Sappi yuko sahihi kuhusu uwezo wa Maximo?

Hapo tulipofika si haba Mahmoud Qassim.Juhudi zote zilizofanywa na kila mmoja wetu zimetufikisha hapa.Kama tuaendelea na kufika tunakotaka kufika ni bora kwetu sote,Maximo akwemo ndani.

Katika uchambuzi mwingi wengi wetu tumesahu kuwa Brazil ni nchi inayoheshimika kwa soka na imechukua kombe la dunia mara nyingi.Sikumbuki mahali mabapo kocha wa Brazil alikuwa foreigner!

Je tungempa Charles Boniface Mkwasa timu hii angeweza kutufikisha hapo tulipofika? I doubt kwa sababu kuna tofauti kati ya Mkwasa na Maximo! That's what makes the difference!Hii ni pamoja na all the support rendered!JK hakuwa na mawazo ya Mkwasa wala Mziray kwa sababu alijua what the team needed most.

Hata kama tutafungwa au kufunga leo hii kauli yangu ni hii,kwamba tumejitahidi na tumefanya vizuri kwa sababu tuna Coach mzuri plus the support of the whole nation.
 
ni sawa kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni ili mradi havunji sheria,lakini yasiwe maoni ya kiwendaazimu kama ya sapi.ameamua kupayuka bila kutoa mtizamo wa kiufundi,lazma tukubali maximo amerudisha kwa kiasi fulani heshima ya tanzania kisoka
 
Hapo tulipofika si haba Mahmoud Qassim.Juhudi zote zilizofanywa na kila mmoja wetu zimetufikisha hapa.Kama tuaendelea na kufika tunakotaka kufika ni bora kwetu sote,Maximo akwemo ndani.

Katika uchambuzi mwingi wengi wetu tumesahu kuwa Brazil ni nchi inayoheshimika kwa soka na imechukua kombe la dunia mara nyingi.Sikumbuki mahali mabapo kocha wa Brazil alikuwa foreigner!

Je tungempa Charles Boniface Mkwasa timu hii angeweza kutufikisha hapo tulipofika? I doubt kwa sababu kuna tofauti kati ya Mkwasa na Maximo! That's what makes the difference!Hii ni pamoja na all the support rendered!JK hakuwa na mawazo ya Mkwasa wala Mziray kwa sababu alijua what the team needed most.

Hata kama tutafungwa au kufunga leo hii kauli yangu ni hii,kwamba tumejitahidi na tumefanya vizuri kwa sababu tuna Coach mzuri plus the support of the whole nation.

Ndugu yangu Alnadaby, nimekusoma vizuri, fikra yako ndio fikra ya waTanzania walio wengi. lakini pia japo si support Makocha wazalendo (sababu ziko wazi, si rahisi tukampa heshima na support tunazowapa Wageni) si Mkwasa peke yake bali kuna makocha wazalendo wengi wangeweza kutupeleka hata Kombe la Mataifa ya Afrika achilia mbali huko Ivory Coast, lakini kwa kuwa haijawa tunaongelea kufikirika tu. wapo wengi wanamzidi Maximo ila hatutawapa support ya kutosha sasa kama ni hivyo Bora kocha wa kigeni aje, ama hata wampe nafasi hiyo Tinoco namuona anauwezo zaidi ya Maximo. si mchukii maximo kwanza ni rafiki yangu huwa anakuja ofisini kwangu japo si mara kwa mara. amewahi kufika kama mara nne tano hivi mwaka jana, na huwa namwambia kwamba sina imani hasa na Upangaji wake wa timu hasa first 11 na substitute, lakini hupinga mawazo yangu na tunaishia hivyo.
Maximo huwa anaogopa mechi ngumu anakuwa na presure sana, kumbuka burkina faso tulipowafunga kwao, ni baada ya yeye kwenda jukwaani kwa kadi na Ali bushiri kuongoza jahazi la ufundi, Bushiri alimuingiza Forward na kupunguza defence wakati tukiwa tayari Nsajigwa ashatolewa kwa kadi nyekundu, Maximo anawaza sana Defensive kuliko Offensive.
Kumbuka mechi na Kameroon hapa Dar, ile mechi tungeweza kushinda kama asingemtoa Chuji, Chuji alianza kuona njia za kuwapiata Kameroon akaanza kupandisha mashambulizi mbele kupitia hizo njia sisi wengine tukaanza kupata matumaini kwa sasa mambo yatakuwa mazuri, badala yake Maximo kwa kuogopa kwamba Kameroona watatumia nafasi ya Chuji kwenda mbele nao kupata nafasi ya kutushambulia akamtoa kwamba atia anavuruga mfumo wake. ni kweli lakini mara nyingine ili kushinda lazima ku risk. usiogope kufungwa ati ni bora usifunge kuliko kufungwa ukijaribu kufunga. ati ni sifa kupata Droo na Kameroon kuliko kufungwa kwa kujaribu kwetu kutafuta bao. hizi fikra mbaya sana.
 
