Sarafu Moja Afrika Mashariki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sarafu Moja Afrika Mashariki?

Discussion in 'International Forum' started by Exaud J. Makyao, May 29, 2009.

 1. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mipango imeanza ya kuona uwezekano wa kuanzisha SARAFU MOJA kwa Afrika mashariki.
  Mimi naona kuwa kiuchumi mpango huu si sahihi kwani nchi za Afrika mashariki bado zinatofauti kubwa sana kiuchumi.
  Mpango huu utazidhoofisha nchi ambazo uchumi wao una suasua nyuma ya wenzake.
  Hili mwalionaje wana JF?
  Ni sahihi kufanya juhudi kufanikisha mpango huo?

  [​IMG]
   
 2. I

  Idda Member

  #2
  May 29, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kenya itawala ile mbaya.
   
  Last edited by a moderator: May 31, 2009
 3. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Why, why, why again.
   
 4. J

  Jobo JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sarafu moja naamini itaongeza urari wa biashara na chumi nzuri kama za kenya zinaweza kujikuta zikitetereka kwani bidhaa zao zitanunuliwa kwa bei halisi ni si kama sasa ambapo kiasi kikubwa hupotea katika exchange rates!
   
 5. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  JOBO.
  Unamaanisha nini unaposema kuwa uchumi mzuri unaweza kutetereka kwa kuanzishwa kwa sarafu moja?
  Je si kinyume chake?
   
 6. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mimi sioni tatizo ila tu ardhi yetu hakuna kuwapa. Biashara itakuwa nzuri na pengine kupunguza mzigo wa bei kwa watanzania maana tuna bidhaa za kenya nyingi sana hapa na wafanyabiashara wetu huwabidi kubadili T.Shs kwenda K.Shs, na shilingi yetu haiko stable inabadilikabadilika kila siku na kuwafanya wafanyabiashara kuweka faida kubwa ili kufidia pengo linalotarajiwa (ingawa wakati mwingine yaweza lisitokee)
   
 7. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sarafu moja ya Africa mashariki haitabadilisha chochote. Si itawekwa viwango vyake vya exchange rate! Itakuwa kama ilivyo sasa inavyotumika Dollar na pesa zetu. Au pesa za nchi zetu zitafutwa kabisa?
   
 8. Margwe

  Margwe JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Binafsi kitu chochote na Kenya nawatch with maximum suspicion!
   
 9. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  single currency is good for the region!

  Angalia Euro ilivyo na nguvu ukilinganisha na Paundi au Dola
   
 10. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Evidence of Paranoia. We are talking about a single currency for the EA community, wewe bado washikilia mambo ya mashamba. LOL.. A Single currency would have a big impact on the business community whereas buying and selling goods on the EA market would be simplified ten folds. The only people who would suffer are the money dealers who deal with the local currencies.

  Though the issue has a lot of positive effects, I dont see it coming any day soon. We still have a long way to go in the EAC, lazima haya maneno yajadiliwe sana, they weigh the pros and cons, so that they can make a final conclusion (benefitial to all countries involved), because as benefitial as it is there are parties which will be adversely affected by the desicion to use a single currency for the whole of EA.
   
 11. m

  mahiya Member

  #11
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnao sema sarafu moja itasaidia naomba mnielimishe mwenzenu. kwa mawazo yangu uchumi au kuongeza kipato cha taifa hakitatokana na matumizi ya sarafu moja Afrika mashariki.Kama unazalisha kitu chenye kuuzika kwa wingi hata sasa hivi utapata fedha nyingi tu za kenya, Tanzania na uganda na za nje ya east Afrika.
  Afrika mashariki wakati huo kenya,Uganda na Tanzania ilisha wahi kuwa na sarafu moja na bado nianavyo mimi haikusaidia sana kukuza uchumi wa kila nchi kwa usawa kwa wanao sema itasaidia urari (balance of Trade ) wa biashara si kweli kwani kwani urari unategemea uwingi na thamani ya bidhaa ulizo uza nje na ulizo nunua toka nje siyo fedha moja, Kenya watauza bidhaa zao,Tanzania zao Uganda zao,Rwanda na Burundi za kwao na usfikiri pamoja na kutumia sarafu moja basi na bei ya vitu vinavyo fanana mfano Ugali Maharage Tanzania itakuwa bei moja na Kenya Uganda na nchi nyingine zitakazo tumia sarafu hiyo.Hiyo itarahisha tu kuondoa usumbufu wa ubadilishaji fedha mpakani au bank ambapo kuna Biashara inayo chukua fedha za bure kwa wahitaji kwani kuna Gains in exchange rate na si urari wa biashara nionavyo mimi Mahiya by
   
