Nanoli
JF-Expert Member
- Oct 15, 2015
- 3,739
- 5,978
Hi guys..
Kuna mambo ya kinafki kwa viongozi wa serikali hasa wale wa juu sana...
Wanapotuambia wanafanya mikutano ya serikali na sio ya kichama, ninachojua mimi ni kwamba, Mkutano huo utahudhuriwa na wananchi wote bila kujali itakadi ya vyama vyao.
Sasa inakuaje kiongozi kama Rais, Waziri mkuu na wengine wanapofanya mikutano kama hii, hutawala jezi za Chama kimoja tu, hawaoni kama wanaleta manyanyaso na ubaguzi kwa vyama vingine kuwepo katika uwanja huo?
Jambo hili pia huchangia mfalme hujisikia kama vile anaongea na wanachama wa Chama kile pekee na kusahau wengine.
Wanachama hawa watashangilia kila baya na bovu atakaloongea mwenyekiti wao ili kukilinda Chama na kupalilia mbwembwe, misifa, kejeli na mipasho kwa vyama vingine.
Mikutano mingi inapewa jina la mikutano ya serikali huku agenda zinazoongelewa ni za kichama, na mkutano kiujumla ni wa kichama... Watu wanaona, na inaumiza sana, wao wanapovunja sheria zilizowekwa kinafki na wao wenyewe, Je huu sio uchwara?
Kama wanashindwa kusimamia kile walichokisema wao wenyewe, basi wawaache na wengine wafanye.
Ipigwe marufuku mikutano ya serikali kuvaa nguo za Chama,.. Zipo nguo za bendera ya Taifa, wavae hizo.