Well done Taifa stars and pole for a very unfortunate goal conceded @ last minute; nevertheless, Maximo has reached his peak and no more to offer... The game mentality and defensive mind speaks it all
 
Kweli kuwa MAXIMO anapenda fomesheni ya ku-defence zaidi
 
Ama kweli waTanzania ni hodari kwa kupenda maendeleo ya haraka bila ya kuwekeza. Hivi kweli mnaweza kumlaumu Maximo kwa haya maendeleo "madogo" tuliyonayo kwenye soka?
Unapolinganisha soka ya Tanzania na ulaya hautendi haki. Ulaya wenzenu wanaanza kupikwa toka wakiwa wadogo. Kuna shule kibao za soka ambazo zinawafundisha watoto. Hao akina lampard, Torres na wakali wengineo wamepikwa kisoka toka wakiwa wadogo. Hebu angalia hapa TZ nini kinaendelea. Watu mpira wanafundishwa "ukubwani". Wakiwa wadogo na hata mchangani wanacheza mpira wakufundishwa na "kocha mbabaishaji" tu. Unategemea mtu kama huyo hata akikuwa atajua soka kweli?

Tufike mahala tukubali kuwa ili kuwa na timu nzuri basi inabidi kwanza mfumo wa soka ubadilike. Timu zianze kutengenezwa toka za watoto. Wapate makocha wenye taaluma ya ukocha wawajengee misingi mizuri then wakiwa wakubwa matunda yao yataonekana.

UBORA WA NYUMBA UNATEGEMEA MSINGI WAKE

Haya maneno uliyosema ni sahihi sana. na kwa usahihi wake ndo maana tulitarajia kwamba, kama umepata fundi mzuri halafu akakukuta ulishatengeneza msingi mbovu, anatakiwa asiendelee na ujenzi bali akushauri ipasavyo hata kama italazimu kuvunja na kuanza kuchimba msingi upya.

Sasa ukitaka kujua kwamba Maximo hana weledi katika soka ni pale aliposhindwa hata kumsamehe Juma Kaseja, Kipa anayeaminika kuwa bora hapa Tanzania kwa miaka zaidi ya mitatu sasa. Matokeo yake tunafungwa magoli ya kijingakijinga tu. Iwapo Kaseja pekee ndiyo Maximo alimwona na kumhukumu kuwa hana nidhamu, iweje tena hawa vipenzi wake wamechemsha halafu anasingizia kuwa hakukuwa na nidhamu. Aende zake huyu, kazi kutulia fweza zetu bure tu.
 
Kweli kuwa MAXIMO anapenda fomesheni ya ku-defence zaidi

Kocha anakuwa na mbinu nyingi za kukabiliana na timu pinzani. Lakini mbinu zote zinatokana na uwezo wa wachezaji alionao. Mpaka leo Taifa stars haijapata washambuliaji agressive kama kina Abeid Mziba, Makumbi Juma, Mtemi Ramadhani na wenye maumbo na kutoa changamoto kwa mabeki kama hao. Ukiangalia maumbo ya wachezaji wetu wa leo utaona kuwa wengi wana maumbo madogo na hawawezi kukabiliana na walinzi na viungo walinzi wenye maumbo makubwa.

