ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,141
- 950
Haya yapo katika mfumo wa Uongozi wetu sasa (Mhe. Tundu Lissu mlimsikia aliponukuu maneno ya Hayati Baba wa Taifa Kuhusu Uongozi wetu na tulipofikia): Mamlaka ya Uteuzi ya Katibu Mkuu Kiongozi: Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania (kwa sasa ni Bw. Philemon Luhanjo ambae alitoka na Mhe. Rais Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiana wa Kimataifa) Mamlaka ya Uteuzi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini: Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mamlaka ya Uteuzi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mamlaka ya Uteuzi ya Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru (PCCB): Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mamlaka ya Uteuzi ya Mdhibiti wa Hesabu za Serikali: Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania. Mtakumbuka kuwa wakati wa kujadili ripoti ya Kamati Teule ya Bunge ya Richmond, kamati ilibanisha wazi kuwa Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru imehusika kwa karibu sana kuupotosha Umma pale ilipobainisha kuwa hakukuwa na ukiukwaji wa Sheria.Kamati ilibaini pia kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa wakati huo akiwa Bw. Johnson Mwanyika (rtd) imeishauri vibaya Serikali na kujikuta ikiingia katika mkataba ambao kama Mwanasheria Mkuu angekuwa makini, basi Taifa lisingeingizwa mkeknge hiuo ambao sasa unaligharibu kwa kutakiwa kulipa takriban Bilioni 110 kwa kampuni ya hewa ya Dowans.Kamati Teule chini ya Uongozi wa Mhe, Mwakyembe ilitoa Mapendekezo yafuatayo:Kamati Teule ya Bunge ya Kuchunguza suala la Bw. David Kitundu Jairo (Katibu Mkuu aliyesimamishwa wa Wizara ya Nishati na Madini) ilibainisha mapungufu makubwa katika Serikali ya JK kusimamia mambo mazito hasa yanayohusu fedha za Umma. Mapungufu haya yameanzia IKULU kwenyewe, ambapo Katibu Mkuu Kiongozi ni kama yupo juu ya Waziri Mkuu na ametumia Ofisi yake Vibaya kupoitosha Umma kuwa Jairo hana hatia ya kufuja fedha za umma (alifanya hivyo kwa sababau binafsi za Kumsafisha kwa staili ile ile iliyowsafisha akina Patrick Rutabanzibwa, Arthur Gwanaloli K. Mwakapugi., Johnson Mwanyika, Edward Hosea, Donald Chidowu na wenzake kwa hofu kuwa wakicvhukuliwa hatua Serikali itajikuta ikiingia katika mzigo mwnigine Mkubwa wa kulipa deni iwapo itashindwa Mahakamani kama watumishi hao wangefungua kesi kutokana na kutoridhika na hatua za Nidhamu zilizochukuliwa. Wakati ule, Ofisi ya Waziri Mkuu ndio iliyotoa taarifa Bungezi za Kuwasafisha watendaji hao wa Umma, hivyo kwenda Kinyume na Mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge (somahttp://lukwangule.blogspot.com/2008/08/taarifa-ya-waziri-mkuu-kuhusu-richmond.html).
