ho.. Ho... Ho.........
Kama kusema kwamba mtu hana uwezo ndio kukosa shukrani au ukisema hivyo inabidi upewe hiyo nafasi tuone utafanya nini then tunapotoka
Kila mtu ana uwezo wake, na wengine kazi yao ni kuangalia uwezo wa watu, Sappi hajakosea (unless wewe si mpenzi wa michezo) hata Ramos aliondoka Spurs, Hullier aliiacha France nk.
Kama umeangalia Stars mechi sita zilizopita, hakuna jipya ni watu wamefikia peak ya mbinu....
Hii ya ukikosoa basi fanya wewe ni kiboko... kwa jinsi tunavyomkosoa JK!! kila mtu angepangiwa siku ya kuwa rais wa TZ
The bottom line is SAPPI IS RIGHT, BUT WHO ELSE CAN DO BETTER THAN MAXIMO? AND IS THERE ANY ONE BETTER WITHIN TZ AU WE HAVE TO LOOK OUTSIDE THE COUNTRY?
Sawa wewe unaweza ukaona kuwa Taifa Stars haijafikia lolote kimpira kutokana na mtazamo wako au labda unaangalia premier league za ulaya na unataka kuzilinganisha na kwetu. Kimsingi hawa jamaa wa Taifa Stars na huyu kocha wamejitahidi sana alikuwepo Bukhard Pape wa Ujerumani sijui wamkumbuka? Alifanya nini? Alikuja Colvis Oliviera alifanya nini? Kaja Maximo akabadilisha walau kidogo mnaanza kutukana. Mpira jamani ni nidhamu hata hao wachezaji wenyewe siku hizi wanalilia kuchezea timu ya taifa. Zamani thubutu! Kwa hiyo Maximo anastahili pongezi tena sio za kubeza. Hawa vijana confidence yao imepanda maradufu.
Point of correction - sijatukana mtu hapa kwahiyo unaposema "mnaanza kutukana nadhani unapotoka
sasa basi... I dont agree with you; kinachofanya wachezaji wetu waamke zaidi ni motivation ya kwenda professional (na hii ni rahisi zaidi kwenye national teams kwasababu kwenye vilabu our chances are limited); level ya government support na sponsorship haijawahi kutokea hivyo once again mchezaji anafanya juhudi za binafsi za ziada; vilevile mwamko wa watanzania umekuwa zaidi kwenye national team baada ya kuona vilabu vinanunua mno ushindi
Labda nikuhabarishe kidogo, ndiyo naangalia sana premier ni supporter wa liverpool na naangalia sana ligi yetu na ninasupport Simba na siku za karibuni na-support JKT ruvu kwasababu kuna vijana wanapewa nafasi na kuna nidhamu
kUMBUKA YANGA SIMBA WALIFANIKIWA KWENDA QUARTER FINALS NA SEMI FINALS ZA AFRICA SABABU YA MOTIVATION
The bottom line ni kwamba: Maximo came at a right place, in a right time so he is lucky, we have a new stadium, our president likes football (which in a way is also a campaigning tool), watanzania WAMEfocus kwenye national team kuliko yanga na simba, wachezaji wapo kwenye era ya opportunities - akionekana national team anaweza kupata professional contracts KIURAHISI KULIKO VILABU VYETU KWA SABABU ZILIZO-OBVIOUS, WAKIWA TAIFA wanapata allowances vizuri, motivation, respect na sponsorship
FOOTBALL IMEKUBALIWA KAMA PROFESSION NA SIO RIDHAA... KAMA ENZI ZA BURKHAD PAPE, JOEL BENDERA, SYLESAID MZIRAY, ETC.ETC.
Mkuu sina hakika kama kweli unachokiongea unakifahamu. Mpira kuwa profession au amature sio sababu ya mafanikio ya kocha. Kama utakumbuka best perfomance ya Tanzania katika historia yetu ya soka ilikuwa wakati mpira sio profession. Wakati uwanja wa taifa ni uo huo uliokuwa wa gwaride namaadhimisho ya siku za taifa. motivation ilikuwa almost zero. Hii unaielezeaje?