Hii ni layman observation ambayo hata Sappi hakuiona, yeye ameshindwa kuona kuwa kuna tatizo fulani kwenye wachezaji wetu, na ndio maana mpaka sasa bado MAXIMO hajaweza kupata kikosi cha wachezaji 11, bado anahaingaika kupata perfect players.

Mara nyingi ukiangalia mpira utaona kuna mbinu nyingi za kudefend. Kama unaona timu yako dhaifu basi inabidi utumie wachezaji wenye uwezo kushambulia kwa nguvu, sisi bado hatuna wachezaji hao, sio kosa la maximo. Options alizo nazo ndio zimemfiksha hapo, kuna uwezekano angefika mbali zaidi.

By the way, ule mchezo wa kununua marefa na kuhonga vibendera tumeacha? au ndio bado unaendelea, inaonekana sasa hivi tumeanza kuongoza kwenye mambo ya ushirikina na kuhonga. Bado kuna wanaodhani kuwa timu tunaweza kushinda kwa namna hiyo. Nakumbuka Victor alipoondoka alisema amefurahishwa zaidi na Jujuman wa timu ya taifa aliyetulostisha Sudan, na aliisambaza vilivyo story hiyo lakini mpaka leo hiyo juju haijatusaidia kuliko alivyoweza maximo.
 
watu kwa Maximo ni kipofu aliyeona Mwezi. hatusemi Maximo hajafanya chochote, ila alichofanya hakilingani na alivyopaswa ikizingatiwa na support aliyopewa.

Hakuna kocha yeyote wakati wowote Tangu uhuru aliyewahi kupata support anayoendelea kupata Maximo, hibyo sio kipimo kumfananisha na mwingine yeyote kwa Mafanikio.
 
Ngoja mtamsikia akija na Tathmini zake za we played 3 games, we lost one, we drew one and we won one. na tutafurahia sana tathmini hiyo.
 
Mategemeo yote yanapokuwa kwako wewe mtu mmoja Maximo kutuvusha hadi kwenye zabibu na asali na ukashindwa kufanya hivyo,ni dhahiri hasira zitakuwa juu yako!

Saikolojia ya jinsi hii imewakumba kina Scolari na wengineo na nadhani sasa kuna haja ya kuangalia mbele!

Lakini ukishafunga virago vyako historia inabaki pale pale.Alifundisha Taifa Stars hadi final za CHAN,alifungwa 1-0 na Senegal,akawatoa wenyeji Ivory Coast 1-0 na kwenda sare 1-1 na Zambia katika mechi ambayo alikuwa akiongoza hadi dk ya 93.

Thats the truth!
 
unajua Mwanadamu unatakiwa kwanza ukubali kwamba sisi wanadamu tunatofautiana sana kwa kila hali, pili kila mmoja anao uwezo wake wa kipekee ambao mwingine hana, tatu kutokana na hayo mawili ya juu, basi fikra mitazamo, upeo na uelewa lazima vote hivyo viwe tofauti. sasa mtu unapolazimisha fikra yako iwe ndio sahihi kuliko mwenzio ni vizuri ulete hoja zenye ushahidi kuitia nguvu fikra yako.
Mimi kwa fikra yangu Mashindano ya CHAN ni mashindano ambayo yalipaswa kutawaliwa na Timu za kutoka ukanda huu, tena kwa bahati nzuri timu zote nne za ukanda huu zinapakata zote. na nilitegemea zote nne ziingie nusu fainali, na zile za magharibi ziage mapema kwasababu sisi timu zetu zote hakuna ambayo inafikisha 75% katika Timu za Taifa za jumla(yaani Zenye professional na non professional player) kwa hivyo timu hizi ni zilezile zilizokuwa katika CAN na world cup qualifiers sasa kama timu ni zilezile kwa asilimia 75 maana yake ni kwamba tunakuwa na uzowefu wa kutosha, wachezaji wamekuwa pamoja kwa muda mrefu ni walewale kwa asilimia 75% japo Taifa Stars ni asilimia 100%. sikutegemea kwenda kufungwa na timu ngeni kabisa kwani kwa timu za magharibi wao timu zao hutegemea wachezaji wa nje kwa asilimia 100%.
 
