Hasara ambayo wafanyabiashara wa masokoni wanaipata baada ya bidhaa zao kuteketea kwa moto unaounguza masoko hayo haipimiki , serikali yao haijali lolote na wala ahadi ya serikali ya kuunda Tume za kuchunguza chanzo cha moto kwenye masoko hayo imegeuka kuwa uongo , hakuna majibu yaliyotolewa hata baada ya Tume hiyo kuundwa .
Ni vema Wafanyabiashara wakaanza kutambua sasa kwamba NI JAMBO LA HATARI SANA kwa wao kuendelea kutumia masoko hayo kama sehemu za kuuzia bidhaa zao , watafute namna ya kufanya , kimsingi Serikali ya Tanzania imeshindwa kuleta ufumbuzi kwenye jambo hili .