AZIMIO NAMBA 7;Wajumbe wote wa kamati ya Serikali ya majadiliano (Government Negotiation Team-GNT) ambao ni maafisa waandamizi wa Serikali wawajibishwe kwa manufaa ya umma kwa kulitia hasara taifa kutokana na kushindwa kutumia elimu na ujuzi wao kulinda maslahi ya taifa.HATUA ZILIZOCHUKULIWA:Katika kushughulikia suala hili (yaani katika mchakato mzima wa zabuni pamoja na majadiliano ya mkataba baina ya Tanesco na Richmond kulikuwa na kamati za aina tatu.Kwanza ni kamati iliyokuwa inaundwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mheshimiwa Johnson Mwanyika (mb) katibu Mkuu wa wizara ya nishati na madini Arthur Mwakapugi pamoja na akatibu mkuu wizara ya fedha na uchumi Gray Mgonja. Kamati hii ilikuwa na jukumu la kutoa ushauri kwa Waziri wa Nishati na Madini na Serikali kwa ujumlaKamati ya pili ilikuwa ni timu ya wataalamu (expert team) iliyokuwa na wajumbe na Taasisi zifuatazo:1. Singi Madata –Fedha na Uchumi (Mwenyekiti)2. Dk Lutengano Mwakahesya- Nishati na Madini (Mjumbe)3. Theophilo Bwakea –Nishati na madini (mjumbe)4. Stephen Mabada –Tanesco (mjumbe)5. Athanas Mbawala –tanesco (mjumbe)6. James Mwalilimo –Tanesco (Mjumbe)7. Julius Sarota –Nishati na Madini (mjumbe)Kamati hii ilikuwa na jukumu ya kutathmini wazabuni wote waliokuwa wameomba zabuni za mitambo ya kukodi ya dharura ya kufua umeme wa megawati 105.6.Kamati ya tatu ni ile ya majadiliano ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Richmond Development Company LLC. Wajumbe wa kamati hii ni:1. Singi Madata –Fedha na Uchumi (Mwenyekiti)2. Theophilo Bwakea –Nishati na madini(mjumbe)3. Stephen Mabada –Tanesco (Mjumbe)4. Godson Makia –Tanesco(Mjumbe)5. Donald Chidowu –Ofisi ya Mwanasheria Mkuu (Mjumbe)6. Dick Tewa –Benki Kuu (Mjumbe)7. Gideon Nassari –CTI (Mjumbe)8. Julius Sarota –Nishati na Madini (Sekretarieti)9. Mwita Wangwe –Tanesco (Sekretariet)Kamati mbili za wataalam (yaani kamati ya pili na ya tatu) zote zilikuwa zinaripoti na kutoa ushauri kwa kamati ya makatibu wakuu wawili wa Hazina, na Nishati na Madini pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Kwa madhumuni ya utekelezaji wa Azimio hili, wajumbe wote wa kamati hizi tatu wamepelekewa barua za kutakiwa watoe maelezo kwa mujibu wa Sheria zinazohusu nidhamu katika utumishi wao.Hatua hii inazingatia Misingi ya Kanuni Asili ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice), kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.Miongoni mwa maeneo ambayo watumishi hawa wametakiwa kutoa maelezo ni jinsi walivyohusika katika mchakato mzima na kuingiza Serikali katika mkataba unaonekana kutokuwa na maslahi kwa Taifa.Maeneo hayo ni pamoja na🙁i) Kutotumia utaalamu na uzoefu wao kikamilifu ili kutambua mapema kuwa Richmond Development Company LLC haikuwa na uwezo kitaalamu, kifedha na kuzoefu na hivyo kutokidhi matakwa ya zabuni.(ii) Kutozingatia kikamilifu Sheria ya Manunuzi ya Umma, ya mwaka 2004 katika mchakato mzima wa kutoa zabuni.(iii) Wajumbe kushindwa kuishauri Serikali kuhusu kuifanyia Kampuni ya Richmond Development LLC uchunguzi wa awali (Due Diligence) pamoja na ukaguzi baada ya tathmini ya zabuni (post qualification)(iv) Kutokuwa makini na hivyo kushinddwa kutambua udanganyifu wa ubia/ uhusiano wa kibiashara kati ya Richmond Development Company LLC na Pratty & WhitneyWatumishi wote wameshawasilisha utetezi wao katkka muda wa siku 14 zilizopangwa. Aidha, hivi sasa utetezi wao unafanyiwa uchambuzi wa kina na Mamlaka zao za nidhamu ili hatua muafaka zichukuliwe kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotawala Utumishi wao.Kwa upande wa watumishi wa Tanesco ambao ni Stephen Mabada, Athanas Mbawala James Mwalilimo, Godson Makia na Mwita Wangwe, Kamati Ndogo ya Nidhamu ya Bodi ya Tanesco tayari imekwisha pitia maelezo ya watumishi wao wote na mapendekezo ya kamati hiyo yamewasilishwa kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco ambayo itatoa maamuzi yake na kuishauri Serikali.