Kuwa soccer analyst sio lazima uende shule ya soka…ni kama vile kuwa Kocha wa soka si lazima uwe ulicheza mpira zamani… ingawa kuna faida ya kukijua kitu ndani nje.

Maximo ni kocha mzuri, na ametufikisha sehemu nzuri… tunakubali. Lakini je, tunapenda haya mafanikio nusunusu?

Hivi nyie mnaosema Maximo aendelee, huwa mnakwenda kuiona Taifa stars ikicheza uwanja wa Taifa… au hata kuiona kwenye TV?

Uwezo wa Maximo tuuangalie zaidi kwa mbinu za wachezaji uwanjani. Kwakweli uwezo wa timu yetu kubadilisha mchezo uwanjani ni mdogo mno… na hilo ni jukumu la Kocha. Kocha huyu, mbrazili Marcio Maximo ameshindwa kabisa. Kumbukeni kwenye mechi yetu ya CAN qualifying dhidi ya Mauritius. Jamaa wa Mauritius hawakuwa na uwezo wowote uwanjani… nasi tulikosa mbinu za kuwafunga licha ya kuhemea lango lao na kupata kona zaidi ya 17. yaani hatukuweza kubadilisha mchezo na tukaishia kwa sare pale national stadium. Licha ya wao kucheza pungufu ya mtu mmoja kwa muda mwingi wa mchezo.

Maximo ameshindwa kutengeneza nguvu ya timu pale tunapopata goli kabla ya wapinzani wetu… hakika hatuwezi kulinda goli kabisa. Na hilo ni jukumu la kocha. Kumbuka mechi kati ya Taifa Stars na Senegal pale Kirumba Mwanza(1:1); Taifa stars na Cameroun pale Yaounde (1:2), lile bao la pili la Cameroun ni upuzi mtupu. Taifa Stars na Ghana hapa Dar(1:1), na sasa Taifa stars dhidi ya Zambia(1:1). Hiyo ni kazi ya kocha ambayo ameshindwa kuifanya kwa muda mrefu kabisa. Timu haiwezi kulinda bao chini ya ukocha wake.

Mafanikio haya tunayoyaona ni mafanikio ya kimorari. Watanzania tuna Morari na wachezaji pia. Kipindi hiki cha Maximo, timu inapata kila kitu… fedha, muda, vifaa vya mazoezi n.k. Hivi mnakumbuka Kocha Zakaria kinanda au Mshindo Msolwa walikuwa wanapewa timu wiki moja kabla ya mashindano? Mnakumbuka wachezaji wa taifa kambi yao ilikuwa jeshi la Wokovu pale Kurasini? Hakukuwa na Morari kabisa.

Hivyo kwa sapoti hii anayopewa Maximo akipewa Kocha kama King Kibadeni au Mziray anaweza kufanya makubwa zaidi. Maximo na aondoke tu!!! Hana jipya, uwezo wake umefikia kikomo.

Kumbukeni Simba ilipokuwa na sapoti ilifika fainali kombe la CAF (1993) chini ya kocha mzalendo.

Tunahitaji kocha mpya Tanzania ambaye ataanzia pale Maximo alipoishia.
 
Maximo wachezaji wake Chuji, Boban wageuka paka na panya
Na Saleh Ally, Abidjan

UNAWEZA ukadhani ni masihala, lakini hiyo ndio hali halisi namna kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo na wachezaji wake wawili nyota, Athuman Idd 'Chuji' na Haruna Moshi 'Boban' wanavyopishana au kupigana chenga kila wanapokutana.

Maximo hana tena mahusiano mazuri na wachezaji hao, hajazungumza hata mara moja uso kwa uso kwa zaidi ya siku tano, jambo linalotokea hapa ni kwa kila mmoja amekuwa akipita upande wake inapotokea wamekutana.

Maximo hataki kabisa kuwaangalia usoni wachezaji hao, ingawa nao wamekuwa wakifanya hivyo hivyo huku wakiishi kama wakimbizi.

Imeelezwa kocha huyo amekataa usuluhishi wake ulishafika kwa Waziri Seif Khatib aliyeamua kuingilia kati na kuzuia uamuzi wa Maximo kutaka kuwarudisha wachezaji hao Dar es Salaam.

