Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 25
Mipango imeanza ya kuona uwezekano wa kuanzisha SARAFU MOJA kwa Afrika mashariki.
Mimi naona kuwa kiuchumi mpango huu si sahihi kwani nchi za Afrika mashariki bado zinatofauti kubwa sana kiuchumi.
Mpango huu utazidhoofisha nchi ambazo uchumi wao una suasua nyuma ya wenzake.
Hili mwalionaje wana JF?
Ni sahihi kufanya juhudi kufanikisha mpango huo?
Kenya itawala ile mbaya.
Sarafu moja naamini itaongeza urari wa biashara na chumi nzuri kama za kenya zinaweza kujikuta zikitetereka kwani bidhaa zao zitanunuliwa kwa bei halisi ni si kama sasa ambapo kiasi kikubwa hupotea katika exchange rates!
Mimi sioni tatizo ila tu ardhi yetu hakuna kuwapa. Biashara itakuwa nzuri na pengine kupunguza mzigo wa bei kwa watanzania maana tuna bidhaa za kenya nyingi sana hapa na wafanyabiashara wetu huwabidi kubadili T.Shs kwenda K.Shs, na shilingi yetu haiko stable inabadilikabadilika kila siku na kuwafanya wafanyabiashara kuweka faida kubwa ili kufidia pengo linalotarajiwa (ingawa wakati mwingine yaweza lisitokee)
Mnao sema sarafu moja itasaidia naomba mnielimishe mwenzenu. kwa mawazo yangu uchumi au kuongeza kipato cha taifa hakitatokana na matumizi ya sarafu moja Afrika mashariki.'''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''
Hii kitu ya sarafu moja iangaliwe kwa makini sana. Mfano mzuri tuchukulie Europian Union(EU) maana ndiyo naona watu wengi wanapenda kulinganisha jumuiya hiyo na yetu ya Africa Mashariki. Kabla ya Euro kuanza kutumiaka The Deutsche Mark (DEM, DM) ya Ujerumani ndiyo ilikuwa moja ya sarafu yenye nguvu sana ulaya na hata duniani. Sasa baada ya Euro kuingia na Ujerumani kuanza kuitumia The Deutsche Mark (DEM, DM) ikafa kabisa na sasa hivi haina nguvu ambayo ilikuwa nayo mwanzo. Great Britain wao waliona mbali zaidi na wakagoma kuadopt the Euro wakaamua kubaki na Pound(GBP). Sababu kuu ya Great Britain kukataa Euro ni kwasababu
1.Walijua Euro itaua nguvu ya Pound(GBP)
2.Wao waliichukulia sarafu yao kama nembo ya nchi yao na hawakutaka ife hivi hivi.
Sasa huu mfano wa wenzetu ni sababu tosha ya kujiuliza mara mbili mbili kabla ya kuwa na sarafu moja.
1.Je sarafu ya Tanzania itakufa kifo kama cha The Deutsche Mark (DEM, DM)? Nadhani hili swali hata wenzetu wa Kenya na Uganda wanaweza kujiuliza.
2.Je tupo tayari kuua The Tsh, Ksh na Ush kabisa kabisa in favor of the EAsh(East African shilling)?
Naombeni mtafakari hayo kwanza na atakaye kuwa tayari kutoa mawazo yake kutokana na post yangu ana karibishwa.
....jamani kama hamuelewi haya mambo ya fedha yanavyofanya kazi bora mkae kimya au mkasome kuliko kumwaga upupu wenu humu!
Hii kitu ya sarafu moja iangaliwe kwa makini sana. Mfano mzuri tuchukulie Europian Union(EU) maana ndiyo naona watu wengi wanapenda kulinganisha jumuiya hiyo na yetu ya Africa Mashariki. Kabla ya Euro kuanza kutumiaka The Deutsche Mark (DEM, DM) ya Ujerumani ndiyo ilikuwa moja ya sarafu yenye nguvu sana ulaya na hata duniani. Sasa baada ya Euro kuingia na Ujerumani kuanza kuitumia The Deutsche Mark (DEM, DM) ikafa kabisa na sasa hivi haina nguvu ambayo ilikuwa nayo mwanzo. Great Britain wao waliona mbali zaidi na wakagoma kuadopt the Euro wakaamua kubaki na Pound(GBP). Sababu kuu ya Great Britain kukataa Euro ni kwasababu
1.Walijua Euro itaua nguvu ya Pound(GBP)
2.Wao waliichukulia sarafu yao kama nembo ya nchi yao na hawakutaka ife hivi hivi.
Sasa huu mfano wa wenzetu ni sababu tosha ya kujiuliza mara mbili mbili kabla ya kuwa na sarafu moja.
1.Je sarafu ya Tanzania itakufa kifo kama cha The Deutsche Mark (DEM, DM)? Nadhani hili swali hata wenzetu wa Kenya na Uganda wanaweza kujiuliza.
2.Je tupo tayari kuua The Tsh, Ksh na Ush kabisa kabisa in favor of the EAsh(East African shilling)?
Naombeni mtafakari hayo kwanza na atakaye kuwa tayari kutoa mawazo yake kutokana na post yangu ana karibishwa.
