Sappi yuko sahihi kuhusu uwezo wa Maximo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sappi yuko sahihi kuhusu uwezo wa Maximo?

Discussion in 'Sports' started by Bongolander, Feb 26, 2009.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Wapenda michezo JF naomba msome makala hii fupi niliyoinukuu toka kwenye tovuti ya gazeti la Mwananchi.

  Kwa ufupi nimesikitishwa na ufafanuzi finyu wa Sappi ambaye anaangalia udhaifu wa kocha bila kuangalia udhaifu wa muundo mzima wa FA ulioifanya Tanzania iwe kichwa cha mwendawazimu na wachezaji kuwa wa kiwango cha chini kwa muda mrefu.

  Huyu mpenda michezo naona amesahau kuwa club ziewahi kuwa na makoca kutoka kwenye maeneo ya hizo nchi lakini wote walishindwa kufaya kazi kutokana na miundo mibovu ya klabu, ambayo inafanana kabisa na ya FAT. Maximo amejitahidi kufika hapo alipo leo anaonekana hana uwezo, sijui ana suggest nini?

  Sijui kama anafahamu kuwa mafanikio ya timu hayatokani na kocha peke yake, tunaweza kumchukua hata Maurinho lakini bado tutakuwa hovyo.


   
 2. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Huyo hana shukrani hata kwa Rais aliyemwajiri kocha huyo.

  Aende akafundishe yeye Taifa Stars tuone ataifikisha wapi. Wabongo tumezidi sana longo longo mara ooh! Kesho utasikia Oooh! Mfumo wa soka la sasa hivi unaweza kulilinganisha na enzi za akina Ndolanga au Rage?

  Inatubidi tukabiliane na changamoto jamani. Uingereza inasifika kwa kupenda soka duniani mbona wameajiri kocha wa nje? Ina maana hakuna makocha wa ndani wenye sifa na ujuzi?

  Mimi nadhani bwana Sappi angekuwa more analytical "yakinifu" kuhusu anachokizungumza kwa kuweka data na sio kupiga domo.
   
 3. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  I hate hawa wanaojiita soka analyst......huyo sappi namjua hana lolote la kitaalam zaidi ya kukaa vijiweni na kubishania simba na yanga.....na kuna yule Dr riki nae hana lolote zadi ya kujua beckam kavaa nini leo......

  ........mie napenda sana mtu anaebadilika yaani hawa mara nyingi unamsikia anaifananisha taifa stars na arsenal au bila kujua mazingira ya soka letu yakoje.....
  marcio kajitahidi sana kaweza kuifikisha leo hapa timu anafaa kupongezwa.....huyo sappi kwanini asiamue kufundisha watoto wadogo soka bure ili kuinua vipaji sio kupiga domo chanel ten......
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huyu ndo wale wenye hangover za U Yanga na Simba...
  nimewaangalia starz jana kwa kweli Maximo amefanya kazi nzuri. wachezaji wanacheza kwa kufikiri..wanatumia angalau akili ya soka japo sijui mfumo mwingine wa elimu(formal) kama wameipata walio wengi pia ukichukulia umaskini wetu.

  kocha amejitahidi sana na natumai confidence alopata toka kwa Raisi na some tff leaders wanaopenda mabadilko endelevu.

  hofu yangu ni kwamba bado tunajaribu kuijenga FA yetu then vilabu vyetu bado havijaelewa maana ya sound mgt principles achilia mbali wanachama wake hawana dira ya vilabu vyao.

  ukiiangalia kwa makini tff wameweza kukaa na maximo kutoka na kwamba Raisi ndo kaamua kocha ndo huyoo.
  siamini nchi ambayo tumeweza kuwa sasa na kiwanja cha kisasa ambacho pamoja na kuwa very good source ya income kikisimamiwa vema na political will ya kuendeleza soka inabidi tusonge mbele.

  huu uyanga na usimba na wale wanaojiita ni watu wa MPIRA vitatumaliza.
  programu ya kuendeleza soka iwe wazi na ifuatwee... tunakubali kuna watu wanataka kuendesha maisha yao kupitia vilabu ila wawe na uwezo wa kuongoza na wawe WAWAZI.

