Sasa niko tayari kuolewa na Nassari!

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
mdee.jpg


Siku moja baada ya kufanikiwa kulitwaa jimbo la Arumeru Mashariki, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) ametoa kali ya mwaka baada ya kudai kuwa sasa yuko tayari kuolewa na Mbunge mteule Joshua Nassari. Akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha na Meru juzi katika viwanja vya Leganga kusherehekea ushindi wa chama chake katika uchaguzi huo, Mdee alisema yeye na chama chake walikuwa busy na kampeni za kuhakikisha Chadema inatwaa jimbo la Arumeru Mashariki na ndiyo sababu hakujibu mara moja maombi ya Nassari ya kumwoa aliyoyatoa katika moja ya mikutano yake ya kampeni.


“Naondoka kwenda Dar es Salaam kujiandaa kwa Mkutano ujao wa Bunge, kisha nitakwenda Dodoma ambako nitamsubiri Nassari na kwa pamoja tutafanya maandalizi,” alisema Mdee huku akishangiliwa na hadhira hiyo huku wakiimba na kucheza katikati ya mvua iliyokuwa ikinyesha.


Mdee alidai ndoa kati ya wabunge hao wawili wa Chadema ni wazo zuri na itatangazwa sana na kuandika historia. Alipoona anashambuliwa sana na wapinzani wake juu ya useja wake katika kampeni hizo, Nassari hatimaye alitangaza kumwoa Mdee ambaye pia hajaolewa.


E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
 
huyu kamanda mdee nilikuwa nammendea labda atanidondoshea zali!!nimeamini shilingi inakaa na shilingi...
 
huyu kamanda mdee nilikuwa nammendea labda atanidondoshea zali!!nimeamini shilingi inakaa na shilingi...

Siku zote mwenye nacho huongezewa na asiyekuwa nacho hata kile alichonacho atanyang'anywa.
 
nilipoiona Heading nikadhani Young Master upo tayari kuolewa na Josh Nassari
 
duh !isha kuwa asubuhi sasa na ndoto imeshayeyuka!mdee nitakumiss ndotoni!
 
Back
Top Bottom