Hi Nono,Fedha ni kwa ajili ya kubadilishana bidhaa tu, kwa hiyo swala eti tukotayari kuziacha shilingi za nchi husika zife halina msingi. Kuwa na sarafu moja ni kushiriki uchumi mmoja na kuwa na wigo mpana wa bishara, badala ya Tsh kwa watu milioni 40, tunatumia Esh kwa zaidi ya watu milioni 100, soko ni kubwa hilo. Wezetu wa afrika magharibi wamekuwa na sarafu moja ambayo wameweza kuifanya kuwa stable sana kwa muda mrefu. Shilingi ya Tz haina maana yoyote kabisa, wakati mkapa anaingia madarakani ilikuwa kama 500 kwa dola moja leo ni kariabia 1400. Tuendelee kuing'an'ania? tuendelee kung'ng'ania kufunga milango yetu? Lets face reality, maybe our way of thinking and acting will change.
Hoja yako nzuri lakini nadhani kuna kona moja itakuwa na manufaa kwa bashara ya nchi husika. Unavyonunua fedha ya kigeni kuna bid-ask spread. Sasa kama nchi hizi zitatumia fedha moja, inamaana hakuna pesa itayopotea kwenye hiyo bid-ask spread yaani bei ya kuuza na ya kununua. Hiyo ni faida mojawapo, kwa mtindo huo inamaana bei ya bidhaa zitaenda chini maana kutakuwa hamna cmpensation ya exchange rate loss. Sasa basi hii inaenda sehem kubwa zaidi mpaka kwenye financial markets huko wanauza shares na bonds nazo zitauzwa kwa pesa moja na kutakuwa na interaction kubwa ya soko. Na ndio issue ya One pricing itaapply. Inamaana hata wateja watakuwa na choice nyingi zaidi ultimately demand na supply itakuwa sawa sokoni.Hii kitu ya sarafu moja iangaliwe kwa makini sana. Mfano mzuri tuchukulie Europian Union(EU) maana ndiyo naona watu wengi wanapenda kulinganisha jumuiya hiyo na yetu ya Africa Mashariki. Kabla ya Euro kuanza kutumiaka The Deutsche Mark (DEM, DM) ya Ujerumani ndiyo ilikuwa moja ya sarafu yenye nguvu sana ulaya na hata duniani. Sasa baada ya Euro kuingia na Ujerumani kuanza kuitumia The Deutsche Mark (DEM, DM) ikafa kabisa na sasa hivi haina nguvu ambayo ilikuwa nayo mwanzo. Great Britain wao waliona mbali zaidi na wakagoma kuadopt the Euro wakaamua kubaki na Pound(GBP). Sababu kuu ya Great Britain kukataa Euro ni kwasababu
1.Walijua Euro itaua nguvu ya Pound(GBP)
2.Wao waliichukulia sarafu yao kama nembo ya nchi yao na hawakutaka ife hivi hivi.
Sasa huu mfano wa wenzetu ni sababu tosha ya kujiuliza mara mbili mbili kabla ya kuwa na sarafu moja.
1.Je sarafu ya Tanzania itakufa kifo kama cha The Deutsche Mark (DEM, DM)? Nadhani hili swali hata wenzetu wa Kenya na Uganda wanaweza kujiuliza.
2.Je tupo tayari kuua The Tsh, Ksh na Ush kabisa kabisa in favor of the EAsh(East African shilling)?
Naombeni mtafakari hayo kwanza na atakaye kuwa tayari kutoa mawazo yake kutokana na post yangu ana karibishwa.
Hoja yako nzuri lakini nadhani kuna kona moja itakuwa na manufaa kwa bashara ya nchi husika. Unavyonunua fedha ya kigeni kuna bid-ask spread. Sasa kama nchi hizi zitatumia fedha moja, inamaana hakuna pesa itayopotea kwenye hiyo bid-ask spread yaani bei ya kuuza na ya kununua. Hiyo ni faida mojawapo, kwa mtindo huo inamaana bei ya bidhaa zitaenda chini maana kutakuwa hamna cmpensation ya exchange rate loss. Sasa basi hii inaenda sehem kubwa zaidi mpaka kwenye financial markets huko wanauza shares na bonds nazo zitauzwa kwa pesa moja na kutakuwa na interaction kubwa ya soko. Na ndio issue ya One pricing itaapply. Inamaana hata wateja watakuwa na choice nyingi zaidi ultimately demand na supply itakuwa sawa sokoni.
Hilo la GBP, ukweli mie huwa naoa uamuzi wa UIngereza ulikuwa na kasoro. Kama utakumbuka mwezi January wakati uchumi wa UIngereza umekamatwa vilivyo, ratio ya GBP na EURO ilikaribia one to one. Au ukirejea report ya recession ya European union, utaona giant nations in Europe, yaani German na France zimeanza kutoka kwenye recession wakati UK ipo deep kwenye recession. Sasa bado siioni kama GBP ni stronger currency anymore, soon or later itazama. Kifupi UK haitaweza kushindana na EMU, soon utaona kitakachowakumba