AZIMIO NAMBA 9"Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru awajibishwe kwa manufaa ya Umma na Maofisa wa Takukuru walioshiriki katika zoezi la uchunguzi kuandaa Taarifa ya Richmond Development Company LLC iliyoficha ukweli nao pia wawajibishwe kwa manufaa ya Umma"Zoezi la kufanya uchunguzi lililofanywa na Takukuru lilihusisha watumishi wafuatao🙁i) Mkurugenzi wa Takukuru, Edward Hosea akiwa ndiyo msimamizi mkuu wa Takukuru, iliyohusika na uchunguzi wa mchakato wa mzima wa zabuni ya umeme wa dharura, ulioipa ushindi kampuni ya Richmond Development Company LLC.(ii) Mkurugenzi wa Upelelezi, Alex Mfungo ambaye ndiye alisimamia zoezi zima la uchunguzi na kuandaa ripoti ya uchunguzi ya Takukuru kuhusu suala hili.(iii) Maofisa wanane wa Takukuru walioshiriki katika zoezi la uchunguzi na kuandaa taarifa katika maeneo yao ya utaalamu katika mchakato mzima wa Zabuni ya ununuzi wa mitambo ya umeme wa dharura ulioipa ushindi kampuni ya Richmond Development Company LLCIli kutekeleza azimio hili, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru amepelekewa barua ya kutakiwa kujieleza na Mamlaka yake ya Nidhamu ambayo ni Katibu Mkuu Kiongozi. Vilevile wasaidizi walio chini yake walioshiriki katika zoezi hilo nao wametakiwa kutoa maelezo yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru ambaye ndiye mamlaka yao ya Nidhamu. Hii ni kuzingatia Misingi ileile ya Kanuni Asilia ya Haki ya Kusikilizwa Kwanza (Natural Justice).Hatahivyo kwa kuzingatia mazingira ya shauri hili, Katibu Mkuu Kiongozi ataamua juu ya utaratibu mzuri wa hatua za nidhamu dhidi ya wasaidizi wote wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru waliohusika katika suala hili.Baadhi ya maeneo ambayo Mkurugenzi Mkuu na Wasaidizi wake wamepelekewa barua wajieleze ni yafuatayo:
Ona sasa: Bunge lile lile lililotofautiana wakati wa kujadili Ripoti ya Utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati Teule ya Richmond linapendekeza Serikali ile ile iwawajibishe wafuatao kwa kutumia vyombo vile vile vya Dola🙁i) Katibu Mkuu Kiongozi, Bw. Philemon Luanjo kwa kupotosha umma na kumkingia kifua Jairo, kumdharau Waziri Mkuu na Bunge (Kutumia madaraka yake Vibaya).(ii) Waziri na Naibu Waziri Wa Nishati Na Madini (Mhe. William Ngeleja na Adam Malima ) kwa uzembe wa kutofuatilia nini kilichokuwa kikitokea katika Wizara yao na pia kusaini malipo ya takrima za milioni 4 kinyume na taratibu;(iii) Bw. David Kitundu Jairo katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini kwa kutumia madaraka vibaya kwa kukusanya fedha kutoka katika mashirika na taasisi za umma zilizochini ya Wizara ya Nishati na Madini na kuzitumia kinyume na Sheria, Kanuni na Taratibu za Kifedha na Waraka wa Hazina wa kuzuia jambo kama hilo katika Wizara na Taasisi za Umma;(iV) Bw. Ludiovick Utoh Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kwa kwa kupotosha Umma na kutumia madaraka yake vibaya kwa nia ya kumkingia Kifua Jairo.(v) Watumishi wengine wote wa Umma waliopokea fedha kinyume cha Sheria (vi) Watendaji wakuu wa Taasisi zilizochangishwa Fedha kwa kukiuka waraka wa Hazina. Hii imekaa vibaya kwa kuwa sasa ni IKULU yenyewe imechafuka.Anayepaswa kushauri katika hili juu ya hatua za Kisheria zinazopaswa kuchukuliwa ni Ofisi ya Rais kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu - UTUMISHI WA UMMA (Chini ya Katibu Mkuu Kiongozi) na pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Katika lile la RICHMOND, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilichafuka lakini ni hiyo hiyo ilitumikwa kutoa sushauri wa kisheri juu ya hatua za kiusheria za kuchukuliwa. Wakati ule