana na wanaCCM wenzako, lakini nilikuwa bado sijashawishika kuona unaongea vitu vya maana. Kwa mfano hoja yako ya kutopenda salamu ya "Nawasalimia kwa Jina la Jamhuri ya Muungano , kazi iendelee" eti unataka salamu ya Yesu asifiwe/Tumsifu Yesu Kristo sijui Assalam Aleikum kwa madai kuwa watanzania ni wacha Mungu na eti salamu ni ibada nikaona hoja yako hiyo haina nguvu maana katiba imekataza serikali kufanya mambo ya dini au mambo yanayofanana na hayo. Na pia salamu yenyewe ni controversial maana ni blasphemy kwa watu wa Imani nyingine.

Anyway turudi kwenye mada. Episode yako ya Jana iligusia mambo yafuatayo yaliyonifurahisha sana

1.Ishu ya katiba mpya, na jinsi katiba ya warioba ingekuwa mkombozi wa nchi kupitia vitu vya msingi kama vile "Maadili ya Uongozi" lakini ikahujumiwa na wahuni, wanamtandao na wasaka vyeo. Na ukagusia uzalendo wa wazee kama Jaji Warioba walivyopambana kujaribu kunusuru mchakato wa katiba mpya ili kuwapa watanzania katiba bora. Kumbe ilifikia hatua hadi wajumbe wa tume ya Warioba na Wazee wenye maadili walitaka mzee Warioba achukue fomu ya kugombea urais mwaka 2015 ili akiingia madarakani aweze kunusuru katiba mpya, akapigwa chenga ya mwili na JK kwa kutumwa Burundi mpaka siku muda wa kurejesha fomu ulipoisha ndo akarejea. Hapa umenigusa sana

2. Umeongea Jinsi wajumbe wa iliyokuwa Tume ya katiba ya warioba walivyoshukuru na kufurahi pale Tume ya Taifa ya uchaguzi ilipositisha mchakato wa kura ya maoni ya "Katiba Pendekezwa" (Ile ya CCM) kwa sababu katiba pendekezwa ilikuwa mbaya, ilikuwa imetupilia mbali mambo ya msingi yaliyokuwa kwenye rasimu ya Warioba ambayo ndiyo maoni ya wananchi. Na ukaeleza kuwa Hata Magufuli alivyositisha kuita kura ya Maoni ili kuibariki katiba mbovu "pendekezwa" lilikuwa ni jambo sahihi, kwa sababu ile rasimu pendekezwa wasiamia show walikuwa wanamtandao.

3. Nimefurahi ulivyoendelea kuwa consistet na message ya kutaka kanuni na taratibu za CCM ziheshimiwe, ukaonyesha wazi kuwa huna chuko binafsi na Samia, bali kuna genge la wanamtandao ambao loyalty yao imegawanyika mara mbili, upande mmoja wanamtumikia yeye lakini upande wa pili wanatumikia genge lao la wanamtandao. Ukasema hata Idara ya usalama wa Taifa inalijua hili, wanamwambia lakini unfortunately hachukui hatua.

4. Ukakemea chama kuwa kama cha kidynasty, cha kifamilia, cha koo fulani fulani hivi. Na kugeuza ubunge na uwakilishi kama kilindi cha "DILI", Ndugu wa viongozi wamejazana kwenye kugombea ubunge utafikiri hii nchi ya masultani. Kwa kweli hili wananchi tunaliona, linatukera sana. Kiukweli hatuwezi kupata bunge la kuisimamia serikali kama waliojazana bungeni ni ndugu, watoto na mashosti wa watawala. Litakuwa bunge la rubber stamp tu, wagonga meza na wala posho.

USHAURI WANGU WA NAMNA YA KUSONGA MBELE:

1. Komaa na ishu ya Mabadiliko a.k.a REFORMS, wananchi wanataka mabadiliko sana. Endelea kukomaa na ishu ya katiba mpya, tena katiba inayonyoosha mabo siyo katiba vague, bosheni, ambayo itaendelea kulinda maslahi ya magenge kama ya wanamtandao. Tunataka Katiba yeneye maadili ya uongozi ndani na katiba inayocriminalize kuvuruga na kuharibu uchaguzi wa Rais, Wabunge na madiwani. Hii message ukiisimamia itakupa uungwaji mkono sana wa wananchi. Mwalimu alipambana na "UNDUGUNAIZESHENI", lakini cha ajabu CCM ya Samia inaupromote.

2. Endelea kupiga nyundo spana kuhusu ulegelege wa serikali hii hasa katika huduma za msingi za wananchi, Maji, Umeme, Afya. Yaani hivi ndo vitu tunavyotaka kuvisikia.

3. Gonga spana kuhusu ufisadi, rejea ripoti za CAG, piga nyundo kuhusu utajiri wa viongozi, Yaani wachape kisawasawa

4. Kuna ishu ya rasilimali zetu, komaa na ishu za madini, bandari misitu na mamikataba mabovumabovu wanayoingia. Ili ueleweke zaidi kwa umma. Kama una ushahidi vijana wa kileo wanaita "receipts“ lete

5. Na ishu ya kanuni, katiba na utaratibu ndani ya CCM usiiache, komaa nayo mpaka message ifike kwa wanaCCM. Hii message inabidi irudiwe mpaka chama kione kuwa kimekosea na ili kiogope siku nyingine kuvuruga utaratibu kwa ajili ya maslahi ya watu wachache.

6. Wanamtandao usiwaache, na huyu mstaafu ambaye naye anajifanya Mwambata wa rais endelea kumpa za uso ili akalee wajukuu zake, Japo sisi wengine tunampenda kwa sababu ya uungwana wake, na freedom of sppech enzi zake lakini hii ya kujifanya ni kumbikumbi mwenza warais inatuput off.Naye apigwe "spana" ili akaandike kitabu cha utawala wake kama wenzie, au anagalu ajikite huko kwenye mambo ya kimataifa lakini mambo ya kila siku ya uendeshwaji wa nchi yetu hatutaki kumona mbelembele.

Ebwana kiufupi next episode tunataka kusikia vitu vzitovizito, tuchomekee zile za "ndanindani" sometime, achana na kuongea vitu abstract!
Ishu na reform za chadema na mazungumzo ya jamaa unaona wako sawa sema utofauti wao ni itikadi zao zakichama lakini wote wako juu ya matumaini ya Tanzania mpya
 
Back
Top Bottom