Chuji na Boban wameithibitishia Mwananchi kwamba wamekuwa wakikwepana na kocha wao ingawa walisisitiza yeye ndiye amekuwa akifanya hivyo.

''Kwanza hatusalimiani kabisa, ukikutana na kocha anaangalia pembeni kabisa. Mwanzo tulikuwa tunamsalimia, lakini sasa hivi tumeacha maana hajibu,' anasema Chuji huku Boban akiongeza, ''Maisha huku Ivory Coast yalikuwa ni magumu sana, acha ifike siku turejee nyumbani kaka.''

Mwananchi ilimfuata Maximo kwa mara nyingine ikiwa ni zaidi ya mara tatu kuliulizia na kutaka kujua kuhusu tatizo kati yake na wachezaji hao.

''Nimesema mara kadhaa napenda kuzungumzia timu na wala si mtu mmoja mmoja, lakini kama mtu hafuati taratibu, hasikilizi kinachoelezwa mimi nalazimika kumbembeleza au natakiwa nifuate yeye anavyosema. Kazi yangu ni masuala ya ufundi na nina vijana wengi ambao inabidi nifanye nao kazi na si watu wawili, tafadhari nielewe,' alisema.

Juzi baada ya timu hiyo kuwasili Yamoussoukro ikitokea kwenye mji wa Bouake ambako ilienda kucheza na Zambia, Maximo aliwataka wote ambao hawakucheza wala kuwa kwenye benchi kuteremka kwenye basi hilo.

Chuji, Boban na Amir Maftah ambaye pia ameingia kwenye sekeseke na Maximo kutokana na kuwa na urafiki na wachezaji hao wawili walilazimika kuteremka na kumuacha Mbrazil huyo akizungumza na wachezaji wengine na benchi la ufundi akiwaeleza mambo kadhaa baada ya kupoteza mechi hiyo muhimu kwa kutoka sare na Zambia.

Hali ya maelewano kati ya Maximo na vijana wake hao wawili imezidi kudorora kwa kiasi kikubwa na kufanya malumbano na mijadala kuzuka kwa kuna kundi linalowatetea wachezaji hao na wale wanaomtetea kocha huyo.

Taifa Stars imeendoka leo hapa mjini Abidjan inategemewa kuwasiri Tanzania kesho asubuhi.

Source: Gazeti la Mwananchi
 
I think Maximo should go now...Tunahitaji ujuzi wa Kocha mwingine,hasa kutoka Ufaransa,makocha wa kifaransa wana uzoefu sana na soka la Afrika,pia watatusaidia kuwauza wachezaji wetu Ufaransa,otherwise daima tutakuwa wasindikizaji tu huku tukijisifia tumecheza vizuri(ilhali tumetolewa)....Hivi mkataba wake unaisha lini????
 
Hata akiondoka na hao jamaa waache kuvuta bangi bila hivyo hata aikja kocha gani mambo ni yaleyale
 
I think Maximo should go now...Tunahitaji ujuzi wa Kocha mwingine,hasa kutoka Ufaransa,makocha wa kifaransa wana uzoefu sana na soka la Afrika,pia watatusaidia kuwauza wachezaji wetu Ufaransa,otherwise daima tutakuwa wasindikizaji tu huku tukijisifia tumecheza vizuri(ilhali tumetolewa)....Hivi mkataba wake unaisha lini????

Mkuu Balantanda, mkataba wa Maximo utaisha July. Lakini yeye alianza sema ataondoka manake kuna timu zinamtaka. Baya anampigia debe Kocha mkuu wa timu za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 17 na 20, mbrazil mwenzake, Marcos Tinoco. Hatakiwi kuingilia mchakato wa kutafuta kocha mpya.
 
Kuwa soccer analyst sio lazima uende shule ya soka…ni kama vile kuwa Kocha wa soka si lazima uwe ulicheza mpira zamani… ingawa kuna faida ya kukijua kitu ndani nje.

Maximo ni kocha mzuri, na ametufikisha sehemu nzuri… tunakubali. Lakini je, tunapenda haya mafanikio nusunusu?