  Maximo amefanya vema na ameshatambua siasa zetu za soka tusubirie huenda akaongeza kale kamktaba klalichobaki na tff wajipange kioungozi vema.
   
 5. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Jamani jamani, hivi hamuoni kwamba Maximo ni failure????. nashangaa sana wachangiaji humu wanavyosema ati hatuna shukurani kwa alipotufikisha Maximo. katufikisha wapi????, Hivi wewe ikiwa safari yako ni ya kufika Dodoma na ukanunua vyote vinavyoweza kukufukisha Dodoma, na mwishowe ukaishia Chalinze hata morogoro hujafika utajisifia kufika chalinze tena kwa wiki mbili badala ya masaa tu?
  nasema hivyo ajili Maximo kapewa kila alichotaka na hata zaidi kutoka kwa TFF na wadhamini na wadau wengine lakini mafanikio ni 20% ya alichostahili kufanikisha je tumsifu, hivi do we need 20% of performance from him kwa support anayopata?.
  Mfano mdogo tu kama mtakumbuka enzi za Serengeti boys na Kibadeni wakitembeza bakuli kupitia ITV na matokea yalionekana kwa muda mfupi tu, sasa hivi tunawachezaji maarufu waliotokana na serengeti boys na hata maximo anawatumia baadhi.
  Hakika sijaona kikubwa alichofanya Maximo.
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hawa ni watu tunaosema kila siku wanaombea mabaya kwa nchi ili wapate kupeleka mikono kinywani. Mtu kama huyu anayejiita soka analyst ana utaalam gani hasa aliosomea kwenye fani hii inayomfanya awe kifua mbele kumshutumu mtaalam?.

  Je huyu Sappi aliisha wahi kucheza mpira?, aliisha wahi kuongoza hata timu ya chekechea?, aliishawahi kuwa mwalimu wa timu yoyote ile?, kama majibu ya maswali hayo ni hapana basi huyu ni mtu wa kumpuuza kabisa. Kama ni ndiyo tumuulize mafanikio aliyoleta yeye mchambuzi uchwara. Huwezi kuwa mchambuzi wa kitu usichokijua radha yake, bali huo utakuwa ni ushabiki wenye lengo la kuangusha.

  Tanzania kwa muda mrefu sana tumekuwa "wanasiasa wazuri sana wa mipira" yaani kila kitu tunajua isipokuwa uwanjani tu ndiyo tunatoka na visingizio kibao. Sasa leo Mtaalam amekuja watu wanaona uwezo wake umefika kikomo, hivi unatarajia mwalimu darasani amfundishe mtoto kutumia Calculator wakati hata namba hawezi kuhesabu na hajui kuziandika?, itabidi amfundishe kwanza kuhesabu na kuandika ndipo aingia hatu ingine, sasa sisi bado tupo kwenye SURA YA KWANZA, ni pale tutakapofuzu hapa tulipo basi mwalimu ataoa umuhimu wa kuanza SURA YA PILI
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ho.. Ho... Ho.........

  Kama kusema kwamba mtu hana uwezo ndio kukosa shukrani au ukisema hivyo inabidi upewe hiyo nafasi tuone utafanya nini then tunapotoka

  Kila mtu ana uwezo wake, na wengine kazi yao ni kuangalia uwezo wa watu, Sappi hajakosea (unless wewe si mpenzi wa michezo) hata Ramos aliondoka Spurs, Hullier aliiacha France nk.

  Kama umeangalia Stars mechi sita zilizopita, hakuna jipya ni watu wamefikia peak ya mbinu....

