Sasa ni hatari kama Taifa kuwa na mfumo wa elimu usiojali. Tutafakari,tujipange

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,030
3,908
Naandika haya kama Mtanzania Mzalendo ambaye ninaamini kabisa kwamba Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe na kwa faida za Watanzania wenyewe.

Ninatambua kwamba katika hili la elimu kunaweza kuwa na mambo mengi sana ila tukubali tukatae "ELIMU YETU INA MATATIZO MAKUBWA SANA"

Baadhi ya matatizo hayo ni:
  1. UZalishaji wa wahitimu ambao ni INCOMPETENT
  2. Uzalishaji wa wahitimu katika Fani ambazo sio Productive
  3. Uzalishaji wa wahitimu ambao hatuna nafasi au uwezo wa kuwaajiri
  4. Mfumo wa elimu unaopoteza Rasilimali watu.
  5. Uwekezaji(Financing) katika elimu
Kwa kuitazama elimu yetu ya Tanzania imegawanyika katika maeneo/Ngazi tofauti kama hapa chini:
  1. Elimu ya msingi ambayo ni ya wote
  2. Elimu ya Sekondari ambayo nayo inapaswa kuwa ya wote
  3. Elimu ya Chuo Kikuu
  4. Vyuo Vya Ufundi
  5. Vyuo vya ufundi standi
  6. Vyuo vya maendeleo ya jamii(Folk development)
Ngazi zote nilizotaja hapo zinaonyesha kwamba tunao mfumo mzuri wa elimu ingawa hatuutendei haki ipasavyo.

Binafsi nafikiri kwamba ingependeza kama tungeutumia mfumo wetu ipaswavyo kwa kufanya yafuatayo:

Kwanza ni kuhakikisha kwamba hakuna mwanafunzi anayeachwa nyuma katika elimu eti kwa sababu amefeli.Hata aliyefeli na kupata sufuri bado kuwa na mfumo wa elimu ambao unaweza kumpokea na kumlea kumfanya awe mwanajamii anayeweza kuzalisha na kuchangia katika maendeleo.

Pili mfumo wa kufinance elimu yetu uwe separate kwa maana ya kwamba tuwe na mfuko wa elimu (EDUCATION FUND) ambao utachangiwa kwa kupitia mfumo wa kodi,misaada na michango ya hiyari)

Tatu Usimamizi wa elimu uwe chini ya Taasisi Moja(National Education Board) ambayo itasimamia masuala yote yahusuyo elimu ikiwamo, TCU, NACTE, VETA, NECTA, TIE na masuala mengine yahusuyo elimu na usimamizi wake.

Nne ni kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanaosoma Public pamoja na private school wanapatiwa RUZUKU kulingana na kiwango kilichowekwa na serikali ili kuhakikisha kwamba mzigo wa gharama ya elimu unapungua na kuhamasisha wazazi na watu binafsi kuwekeza katika utoaji wa elimu,

Tano ni kuanza kutoa elimu kwa kuzingatia mahitaji huku tukisisitiza elimu ambayo inamuwezesha mtu kujiajiri ikiwamo,Ufundi,Ujasiriamali na Teknolojia.

Binafsi naamini kwamba hili swala linahitaji mjadal mpana sana na kwamba kila mmoja wetu anaweza kuwa na fikra zake lakini mwisho wa siku tunapaswa kuangalia namna bora ya kuhakikisha kwamba tunakuwa na mfumo wa elimu wenye maslahi kwa taifa letu.
 
Sasa wewe umeanza vizuri kwa kusema kuwa kuna uzalishaji wa wahitimu ambao ni INCOMPITENT, halafu mbele unapendekeza eti wachukuliwe wanafunzi wote hata waliopata Zero..

Hhhm! Kazi ipo. Muelimishaji nae anahitaji kuelimishwa.
 
Sasa wewe umeanza vizuri kwa kusema kuwa kuna uzalishaji wa wahitimu ambao ni INCOMPITENT, halafu mbele unapendekeza eti wachukuliwe wanafunzi wote hata waliopata Zero..

Hhhm! Kazi ipo. Muelimishaji nae anahitaji kuelimishwa.
Mkuu kama umenisoma vizuri nimesema kwamba hata wale wanaopata zero wanaweza kuingia katika mfumo wa elimu kama vile vyuo vya maendeleo ya Wananchi(FDC).Cha muhimu ni kuhakikisha kwamba hakuna hata mmoja anayeachwa nyuma
 
Inakuwaje mzazi analipa mamilioni kuanzia nursery hadi A level afu chuo anakataa kulipa akitegemea kukopeshwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Umejiuliza alipata wapi hela ya kulipa? Labda alipata mfadhiri kwa primary Na secondary tu, au kipindi hicho alikuwa na uwezo sasa hivi hana! zipo sababu nyingi tu. Usiwe mwepesi Wa kutoa maamuzi!
 
Back
Top Bottom