Sasa Ni Too Much

Ndallo

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Posts
7,619
Reaction score
4,303
Kweli magonjwa yako mengi na tunajua kila mtu anayekwenda kule kwa Babu Loliondo anataka kupata ile dawa ili apone maradhi sugu kama babu alivyosema kua dawa ile ambayo ameoteshwa na Mungu kama alivyonukuliwa na vyiombo vya habari. Babu kasema dawa ile inatibu magonjwa sugu kama vile Pumu/Kisukari/Kansa/Presha/Ukimwi na vidonda vya tumbo. Sasa hii niliyoisikia kwa jamaa waliofunga safari tena kwakutumia nauli kubwa tu na kwenda kushinda kwenye mazingira magumu kule Loliondo wamekwenda kupata dawa kwa Babu ili waongeze nguvu za kiume! Jamani hembu kwa wale waliotoka kwa babu hizi siku mbili je Babu ameshaanza kutoa tiba hii ya kuongeza nguvu za kiume? mimi nilitoka huko wiki kadhaa lakini sikusikia kama kuna matibabu haya! Nawasilisha.
 
Ndugu yangu mi naona hao wamechanganyikiwa tu au wanazuga walikuwa na magonjwa mengine tu.
 
Mkuu wewe ulikuwa kwa babu halafu unatuuliza sie ambao hata kwenda hatujakwenda. I think uko na contact za huko kwa babu why don't you take an effort and ask them??
 
Mkuu wewe ulikuwa kwa babu halafu unatuuliza sie ambao hata kwenda hatujakwenda.


Kweli Da, labda mkuu ndallo kwanza utuambie wewe ulienda kufanya nini ili na wao wawe wawazi???
 
Ninachojua ni kwamba wale waliokuwa na matatizo ya Kisukari, kweli kabisa ndoa zao sasa zina heshima kubwa, maana wanadumisha mila kama zamani, hiyo haina ubishi!
(Na ijulikane kwamba kisukari na yale mambo yetu ni kama maji na moto!)
 
Kuna vijana mtaani kwetu walikuwa wanajipanga ili kwenda kusaka dawa ya utajiri kwa babu, nikajiuliza au babu anatoa dawa ya chochote kinachokusibu...!!
 
JF kiboko aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…