  Hii ya ukikosoa basi fanya wewe ni kiboko... kwa jinsi tunavyomkosoa JK!! kila mtu angepangiwa siku ya kuwa rais wa TZ

  The bottom line is SAPPI IS RIGHT, BUT WHO ELSE CAN DO BETTER THAN MAXIMO? AND IS THERE ANY ONE BETTER WITHIN TZ AU WE HAVE TO LOOK OUTSIDE THE COUNTRY?
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  NI maoni mazuri mkuu na una haki ya kuyatoa, lakini nikiangalia rank ya timu yetu ya taifa na soka inayochezwa ikilinganishwa na kabla ya yeye kuja nadhani nina kila sababu ya kuona Maximo amepata mafanikio. Sikumbuki lini timu yetu ilishinda west Africa kabla Maximo hajaja, sikumbuki lini Sappi alitoka na kupinga ufisadi, mizengwe na porojo zilizokithiri FAT, leo anaeda kwenye vyombo vya habari na kuanza ku-criticize mafaniko kidogo yanayoonekana. Kama tukianza kuwa na lay men arguments kama za kina Sappi na Ricky basi JF itakuwa ina haribu credibility yake. Kama wewe umepima na umeona perfomance yake ni 20% naona ni better kuliko 5% au below hapo iliyokuwepo kwa zaidi ya miaka 30
   
 9. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wabongo tunajua kubwabwaja tuuu huyu Sappi na wenzake wote mfano wake wazushi tuuuu. Maximo kwa uwezo wake amejitahisi sana na hata hapa tulipofika sasa nafikiri anahitaji pongezi sana.
   
 10. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  uwezo wa maximo ni mdogo sana, we kocha gani miaka miwili hana first eleven wala formation hana. jamaa ana support kubwa sana lakini ndio uwezo wake umefikia kikoma. mafanikio tunayoyapata ni sababu ya juhudi binafsi za wachezaji.
  Amekataa kumwita Kaseja ambaye i believe ni TZ 1.
  Alimwita Mrisho Ngassa kwa kulazimishwa sana
  Amewakataa Mwakingwe akamng'ang'ania Mapunda ambaye alitu-cost sana.
  Halafu Brazilian hawana records za mafanikio Africa, wape Wafaransa, Germany,Soviets n Africans
  MMSIMKUBALI KABISA HUYO MAXIMO
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mkuu mimi nashangaa huyu jamaa amepata wapi akili hiyo au maneno hayo ya kumkejeli Maximo, naona anadhai kila mtanzania ni mtu wa sog na porojo. Nadhani wenye akili timamu tumeona kuwa Maximo amefanikiwa. Sio siri tunapenda na sisi siku moja tuwe kwenye world cup, lakini ni lazima tuanzie chini kwanza. Hata kama tukienda leo world cup tunaweza kutia fora kwa kufungwa, naona hilo ndi analotaka Sappi, sijui anazungumzia soka kutokana na kusoma kwenye magazeti au kuangalia luninga, inaonekana hajua anachozungumza na yeye si msemaji wa watanzania.
   
 12. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Maximo amatufikisha katika fainali adhimu huko Ivory Coast na mara ya mwisho kufika huko ilikuwa 1980.Hii ni kazi nzuri.
  Tumeweza kufika huko baada ya kuzifunga timu za Kenya,Uganda na Sudan na jan tu tumewakandamiza wenyeji wa CHAn na kujipatia point 3.

  Lini tuliwahi kufanya vitu kama hivi?
  Maximo ameonesha kwa vitendo kuwa Watanzania wanaweza kufundishika wakashinda!na kama ni soko sasa hivi amekwishajiweka katika hali nzuri ya kutakiwa na timu nyinginezo Afirka na duniani.

  Alitukuta hatuna lolote na akatufikisha mahali tulipo na tunajivunia matunda yake.So..Sappi hana hoja hapa!
   
 13. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Tatizo alilolianisha Sappi si la kimpira, tatizo lake kubwa ni 'Ubrazili' wa Maximo, ina maana Maximo angekuwa Mfaransa au Mserbia basi jamaa angemkubali- which doesnt make sense at all!
  Kinachohitajika kwa Maximo ni muda, niliwahi kusema hapa kwamba it will take at least 10years kuanza kuvuna matunda ya kazi anayoifanya sasa. Ikumbukwe kwamba jamaa alipoanza kazi taifa stars ilikuwa imejaa mizee na alikuwa na kazi ya kujenga kikosi kipya kabisa, sasa kina Tinocco wanawapika vijana wadogo kabisa ili watufae baadae. Akitimuliwa na kuondoka, yeyote atakayekuja atakuwa na programs zake na ataanza mwanzo and to me this will be a step back, tutakuwa hatuendi mbele bali kurudi nyuma.
   