wa Richmond pia Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nayo ilichafuka na ndio iliyopaswa kuwachukulia hatua za jinai wote waliohusika...Wabunge waliahamaki walipojadili hii ya Jairo, wakiwa wamesahau ya RICHMOND..walipendekeza kuwa " wote wanaohusika wachunguzwe na TAKUKURU" (Takukuru inayoongozwa na Dr. Edward Hosea ambaye wakati ule wa Richmond wabunge walionyesha kupoteza imani nae!!) sasa IKULU ndio imechafuka na tunaomba IKULU ichukue hatua za kisheria kwa wale wote waliohusika....AZIMIO NAMBA 7:"…Maofisa Waandamizi wa Serikali wawajibishwe kwa manufaa ya Umma…".AZIMIO NAMBA 9:"… wawajibishwe kwa manufaa ya Umma."AZIMIO NAMBA 14:"…Wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza Taifa kwa makusudi kwenye Mkataba wa Kampuni ya Mfukoni,"8. Mheshimiwa Spika, katika kutafsiri maana ya maelekezo haya, Serikali imeona kwamba yanaweza kuwa na maana ya kushtakiwa Mahakamani kwa Makosa ya Jinai; ama kutumia Mamlaka ya Rais ya kuwastaafisha kwa manufaa ya Umma; ama kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa Umma na kanuni zake.Serikali baada ya kutafakari kwa kina suala hili, imeona kuwa katika mazingira ya suala hili, ni busara kutumia utaratibu wa hatua za mashtaka ya nidhamu chini ya sheria ya Utumishi wa Umma. Utaratibu hu ni mwepesi na unaweza kusimamiwa kwa haraka zaidi lakini bila ya kuathiri misingi ya Haki Asilia(Natural Justice) ya mtu kupewa haki ya kusikilizwa kwanza. Hii ni hatua muhimu sana kwani hata chini ya Mamlaka ya Rais ya kumstaafisha Mtumishi kwa manufaa ya umma, taratibu zinataka mtumishi apewe fursa ya kutoa maelezo ya kutetea kabla ya hatua yoyote kuchukuliwa. Hii inatuondolea hatari ya serikali kushtakiwa kwa kutofuata sheria, Kanuni na taratibu kama ilivyowahi kutokea huko nyuma ambapo baadhi ya viongozi na watendaji walistaafishwa kwa manufaa ya umma kimakosa, na baadaye serikali ikalazimika kuingia gharama kubwa ya kuwalipa fidia. Vilevile, hatua hii inaipa nafasi serikali kupitia utetezi utakaotolewa kuona ni watumishi gani wanaoweza kustahili kushtakiwa kwa makosa ya jinai kwa mujibu wa Sheria za Nchi.
JE, UTOH ANAKINGA YA KISHERIA??. ISEMAVYO SHERIA YA UKAGUZI WA UMMA:View attachment PUBLIC%20AUDIT%20ACT.pdf
14. Immunity from legal proceedings
No action or other proceedings shall lie against the Controller and Auditor-General or any public officer, audit firm or expert authorized by him for or in respect of the findings of any audit examination or inspection carried out by him in good faith in the exercise or purported exercise of powers under this Act.
Kwa nini sheria iweke mipaka ya kuwajibika kwa maafisa wengine tu wanaofanya kazi chini ya CAG na sio CAG mwenyewe pia??
47(2) Any staff of the National Audit Office, an auditor and an expert acting on behalf of the Controller and Auditor-General commits an offence if he-
(a) demands or takes bribe, recompense or reward for the neglect or non-performance of duty;
(b) willfully fails to report to the Controller and Auditor-General any abuse or irregularity that comes to his notice in the course of auditing duties;
(c) makes any report to the Controller and Auditor-General which he knows to be false or has no reason to believe it to be true;
(d) abuses his powers, engages in malpractices for personal gains, neglects duties or divulge State's or auditee's business secrets; or
(e) any other matter as the Controller and Auditor-General may consider an offense.
(3) When the Controller and Auditor-General has reason to believe that an offence has occurred, he shall refer the matter to the Director of Public Prosecutions for appropriate action.