Sasa hivi natarajia kurudi kazini. Je, nianzie wapi?

upeo

JF-Expert Member
Jun 10, 2013
356
207
Wakuu habari zenu,

Sasa naomba ushauri miaka mitano iliyopita, nilikuwa nafanya kazi znz serikqlini

Kwa bahati mume wangu akahamia dar kikazi.

Inabidi nimfate ..na nikaomba likizo bila malipo miaka miwili..na nikapewa
Miakq miwili kwisha nikaomba miwili mingine nikapewa baada ya miaka mengine

Miwili ikamalizika nilikwenda kuomba tena lakini safari hii wakanikatalia

Nikaambiwa chagua moja urudi kazini au andika barua ya kuacha kazi
Hapo inabidi niandike barua ya kuacha kazi shingo upande

Sasa hivi natarajia kurudi kazini je nianzie wapi?
Na je ni haki kuambiwa niwache kazi. Sheria inasemaje?

Na nini nifanye ili nirudi kazini?

Shukrani
 
Wewe unatakache ebu chagua moja kazi au mume?

Pia vipi mshahara walikua wanakuwekea kipindi chote hicho??
 
nahisi hatopendeza kusema sehemu husika
Nahitaji muongozo wa kisheria kama muajiriwa wa serikali
 
Hakuna namna ya wewe kurudi serikalini. Ulishaandika barua ya kuacha kazi mwenyewe. Imeisha hiyo, angalia utaratibu mwingine.

Eidha mume akufungulie biashara, au uombe kazi sehemu za binafsi uendelee na mambo yako. Utajipa stress na frustrations bure kuhangaika na jambo ambalo hata ufanyeje matokeo hayatabadilika. ANGALIA MAISHA MENGINE TU.
upeo
 
Hizo likizo kwa hiyo miaka yote zinanifikirisha sana,,,by the way ulishaharibu kuandika barua ya kuacha kazi,,jaribu kuwa submissive kwa kuwasiliana na crew wenzio uone kama kuna possibility hiyo coz kwa upande sheria sifahamu.
 
Nikaambiwa chagua moja urudi kazini au andika barua ya kuacha kazi
Hapo inabidi niandike barua ya kuacha kazi shingo upande

Sasa hivi natarajia kurudi kazini je nianzie wapi?

Sasa unataka kurudi kwenye kazi ipi ambayo ulishaandika barua ya kuacha kazi kwa sababu zako binafsi?

Jiajiri au kama wapenda ajira za serikali basi omba kazi kwa upya pindi nafasi zitapotangazwa...
 
Back
Top Bottom