 14. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Bwana Sappi kama kwa namna yoyote unaweza kupata ujumbe huu ni vizuri ukaelewa haya. Soka sio kocha peke yake, kuna mengi sana yanayohitaji kushughulikiwa toka TFF mpaka kwenye klabu. Kama wewe ni mahamasishaji basi ungeanza huko ambako ndo kunajenga msingi wa yote tunayoyaona juu.
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Huu sasa ni ushabiki na si kujenga. Huyo Tanzania 1 wako ndiyo anafunga magoli. Mbona DIHILE ni kipa mzuri tu na ninakuhakikishia tukisonga mbele atakuwa ni kipa bora wa mashindano.
   
 16. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu Sappi nadhani bado yuko kwenye zama za kuongea bila ya kufanya utafiti wa kutosha. Laiti kama angeamua kufanya utafiti kabla ya kuongea sidhani kama angethubutu kuyaongea hayo ambayo yamesikika.

  Mifano anayoitoa hailingani kabisa na hali halisi ya kiuwezo katika fani nzima ya kandanda kati yetu na hao anaowafananisha. Brazil ni taifa ambalo linaheshimika kwa miongo kadhaa katika uwezo wake kisoka. Pia Brazil ni nchi ambayo imewekeza kwa kiwango kikubwa katika soka na elimu ya soka kwa wabrazil.

  Sappi pia anasahau kuwa kiwango chetu cha uwekezaji katika soka na elimu ya soka kwa watanzania ni kidogo mno na hakiwezi hata kulinganishwa na nchi zilizokwisha piga hatua katika soka kama Uingereza, Spain, Portugal etc.

  Kama tutakumbuka, wakati Maximo anaingia nchi kuanza kazi alieleza program yake kupitia katika vyombo vya habari. Moja kati ya concerns zake ni kutokuwa na programu za maendeleo ya soka la vijana katika ngazi za vilabu, kwa kifupi ni kwamba alivitaka vilabu kuanzisha programu hizo ili kukuza kiwango cha mpira. Vilevile nakumbuka Maximo alionya kuwa kwa tathmini aliyoifanya ameona wachezaji wengi wa timu ya Taifa hawafundishiki kwa urahisi tena kutokana na umri na uwezo wao waliofikia. Alibainisha kuwa itachukuwa muda mrefu kuifanya Tanzania iwe katika uhakika wa kiwango kizuri na bora ambapo alisema inaweza kuchukua hata miaka hadi 15 - 20 kuanzia wakati ule.
  Maximo alisema kuwa wachezaji wa kutumainiwa hapo baadae ni vijana walio katika umri wa chini ya miaka 15. Hapa ndipo watanzania kama akina Sappi hawataki kupafanyia kazi na kujituma, tulitakiwa bila ya kungojea mradi wa Tinoco kumalizika wananchi tuanze kuwekeza katika kutoa elimu ya soka kwa vijana hawa wadogo ambapo hapo baadae hata ukimleta Mourinho au Wenger basi ajue anataka kushinda kwa namna gani. Lakini kama hatuangalii huko na badala yake tunatoa porojo hatutafika mbali.

  Angalizo:Mradi wa Tinoco unapaswa kuwa na kikomo, je vilabu na wadau wengi wamefikia wapi sasa hivi? kwani somo limeshatolewa, tumejifunza nini au tumefikia hatua zipi?
   