Unakumbuka kuwa mabadiliko ya soka Tanzania ambayo walau sasa tunaona imefufuka, yalianza na mabadiliko ya uongozi wa juu wa FAT? Kupata kocha mgeni sio mara ya kwanza na mazingira hayana tofauti sana kati ya makocha wote, tofauti kubwa ni kuwa uswahili TFF umepungua sana, hata kuingiliwa kwa kocha kumepungua sana, japo kuna wengine wanaendelea kujaribujaribu bila mafanikio. Umetaja Burkhard Pape, Oliveira, ukamsahau Stanculescu.. unataka kutuambia kuwa hao hawakufanikiwa kwa sababu hatukuwa na uwanja mzuri, au kwa kuwa walikuja kwenye wrong time?. Ipi ni wrong time kwako na ipi ni right time.
Lazima tukubali Sappi amemkosea heshima Maximo na amekosa shukurani, lazima aheshimu mafanikio madogo yaliyonekana. Tutakuwa ni watovu wa shukurani kama tukimponda Maximo kwa kitu tulichoshindwa kufanya kabla yeye hajaja.
Wapenda michezo JF naomba msome makala hii fupi niliyoinukuu toka kwenye tovuti ya gazeti la mwananchi. Kwa ufupi nimesikitishwa na ufafanuzi finyu wa Sappi ambaye anaangalia udhaifu wa kocha bila kuangalia udhaifu wa muundo mzima wa FA ulioifanya Tanzania iwe kichwa cha mwendawazimu na wachezaji kuwa wa kiwango cha chini kwa muda mrefu. Huyu mpenda michezo naona amesahau kuwa club ziewahi kuwa na makoca kutoka kwenye maeneo ya hizo nchi lakini wote walishindwa kufaya kazi kutokana na miundo mibovu ya klabu, ambayo inafanana kabisa na ya FAT. Maximo amejitahidi kufika hapo alipo leo anaonekana hana uwezo, sijui ana suggest nini? Sijui kama anafahamu kuwa mafanikio ya timu hayatokani na kocha peke yake, tunaweza kumchukua hata Maurinho lakini bado tutakuwa hovyo.
Date::2/25/2009
Maximo adaiwa hana uwezo zaidi ya hatua aliyoifikisha Taifa Stars
Na Mwandishi Wetu
MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Hussein Sappi amesema tukubali ukomo wa kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo na staili ya soka anayofundisha timu haiwezi kufika mbali.
Akizungumza katika kipindi cha Kumepambuzuka cha Radio One jana, Sapi alisema makocha wa Brazil wengi hawana rekodi katika ulimwengu wa soka zaidi ya nchi yao.
Alisema Brazil wazuri kwa wao wenyewe lakini hawana rekodi nzuri duniani.
Mimi nadhani wakati umefika sasa tubadilike, tuangalie Ulaya Mashariki, kule tunaweza kupata makocha wazuri na hata soka yao inajulikana.
Tunakubali kuwa Brazil wana makocha wazuri lakini kwa faida yao, wapi kuna mafanikio kwa kocha wa Brazil? Tunaona Afrika Kusini inavyoyumba.
Kulikuwa na Felipe Scolari, alikuwa Ureno, hakuna kitu, kaondoka akaenda Afrika Kusini, akatoka akaja Chelsea, na sasa hayupo, kuna nini pale. Angalia makocha wa Hispania, Ufaransa, Uholanzi, Russia, Jamhuri ya Czech wapo na naamini tunawamudu..., alisema.
Akizungumza huku akionyesha kukerwa, alisema: Isije kufika wakati tukapigana mawe Uwanja wa Taifa pale, mimi hili nalisema kama Mtanzania mwenye haki ya kuzungumza langu na sidhani kama Maximo anatufaa tena, alisema.
