Sasa ni dhahiri kwamba Nape Nnauye anaumwa na anahitaji msaada wa daktari

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Sasa ni dhahiri kwamba Nappe anaumwa na anahitaji msaada wa daktari. Kitendo cha kila wakati kukumbuka matukio aliyofanya zamani ni dalili mojawapo ya Hyperthymesia.

Hyperthymesia ni tatizo la akili linalofanya mgonjwa kutumia muda mwingi kufikiria mambo yake ya zamani, hususani mazuri aliyofanya (spending an excessive amount of time thinking about one's past, and displaying an extraordinary ability to recall specific events from one's past).

Watu wengi wanaougua ugonjwa huu ni waliowahi kuwa matajiri lakini wakafilisika, waliowahi kuwa na madaraka makubwa lakini wakayapoteza, au waliowahi kuwa na wapenzi waliowapenda sana lakini wakawapoteza. Watu hawa hutumia muda mwingi kukumbuka enzi zao walipokua kwenye fedha/madaraka/mahaba na kila mara hupata hasira au kujutia wanapokumbuka.

Hii ndio hali anayopitia Nappe kwa sasa. Hyperthymesia. Ndio maana tangu afukuzwe uwaziri amekuwa akiweweseka kila mara kutuma picha za matukio yake ya zamani, zinazoonesha alivyoisaidia CCM kushinda. Mara akiwa kwenye mtumbwi, mara akiwa vijijini, mara akiwa vijijini, mara alipovunjika mkono etc. Hizi ni dalili za Hyperthymesia.

Ni kama vile anajutia kuwa alitumia muda mwingi kuisaidia CCM lakini haioni thamani yake. Ni sawa na mtu aliyejitolea kwa hali na mali kumsaidia mpenzi wake kwa kumsomesha au kumpa mtaji wa biashara, kisha baada ya huyo mpenzi wake kufanikiwa akamtosa. Kwa vyovyote vile mtu huyu lazima atakumbwa na Hyperthymesia. Atakumbuka nyakati nzuri enzi zake na mpenzi wake, namna alivyomsaidia na namna alivyompoteza. Atajikuta anajutia au kusikitika. Nappe is suffering from Hyperthymesia.

Kuna watu wanamuunga mkono wakidhani ni sahihi kuzungumza kwa kuwa eti si waziri tena. Wanasema kwa sasa ni mbunge kwahiyo anaweza kusema lolote. Hii si sahihi hata kidogo. Wamesahau kuwa Nappe ni mjumbe wa mkutano mkuu wa ccm, ni mjumbe wa Halmashauri kuu (NEC) na pia ni mjumbe wa Kamati kuu (CC). Huko kote anaweza kupeleka hoja zake na zikasikilizwa. Otherwise aongee bungeni.

Kitendo cha kuwa mjumbe wa vikao vyote vikubwa ndani ya ccm kinamfunga kukikosoa chama chake hadharani. Nappe kama mjumbe wa NEC/CC na mkutano mkuu wa Ccm hapaswi kuwa sehemu ya wanaoilaumu CCM hadharani, bali anapaswa kuwa sehemu ya wanaoisaidia CCM kujibu hoja za wanaoilaumu.

Lakini kulalamika mitandaoni na kutuma picha kila wakati zinazoonesha alivyokisaidia CCM si sahihi. Ni sawa na kujaribu kuvunja nyumba ambayo anaishi ndani. The best thing ni kutoka ili aivunje vizuri akiwa nje, au walioko ndani wakufukuze usiendelee kuharibu nyumba yao.

Criticism of scientific management inamtaka afanye hivyo. Ndio maana wabunge wa vyama vingine hawawezi kukosoa vyama vyao hadharani just because sio viongozi wa vyama hivyo. Wana mahali ambapo wanaweza kuwasilisha hoja zao na zikafanyiwa kazi. Wanaoshabikia Nappe aivue nguo ccm kisa sio waziri, ni sawa na wanaoshabikia mbunge wa Chadema au Cuf akilaumu chama chake hadharani kisa sio kiongozi wa chama. Sio sahihi.

Namshauri Nappe akae kimya ili kulinda heshima yake na chama chake. Kama hawezi kukaa kimya aondoke ili aweze kukikosoa vizuri zaidi akiwa nje. Wataalamu wa afya ya akili wanaweza kukaa nae karibu ili kumpa msaada zaidi katika kipindi hiki kigumu anachopitia.

NOTE: Ushauri huu nimeutoa kama "mchambuzi huru" wa masuala ya kisiasa. Nimeamua kuweka itikadi kando. Maana ningeamua kujadili kwa itikadi yangu nilipaswa nifurahie mgogoro kati ya Nappe na chama chake maana ni credits kwetu. Adui wa adui yako anapaswa kuwa rafiki yako. So nilipaswa nifurahie ugomvi wao lakini nimemshauri akae kimya, otherwise aondoke humo.!

Malisa Godlisten
 
Malisa GJ
Mkuu Uchambuzi wako nimeupenda/Mzuri, ila mi naona waachwe wavurugane tu mana hakuna namna ingine.
 
Nimeipenda hii.. Kwa hakika hiki ndio kipindi anachopitia Nape.... But sometimes kuna laana zinamuandama ndio maana anaweweseka sana
Laana ndo zitammaliza Nape Nnauye kukosa uwaziri limemuuma sana hayupo sawa kiakili nikikumbuka sheria kandamizi kwenye social media ,kuzima bunge live ni laana mbaya sana labda alijua atakuwa Waziri milele!
 
Well said inatakiwa akae kimya kwa sababu katika kipindi hicho alikuwa anafanya shughuli za chama kwa nafasi aliyokuwa nayo yaani ni kama umsomeshe kijana wako vizuri then ukataka kung'ang'ania ukulipe fadhila kitu ambacho sio lazima sana.
 
pole zake ila kuugua sio kufa, hata mzee lowasa walisema anaumwa hadi leo yuko anadunda tu.....
 
nape akae kimya kwa sasa, ajaribu kutuliza akili yake kama wananchi tupo pamoja naye, makelele ya nini? hajiamini?
 
Back
Top Bottom