  Last edited: Feb 27, 2009
 17. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2009
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  Akhsante Waungwana Marcio Maximo, hana tatizo ktk idara Zote MuhimuUdhamini Pesa Malazi Vitendea Kazi Ungwaji Mkono nk. Lakini ikubalike katlka historia(kama itakuwa ina nafasi hapa)na takwimu Makocha Wa Kibrazil hawana Rekodi nzuri katika medani ya soka afrika Mpaka Napochangia kumbukumbu zinaonyesha Mbrazil pekee Mwenye Mafanikio Ni Jose Faria(Baadae aliitwa Jaffar Faria) Mwalimu Wa Lion of Atlas Morroco Mwaka 1985-1988 mafanikio yake ni kuifikisha Hatua ya pili Morrocco katika fainali Za Kombe la Dunia 1986 Mexico Hakuna Zaidi Ya huyo Alieishia kutupiwa Virago kwa Aibu baada ya kutolewa katika Nusu Fainali Ya CAN 1988 Na Cameroun Huku Morroco wakiwa Wenyeji.Makocha Waliopita Hapa Tanzania Kutoka Brazil Ni Moreira"Wonder"Foreirra(Yanga)Mafanikio 0 Clouves Oleveira(Taifa Stars) 0 Sijui Mpaka Sasa Nader do Santos(Simba SC Azam FC) Na Nilsein(Simba SC)
   
 18. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tumekusikia Mkuu, lakini analysis yako haijakamilika, tuelezee
  -viwango vya wachezaji wetu katika ngazi za vilabu
  -Programu za kufundisha wachezaji katika umri unaohitajika
  -Tupatie analysis ya umahiri wa viongozi kwenye vilabu
  -Nipatie top 10 ya individual or collective efforts za sisi watanzania wenyewe ambazo zilishachuliwa kuendeleza soka la vijana wa umri wa chini ya miaka 15
   
 19. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #19
  Feb 27, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ,,,Mmh lakini wazee hata mimi huwa najiuliza sana,hivi wachezaji wetu wa Tanzania,mbona hizi skills za kawaida tu za ki futball ie,Controlling,Driballing hatuzioni kwa wachezaji wetu,yaani mchezaji wa STARS akipewa mpira utafikiria kapewa KAA LA MOTO,ni haraka sana kwa mwenzake au kuutoa nje,na hili ndo linatufanya kila siku kwa tunaoungalia mpira tujione kama hatujui hivi,Kwanini kocha MAX,na kukaa kooote huku na timu hii,Hawezi kuwapa wachezaji wake KUJIAMINI,hiki nikitu hata mimi na wasiwasi nacho,Ndio RESULTS ina matter,lakini tunataka wachezaji wetu wajisikie HURU kidogo,pewa pasi,tuliza,vuta moja mbili,geuka huku,maguu mawili matatu kama ya RONALDO,then release mpira.
   
 20. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu King Zenji,
  Soka ni profession kama zilivyo professions zingine. Ndani ya professional unaweza kuwapata watu ambao wanavipaji. Kwa hiyo kitu ambacho tunakikosa hapa kwetu ni kwamba mafunzo ya soka yanaanzia ukubwa kwenye umri mkubwa wakati mwiingi ni over 20 years, this is weird. Mafunzo ya msingi kabisa huanziakwa vijana wakiwa na umri mdogo from 8 years. Ndiyo maana leo hii umeweza kuona matatizo kwa wachezaji wa timu ya taifa ambayo hawakutakiwa kuwa nayo in any way. Tunategema kuwa mchezaji wetu ambaye ataitwa katika timu ya taifa awe ni mchezaji alikamilika, anakwenda kwe timu ya taifa kupanga mbinu ya kucheza kitimu na wenzake ili waweze kushinda.
  It is very sad kwamba kwahali ya viwango vya wachezaji wetu na kutaka kuwa na walau ushiriki wa timu ya taifa katika mashindano mbalimbali basi inatubidi tuchukue wachezaji wenye afadhali wafundishwe katika timu ya taifa. Lakini endapo kama tungekuwa na base ya vijana waliotayarishwa na kupewa mafunzo tangu wakiwa na umri mdogo basi ni wazi kabisa hata kazi ya kocha inakuwa ni nyepesi. Leo hii tuna makocha wengi sana Tanzania lakini unaweza kunitajia do we have soccer trainers? Do we have Classes for teaching soccer? Do we have syllabus for soccer lessons?

  We need to invest vinginevyo tutaendelea kuvuna tunachokipanda.

  Hatima ya soka la Tanzania ipo mikononi mwetu mimi na wewe, tunaweza kuleta tofauti endapo kama tutaamua kutumia muda wetu wa ziada katika maeneo yetu ku-organize mafunzo ya football kwa vu-ijana wa mtaani kwetu
   
Loading...