Hivi nyie mnaosema Maximo aendelee, huwa mnakwenda kuiona Taifa stars ikicheza uwanja wa Taifa… au hata kuiona kwenye TV?

Uwezo wa Maximo tuuangalie zaidi kwa mbinu za wachezaji uwanjani. Kwakweli uwezo wa timu yetu kubadilisha mchezo uwanjani ni mdogo mno… na hilo ni jukumu la Kocha. Kocha huyu, mbrazili Marcio Maximo ameshindwa kabisa. Kumbukeni kwenye mechi yetu ya CAN qualifying dhidi ya Mauritius. Jamaa wa Mauritius hawakuwa na uwezo wowote uwanjani… nasi tulikosa mbinu za kuwafunga licha ya kuhemea lango lao na kupata kona zaidi ya 17. yaani hatukuweza kubadilisha mchezo na tukaishia kwa sare pale national stadium. Licha ya wao kucheza pungufu ya mtu mmoja kwa muda mwingi wa mchezo.

Maximo ameshindwa kutengeneza nguvu ya timu pale tunapopata goli kabla ya wapinzani wetu… hakika hatuwezi kulinda goli kabisa. Na hilo ni jukumu la kocha. Kumbuka mechi kati ya Taifa Stars na Senegal pale Kirumba Mwanza(1:1); Taifa stars na Cameroun pale Yaounde (1:2), lile bao la pili la Cameroun ni upuzi mtupu. Taifa Stars na Ghana hapa Dar(1:1), na sasa Taifa stars dhidi ya Zambia(1:1). Hiyo ni kazi ya kocha ambayo ameshindwa kuifanya kwa muda mrefu kabisa. Timu haiwezi kulinda bao chini ya ukocha wake.

Mafanikio haya tunayoyaona ni mafanikio ya kimorari. Watanzania tuna Morari na wachezaji pia. Kipindi hiki cha Maximo, timu inapata kila kitu… fedha, muda, vifaa vya mazoezi n.k. Hivi mnakumbuka Kocha Zakaria kinanda au Mshindo Msolwa walikuwa wanapewa timu wiki moja kabla ya mashindano? Mnakumbuka wachezaji wa taifa kambi yao ilikuwa jeshi la Wokovu pale Kurasini? Hakukuwa na Morari kabisa.

Hivyo kwa sapoti hii anayopewa Maximo akipewa Kocha kama King Kibadeni au Mziray anaweza kufanya makubwa zaidi. Maximo na aondoke tu!!! Hana jipya, uwezo wake umefikia kikomo.

Kumbukeni Simba ilipokuwa na sapoti ilifika fainali kombe la CAF (1993) chini ya kocha mzalendo.

Tunahitaji kocha mpya Tanzania ambaye ataanzia pale Maximo alipoishia.

Mkuu kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa correlation kati ya kuwahi kuwa mchezaji na kuwa kocha mwenye mafanikio. Kuna mambo mengi ambayo unatakiwa uwe na ptactical experience kabla ya kuya-analyse kwa lay men kama mimi. Soka ni zaidi ya kuangalia kwenye luninga au kujua idadi ya wachezaji uwanjani, na kucheza football kwenye computer game. Analysis za Sappi sio technical na hazioneshi practical experience ya analyst, kwa hiyo ndio maana nyingi ziko ill.

Kama unafahamu ukweli kuhusu makocha wetu hata siku moja usingesema. Ufisadi unaolalamikiwa hapa pia uko hata kwenye soka. Kuna Kocha mmoja amabye anasifiwa sana leo hapa TAnzania, aliivuruga timu nzima kutokana na tabia yake ya kutembea na wake wa wachezaji wake, kuna mwingine amewahi kunitamkia kabisa kuwa huwa anachota hela anazopewa kwa ajili ya wachezaji. Na hiyo ni karibu kwa makocha wengi wa hapa Bongo. Wao wenyewe hawana nidhamu, kwa hiyo wanashindwa kuunda timu zenye nidhamu.

Tunajaribu nje, kwa tunafahamu kilichopo nyumbani.
 
Back
Top Bottom