 12. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wana jamii kama FELISTER n.k,
  Bado MAHIYA hajapatiwa ufafanuzi wa swali lake.
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hii kitu ya sarafu moja iangaliwe kwa makini sana. Mfano mzuri tuchukulie Europian Union(EU) maana ndiyo naona watu wengi wanapenda kulinganisha jumuiya hiyo na yetu ya Africa Mashariki. Kabla ya Euro kuanza kutumiaka The Deutsche Mark (DEM, DM) ya Ujerumani ndiyo ilikuwa moja ya sarafu yenye nguvu sana ulaya na hata duniani. Sasa baada ya Euro kuingia na Ujerumani kuanza kuitumia The Deutsche Mark (DEM, DM) ikafa kabisa na sasa hivi haina nguvu ambayo ilikuwa nayo mwanzo. Great Britain wao waliona mbali zaidi na wakagoma kuadopt the Euro wakaamua kubaki na Pound(GBP). Sababu kuu ya Great Britain kukataa Euro ni kwasababu
  1.Walijua Euro itaua nguvu ya Pound(GBP)
  2.Wao waliichukulia sarafu yao kama nembo ya nchi yao na hawakutaka ife hivi hivi.

  Sasa huu mfano wa wenzetu ni sababu tosha ya kujiuliza mara mbili mbili kabla ya kuwa na sarafu moja.
  1.Je sarafu ya Tanzania itakufa kifo kama cha The Deutsche Mark (DEM, DM)? Nadhani hili swali hata wenzetu wa Kenya na Uganda wanaweza kujiuliza.

  2.Je tupo tayari kuua The Tsh, Ksh na Ush kabisa kabisa in favor of the EAsh(East African shilling)?

  Naombeni mtafakari hayo kwanza na atakaye kuwa tayari kutoa mawazo yake kutokana na post yangu ana karibishwa.
   
 14. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MWANAFALSAFA1,
  Mawazo yako ni changamoto kubwa kwa wanauchumi.
  Naamini katika michango yetu, tutazingatia challenge uliyotoa.
   
 15. K

  Koba JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ....jamani kama hamuelewi haya mambo ya fedha yanavyofanya kazi bora mkae kimya au mkasome kuliko kumwaga upupu wenu humu!
   
 16. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Toa elimu mkuu
   
 17. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Fedha ni kwa ajili ya kubadilishana bidhaa tu, kwa hiyo swala eti tukotayari kuziacha shilingi za nchi husika zife halina msingi. Kuwa na sarafu moja ni kushiriki uchumi mmoja na kuwa na wigo mpana wa bishara, badala ya Tsh kwa watu milioni 40, tunatumia Esh kwa zaidi ya watu milioni 100, soko ni kubwa hilo. Wezetu wa afrika magharibi wamekuwa na sarafu moja ambayo wameweza kuifanya kuwa stable sana kwa muda mrefu. Shilingi ya Tz haina maana yoyote kabisa, wakati mkapa anaingia madarakani ilikuwa kama 500 kwa dola moja leo ni kariabia 1400. Tuendelee kuing'an'ania? tuendelee kung'ng'ania kufunga milango yetu? Lets face reality, maybe our way of thinking and acting will change.
   
 18. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Hi Nono,
  I think the same applies to land.
   
 19. b

  bnhai JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Hoja yako nzuri lakini nadhani kuna kona moja itakuwa na manufaa kwa bashara ya nchi husika. Unavyonunua fedha ya kigeni kuna bid-ask spread. Sasa kama nchi hizi zitatumia fedha moja, inamaana hakuna pesa itayopotea kwenye hiyo bid-ask spread yaani bei ya kuuza na ya kununua. Hiyo ni faida mojawapo, kwa mtindo huo inamaana bei ya bidhaa zitaenda chini maana kutakuwa hamna cmpensation ya exchange rate loss. Sasa basi hii inaenda sehem kubwa zaidi mpaka kwenye financial markets huko wanauza shares na bonds nazo zitauzwa kwa pesa moja na kutakuwa na interaction kubwa ya soko. Na ndio issue ya One pricing itaapply. Inamaana hata wateja watakuwa na choice nyingi zaidi ultimately demand na supply itakuwa sawa sokoni.
  Hilo la GBP, ukweli mie huwa naoa uamuzi wa UIngereza ulikuwa na kasoro. Kama utakumbuka mwezi January wakati uchumi wa UIngereza umekamatwa vilivyo, ratio ya GBP na EURO ilikaribia one to one. Au ukirejea report ya recession ya European union, utaona giant nations in Europe, yaani German na France zimeanza kutoka kwenye recession wakati UK ipo deep kwenye recession. Sasa bado siioni kama GBP ni stronger currency anymore, soon or later itazama. Kifupi UK haitaweza kushindana na EMU, soon utaona kitakachowakumba
   
 20. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mawazo mazuri.
  Naamini wachambuzi wa masuala ya uchumi watakuwa na neno la kusema.
  Hata hivyo utabiri wa kuanguka kwa GBP utategemea sana athari zitakazo tokana na juhudi za kuchochea uchumi zianazofanywa na Uingereza na mataifa yale yenye strong Economies.
   
Loading...