Sasa ngoma droo, wanaume nao kutumia vidonge vya majira!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Wanasayansi nchini Uingereza, wamefanikiwa kutengeneza kidonge kisicho na homoni wanachosema kitawafanya wanaume nao wasiwe na uwezo wa kuwapa wanawake mimba kwa saa kadhaa! Kidonge hicho kilichotengenezwa na watafiti kwenye chuo cha Kings mjini London, kinaweza kumezwa na mwanaume saa chache kabla ya kukutana na mwanamke kimwili na kina uwezo wa kumuondolea mwanaume uwezo wa kumpa mimba mwanamke. Hata hivyo uwezo wake utarudi katika hali ya kawaida saa chache baadae.

Mpaka sasa vidonge vyote vya kuzuia mimba vinavyopatikana sokoni ni vile vinavyotumiwa na wanawake. Kwa wale wanaume wanaotaka kushiriki katika kuzuia upatikanaji wa mimba, wanazo nafasi chache sana za kufanya hivyo, ambazo ni ama kutumia kondom, au kufanyiwa upasuaji (vasectomy) ama kuacha kabisa kufanya mapenzi.

Kidonge hicho kilichogunduliwa na Nnaemeka Amobi kwa kushirikiana na watafiti wengine, kinaelekea kuaminiwa na wanawake, kwani hawahitaji kukumbushwa na waume au wapenzi wao kutumia vidonge vya ‘majira’ kila siku ili wasipate mimba. Wataalamu wanaona vidonge hivi vinaweza kugawa jukumu la kupanga uzazi kwa familia, kwani linawapa wahusika wote wawili jukumu la kutumia vidonge vya kuzuia mimba, jukumu ambalo mpaka sasa hubebwa na wanawake peke yao. Lawama hazitakuwepo kwa upande mmoja, mimba isiyotakiwa itakapopatikana, maana wanawake ndio wahanga katika jambo hilo.

Kama hamuamini gongeni hizo link mbili hapo chini:
MaleContraceptives.org -- 'Dry orgasm' pill

MaleContraceptives.org -- Why new male contraceptives?


 
du bora. Nakumbuka kuna mchungaji alikamatwa mwaka huu akiwa na vidonge vya uzazi wa mpango huku akiwa amekiandaa ki dent gesti.
 
afadhali hizi njia za uzazi wa mpango baadhi viliwaumiza wanawake wengine kukondaaa wengine kunenepeanaaaa heri waanze kunywa wanaume sasa. ila mmmmh isije ikaharibu mbegu moja kwa moja!!!!!!!!!
 
Hata vasectomy ipo kwa miaka mingi ila wanaume wengi hawafanyi! Reasons: Wanaume hawana motivation ya kuzuia mimba sababu si wao wanaopata mimba!!

Vacectomy ni njia ya kudumu, na hii inayoelezwa hapa ni ya muda tu, hii inaweza kuleta matokeo mazuri hasa kwetu sisi mabinti, maana ukimwambia mvulana afanye vacectomy ndio umgawie atakushangaa, lakini ukimwambia ameze vidonge vya majira, fasta atawahii duka la dawa lililopo karibu kuvinunua.
 
mungu kaskia sala zangu!! atakoma !!!!,nammezesha mividonge ka pipi tofi!!

Mwenzangu, mbona hii habari kama imechelewa!? yaaani sasa hakuna kutegeana. No pills, no Sex! hagaiwi mtu mpaka mtu abwie vidonge.
 
Shikamoo baba,naona leo umekuja kivingine nimefurahi!
Yani japo wanaume wengi hawaonekani kulifurahiahili,ila ni msaada mkubwa kwao hasa pale wanapohisi wapenzi wao wamewategeshea kushika mimba au kuepusha mimba zisizotakiwa mpaka watakapokuwa tayari na kushirikishwa swala la kuwa na mtoto.
 
Back
Top Bottom