"Maximo came at a right place, in a right time so he is lucky, we have a new stadium, our president likes football"
there you are, kila siku nawaambia watu kuwa Maximo alikuja wakati muafaka kabisaa kipindi ambacho kuna kila aina ya support kutoka kwa wadau mbalimbali serikalini na kwenye chama cha soka chenyewe. Mimi sidhani kama kuna kocha aliyewahi kupata support kubwa kama hii. Nakumbuka kipindi akina Boniface Mkwasa na wenzake wanalalamika kuwa wanapeleka programme zao a mazoezi kwenye football association lakini timu inaitwa kambini wiki moja kabla ya mashindano husika. Pia kwenye suala zima la maandalizi hivi iliwahi kutokea lini national timu kupelekwa nje ya nchi kwa kambi mfano kama ilivyopelekwa Brazil na Denmark? Mimi sijawahi kuona wala kusikia mpaka Maximo amekuja. Pia hata suala la malipo kwa kocha mwenyewe linahusika sana. Hivi mnajua mshahahara wa Maximo? Hakuna kocha mzalendo aliyewahi kulipwa huo mshahara halafu on time na sio kwa kubabaishwa kama ilivyokuwa hapo nyuma. Tuwaulize akina Mkwasa, Mziray, na wengineo inawezekana hadi leo wanadai masurufu yao. Kwa hiyo kimsingi ni wakati tu umempenda bwana Maximo na mimi naamini hata kocha mzawa angepata support hii kubwa kiasi hiki angeweza kufanya mambo mkubwa pia.
Hakika hii inanithibishia kuwa waTanzania tu wepesi sana wa kudanganyika kwa fulana, upande wa kanga na kilo ya sukari unatoa kura yako.
Maximo ashukuru ameingia kipindi muafaka kakutana na bahati angekuta kipindi Taifa Stars wanaenda mazoezini kwa daladala na kambi zisizo na maji ya kuoga ndio mngeona ni nini tunaongea hapa. Kwa support aliyopata tulitarajia makubwa zaidi ya haya. alipaswa kuleta mageuzi mengi sana katika soka. Kocha gani tuliyewahi kuwa naye ambaye angeweza hata kuonana na waziri mkuu ndani ya wiki moja achilia mbali yeye mwenye direct mawasiliano na Rais. acheni kumsifia mtu. Hakika matunda ya mafanikio haya ni ya Support ya Wadhamini pamoja na Wadau wengine yeye anamchango mdogo sana hapo.
Hakika hii inanithibishia kuwa waTanzania tu wepesi sana wa kudanganyika kwa fulana, upande wa kanga na kilo ya sukari unatoa kura yako.
Maximo ashukuru ameingia kipindi muafaka kakutana na bahati angekuta kipindi Taifa Stars wanaenda mazoezini kwa daladala na kambi zisizo na maji ya kuoga ndio mngeona ni nini tunaongea hapa. Kwa support aliyopata tulitarajia makubwa zaidi ya haya. alipaswa kuleta mageuzi mengi sana katika soka. Kocha gani tuliyewahi kuwa naye ambaye angeweza hata kuonana na waziri mkuu ndani ya wiki moja achilia mbali yeye mwenye direct mawasiliano na Rais. acheni kumsifia mtu. Hakika matunda ya mafanikio haya ni ya Support ya Wadhamini pamoja na Wadau wengine yeye anamchango mdogo sana hapo.
[COLOR="Blue[B]"]...Mkuu, hapo naomba tutofautiane kidogo. Haya makubwa tuliyotaraji ulitaka yapatikane kwa kipindi gani? Ndani ya Miaka mitatu tuliyokaa na Maximo? Maandalizi yetu kwa ajili ya hilo yalikuwaje? Unafahamu kwamba tungeweza kudai hilo iwapo tu tungekuwa na mfumo unaoeleweka wa wachezaji chipukizi na kwa hiyo Maximo angefika tu na kuanza kuvuna na kuunda kikosi kabambe cha timu ya Taifa? Tunadai makubwa kuliko haya wakati kocha alilazimika kuanza kufundisha hata namna kudribble mpira wachezaji wenye umri mkubwa?? Fair Play Please, kwa Maximo![/B][/COLOR]
Maximo anastahili pongezi. Kaleta heshima ndani ya timu. Kuna baadhi ya wachezaji walikuwa wanajiona wao ni Timu ya Taifa, panga pangua wataitwa. Ila jamaa kaliondoa hilo, na ni zuri sana manake kasaidia wachezaji kujituma. Mtu anateuliwa kwa kujituma na jinsi atakavyozidi weka jitihada akiwa ndani ya timu. Tunaposema Maximo kapewa kila kitu hatutendi haki, sasa kumjaribu tulitaka atembee kwa miguu na wachezaji watoke nyumbani kwa dala dala kuja mazoezini?, kila wakati una raha na karaha yake. Hivyo wakati wake wachezaji na timu kwa ujumla imeweza kupata angalau kila kitu. Hongera Maximo, unatutoa kimasomaso kutoka katika kuwa Kichwa cha .......